DOKEZO Waandishi wa Habari Azam wanataabika Mikoani, wanahitaji msaada kulipwa stahiki zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Usije ukamshauri mwanao, mdogo wako au ndugu yako wa karibu kusomea UANDISHI wa habari. Ni kazi ya maana ya heshima lakini ya kuja kukutia umasikini tu. Sio cha Azam wala nani; vyombo vya habari Tanzania with the exception of public media houses like TBC nk; kwingine huko hapana
 
Sauti ipazwe haswa, na wao wanahitaji maisha mazuri kama wengine
 
Mjadala wa kitaifa unatakiwa
 
😆😆
 
Na hao ndio tunaaminishwa wana unafuu kuliko wengine.
Niliwahi kufanya field kwenye chombo cha habari (radio) miaka kumi iliyopita, wakati mwingine sisi wa field ndio tulikuwa tunaokoa jahazi ya kuwanunulia vocha na chai tuliowakuta kazini maana hali ngumu.

Baadaye nikafanyaga kwenye gazeti kitengo tofauti na habari, hapo palikuwa na unafuu maana tulikuwa tunakunywa na chai ya bure + 5000 ya nauli.
Baadaye nikaacha kabisa hiyo sekta nikakimbilia kwingine.
 
Pahala popote kazini ama katika taasisi shida inakua sio mmiliki bali ni yule anayepewa mamlaka ya uendeshaji taasisi.
Waswahili tuna roho za korosho sana na ubinafsi uliopitiliza.
Sio tu Azam media,hata upande wa viwanda vya ngano katika usafirishaji/madereva mie nimeshuhudia wakilalamika.
Ila unakuta masikini Bakhresa hajui wala wakuu wa juu hawajui.
Waswahili tuna shida sana kwa kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe.
 
Inataka Moyo
 
Nionyeshe media yoyote ambayo haina matatizo kama haya (Labda TBC ambayo ni Serikali) in short this is a dying industry kwahio inabidi hao wadau wawe wajanja watumie kuwa kwao AZAM na kuvuta kilichopo kila kinapopatikana na hapo hapo kutokusita kufanya freelancer, kuna ma MC kibao sikuhizi wanatumia kuwa kwao kwenye Kampuni fulani kupata tenda za harusi na wengine kufanya vijiblogu vyao kuwa angalau na authenticity kuliko ingekuwa vinginevyo....

That said sekta zote zinapumulia mashine unless una mbinu zako kinachopatikana hakikidhi mahitaji
 
Kwamba wanapewa kidogo kuliko kilichopo kwenye Mkataba ? Sababu akiamua kutoa kingi kwenye kusafirisha hizo ngano, atashindana vipi bei na Mo ambaye yeye labda hatoi kingi kama hicho ? Siongelei Azam per se ila hizi kampuni wateja wao ni shareholders ambao wao wanachojali ni as much profit as possible na sio wametoa welfare kiasi gani (ukiona wanatoa welfare hio ni Publicity Stunt)...

That is the nature of the Beast..,

 
Mkuu nina ndugu amefanya kazi kama dereva hapo Bakhresa group.
Msimamizi wao alikua akiwapunja pesa za posho za kupakua ngano.
Kila trip moja kuna posho inawekwa.
Mathalan kila trip mfano elfu 6.
Msimamizi anakata anaweka kila trip elfu 3.
Ndio maana nikakwambia shida sio mmiliki ni mtu anayepewa kazi ya uendeshaji taasisi.
Embu rudi usome kwa uelewa nilichoandika kaka.
Na nikazidi kuongeza kuwa sisi wenyewe waswahili tunahujumiana.
 
Je hata wakipewa hio Posho ya elfu sita inakidhi hayo mahitaji ? Na mimi rudi kunisoma ndio maana kuanzia mwanzo kwenye media sijazungumzia AZAM pekee bali Industry kwa ujumla na kwenye hili la Kampuni nimezungumzia kampuni zote kwa ujumla in the capitalists environment..., yaani hata hio tatu anayowapa hata kama akitoa mbili kuna watu bado watakuja kuomba kazi..., hivyo huyo msimamizi anakula kwa urefu wa kamba yake kama wanavyofanya wengine..., Au kama mataifa ya Ulaya yanavyo-marginalize mataifa yanayoendelea...

Matsya Nyaya; (Sanskrit: मात्स्यन्याय; IAST: mātsyanyāya) is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish.

 
Nakataa kuamini kwamba bakhresa hajui.

Hajui kivipi?

Tatizo ni kwamba wabongo tunaabudu matajiri.
 
Burudani kwa wote
 
Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe

Wanaleta malalamiko jf kwan akuna vyombo vya kuwatetea na kupeleka malalamiko yao
Kwan akuna sheria za kaz kwan akuna mahakama ya kaz na km sio mahaka ya kaz kwan akuna sheria zinazoeza waruhusu wao kufungua kesi

Ttzo waandishi wengi ni Ccm na akili zao na mawazo yamekaa ki ccm
 
Mchawi wa mswahili ni mswahili mwenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…