PreGE2025 Waandishi Habari Wasiothibitishwa hawatoruhusiwa kuripoti uchaguzi mkuu 2025

PreGE2025 Waandishi Habari Wasiothibitishwa hawatoruhusiwa kuripoti uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa habari (JAB) imesema waandishi wa habari ambao hawatakuwa wamethibitishwa na ithibishwa ni bodi hiyo hawatoruhusiwa kutekeleza majukumu yoyote yanayohusiana moja kwa moja na mchakato wa uchakuzi mkuu 2025.

Kundi hilo la waandishi wa habari linajumuisha Wahariri, Waandishi wa kujitegemea (freelancers na correspondents), watangazaji wa Radio na Televisheni, Wapiga picha, Waandaaji wa vipindi vya habari (News producers) na Waandishi wa habari wa kigeni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 22,2025 na bodi hiyo kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Patrick Kipangula, waandishi wote wanatakiwa kujisajili kabla ya 21 Juni, 2025 kwa kufuata vigezo na masharti.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ili kukidhi vigezo kwa mujibu wa Kanuni za sheria ya huduma za habari, tangazo la serikali Na.18 la Februari 3, 2017 waandishi hao watahitaji kuambatanisha vyeti vyao vya elimu kuanzia diploma vilivyothibitishwa na mamlaka husika.

Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo imetaja mahitaji mengine kuwa ni pamoja na picha ndogo, utambulisho wa taasisi anayotoka, namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA), namba ya simu, barua pepe pamoja na ada ya ithibati Sh.50,000.

Bodi hiyo imewasisitiza waandishi kutumia muda huo uliotolewa kuhakikisha wanajisajili na kuthibitishwa kupitia mfumo wa TAI.
Hakuna uchanguzi kuna maigizo
 
Matokeo ya magufuli hayo hayo ndiyo yatakayotangazwa
Hiyo nusu trillion waliyopanga kutumia kwenye hili igizo ingeelekezwa kuimarisha sekta ya afya na elimu kwani matokeo tayari yako INEC.
 
Huelewi wewe.kinachoongelewa hapo ni waandishi wa habari wa vyombo vya habari vilivyosajiliwa sio wambeya wa vijiweni
Ongea kama mwanaume umbea unatoka wapi kwenye mambo ya uchaguzi?
 
Back
Top Bottom