Waandamanaji wachoma moto Biashara za Wabunge zikiwemo Hotel, Maduka na Mabasi, Ofisi ya Kimani yateketezwa!

Waandamanaji wachoma moto Biashara za Wabunge zikiwemo Hotel, Maduka na Mabasi, Ofisi ya Kimani yateketezwa!

Sasa kuiba hadi Siwa huo ni uporaji,maandamano yanatakiwa yawe ya AMANI kama sisi CHADEMA.

Sasa watampa Ruto sababu ya kuingiza Jeshi Barabarani.
Nani kakwambia jeshi ndio suluhisho? Bado una akili za kijima sana.

Nguvu ya umma haijawahi kufeli popote ulimwenguni hata umwage wanajeshi kila kona ya miji haitasaidia kitu.
 
Nani kakwambia jeshi ndio suluhisho? Bado una akili za kijima sana.

Nguvu ya umma haijawahi kufeli popote ulimwenguni hata umwage wanajeshi kila kona ya miji haitasaidia kitu.
Nilichokuwa nasema ni hivi Waandamanaji wakianza kuvunja Maduka kupora na kuchoma moto watampa sababu Ruto ya kutangaza hali ya hatari na kuliingiza Jeshi kwa kisingizio cha kurejesha Amani.
 
Hii sasa ni mbaya jamani Biashara za Mbunge ni za kifamilia

Waandamanaji Nchini Kenya wameharibu Mali na Biashara mbalimbali za wabunge waliopigia Kura ya Ndio Finance Bill

Aidha Ofisi za Kiongozi wa Walio wengi Bungeni mh Kimani na zile za Gavana wa Nairobi zimechomwa moto

Mali hizo zimeoneshwa na Citizen Tv zikiteketea

Wanadai Zakayo Ashuke

PIA SOMA
- LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi
hivi tuwe wakweli, hivi demokrasia ndio hii? uhuru wa kuandamana ni huu au ni ule wa kutoa maoni bila kuumiza wenzako. sidhani kama wanajenga kitu.
 
Back
Top Bottom