Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa


Hakuna cha malengo wala shabaha, hiyo ni rushwa, nasita kukulaani kwa sababu mafundisho ya dini yangu yananikataza kumlaani mtu, lakini kitendo cha rushwa kutowa au kupokea ni laana kubwa sana.
 
Kama inabidi utengeneza pesa kwa njia hata ya haramu, mimi naweza kukusaidia ushauri wa kutengeza pesa za halali kwa njia ya uandishi na hauna wala hautakuwa na haja tena ya kupokea au kugawa vibahasha vya pesa, utakuwa unalipwa ki halali kwa invoice na utaweza kuitetea popote lakini hii? no way.

Matatizo ya mtu kama wewe ni "exposure" uliyoipata, umeyakuta hayo ya vibahasha kwenye industry na ukaiona ndio norm na sasa unajaribu kuitetea ingawa ni dhambi. Tafadhali sana, achana na hizo rushwa, hutokuwa na amani maisha yako.
 
6. Jee Bahasha za "asante"-Takrima nayo ni rushwa?
Nimeruka number 5 ili kumalizia kundi la mwisho la bahasha safi, hizi zinaitwa bahasha za asante, bahasha hizi waandishi hulipwa kupewa asante kwa kazi nzuri walizofanya, hizi ni kama tip au keep change, hazina uhusiano wowote na kuimfluence bali hizi ni appreciation.
Kulitokea news ya mteja mmoja muhimu alikuwa ana news yake siku ya Alhamisi mchana, akataka magazeti 6 ya Kiingereza, Daily News, Guardian, Citizen, This Day, The Express, na The African. Nikamtajia the Bussiness Times, akasema yeye ofisi yake hawalinunui na wanaliona kama lipolipo tuu.

Siku ilipofika nikawapitia hao waandishi waliochaguliwa nikawapeleka, miongoni mwao kukawepo mwandishi wa Bussiness Times nikamwambia gazeti lako halitakiwi, akaniomba sana aje, nikamkatalia taharibu bajeti, akaomba kuja hata bure bila bahasha!, nikamkubalia!.

Kufika pale waandishi wakajitambulisha, ilipofika zama ya jamaa wa Bussiness Times, yule bosi akamzodoa wewe nani kakuita hapa?, kabla hajajibu, nikaingilia kati kuwa nimemleta mimi, bosi akatoa amri aondoke kwa vile hatamlipa, mimi nikamwambia bosi, nitamlipa mimi!. Hoyu bosi akasema kuna vijigazeti vingine viko viko tuu, vinachapishwa na kuishia kufungia samaki na maadazi!. Hata mimi nilijisikia vibaya!.

Akamuita mzungu wake akazungumza saa nzima!, kuja kumaliza jamaa wa Bussiness Times akaniaga, fasta, nikamlinda, akaondoka zake!. Wale wengine wakasubiria bahasha nene, by the time zimetoka ni saa 10 jioni!. Tukaondoka zetu.

Kesho yake asubuhi, boss kanipigia simu kuniambia asante sana, amesikia news yake imetoka lead story front page na picha kubwa full color ila hajui gazeti gani!. Akiwa njiani kuelekea kazini akanunua Daily News, Guardian, Citizen, This Day, The Express na The African. Kutafuta story hakuona kitu!. Akanipigia tena kuniuliza iko gazeti gani?. Nikamwambia bado sijaliona ila nitakwenda ofisi kwake saa 4.

Nikapitia ubao wa Magazeti ndipo nikaona big headline kwenye Bussiness Times!, of all the papers!. Nikalinunua kwenda nalo huku njia nikawapigia wale wengine wote licha ya bahasha nene, there is nothing!, wote wakasema shauri ya kusubiria bahasha, walichelewa deadline, hivyo wataitoa kesho yake!. Kufika ofisi nikaripoti kwa boss sababu ya kuchelewa na kumkabith the BT, alifurahi na kushukuru sana, ila hakukumbuka ndio yule jamaa aliyemzodoa!.

Kesho yake Jumamosi kucheki magazeti yote hamna kitu!. Nikapiga tena simu na kuuliza kulikoni, ndipo wakanijibu story imekaa kibiashara zaidi, hivyo imewekwa bussiness news, Jumamosi na Jumapili hakuna bussiness news!, hivyo nisubirie mpaka Jumatatu, huku mzungu anaondoka Jumapili anataka kuondoka na news clips zake!. Nilalaumiwa nimemlet down!. Ikabidi Mzungu aondoke na clip moja tuu ya BT!.

Jumatatu kweli magazeti mengine wakatoa, sio front page na sio headline!. Wakati wa postmortem na boss akaishukuru sana BT, akanituma nimtafuteb yule mwandishi amuombe msamaha in person na kuamua kumlipa 5 times more as appreciation!. Hii ni bahasha ya shukrani, it has nothing to to na rushwa!. Zile tuzo mbalimbali wanazopata waandishi zikiandamana na bahasha nene, ni shukrani na sio rushwa!. Waandishi wengine hupewa trips za abroad kama asante kwa kazi nzuri. Bahasha hizi za asante ndio kundi la nmwisho la bahasha safi.

Saa hizi usiku umekuwa mkubwa, kesho nitaakia bahasha chafu ambazo ndizo rushwa na ni za kuogopwa kama ukoma!.
 

You are too low kama mwandishi wa habari, kuanza kuingiza mambo ya dini na mambo ya Mohamed Said, tena huyo wala usiseme, huyo ni author wa vitabu, usitake kudanganya watu, wewe ni kanjanja.

Huna zaidi ya kuwa ni mla rushwa na mgawa rushwa na usitake kuingiza mengine kwa kujitetea. Nakuona unaanza kutaka kupoteza mada kwa kuingiza yasiyokuwemo. Na hiyo MoU inayosema kuwa ni kibahasha basi na wewe tuoneshe MoU yako iko wapi?

Too low, nilikuwa nakuona wa maana kumbe msemo "you cant judge the book by its cover" kwako ndio umehitimisha.
 
Pasco,
Nimeipenda story ya Business Times. Sote katika fani hii tunatakiwa kuwa hivyo. Hudhuria press conference, kimbia ofisini na andika story yako to meet the deadline.
 

Una uhakika wa hayo maneno kwenye red?
 

Sasa hiyo ndio hadithi ya bahasha safi, that is total corruption, no more no less. Samahani sana lakini huo ni uozo unaojisifia hapo juu. Sina hata la kusema! Jamani Pasco kumbe ni bigger problem than I thought!
 
FaizaFoxy kalale saa hizi ni usiku mkubwa!. Nakupa tofauti ya bahasha za uwezeshaji na matokeo ya kutowezeshwa unapiga kelele!. Nakudhibitishia hata wewe, wazazi wako wasingekuwezesha na ilmu na Mungu kukujali mume, you never know saa hizi ungekuwa wapi!.

Nakuambia ziko bahasha kwa waandishi wanapewa ili kuwezeshwa kutekeleza majukumu yao, wewe unashiupalia ni rushwa!. Nakushauri muulize maalim suala la uwexzeshaji, mwandishi wa habari ni swa na mwandishi wa vitabu anaelewa maana ya uwezeshaji, wewe huelewi ndio maana kila uwezeshaji kwako ni rushwa!.
Haya nimekubali, mimi Pasco wa JF ni mla rushwa mkubwa!. Haya kalale!.
 

Kutaka kuhalalisha dhambi zake anatupa hadithi za kusadikika zisizo na vielelezo, itabidi uwajibu BBC na CNN na ubalozi wa US kwa kumtaja Obama kuwa mtoa rushwa kwa waandishi wa habari. Nna uhakika watakusoma.

Na hiyo haihalalishi upokeaji wako wa rushwa!
 

Kesho ntakupa darsa kuhusu rushwa halafu wewe uende kwa Maalim wako unaemtegemea akueleze vizuri.

Huwezi kuhalalisha haramu hata uwe nani. Huna zaidi ya dhambi tupu zilizokujaa na leo umejiumbua mwenyewe, kamuamrishe mkeo akalale, usintafute saa hizi.
 
Una uhakika wa hayo maneno kwenye red?
Mkuu Wacha1, hivi ulidhani wale waandishi wanaosafiri na Obama wanasafiri bure, wanakula bure na kulala bure?. Si wanapewa bahasha nene huko makazini kwao! Wanaotoa hizo pesa za hizo bahasha nene ni kina nani?.

Au unatazama na kusikiliza BBC ukijua ni bure tuu kama sadaka?!. Kila aliye Uingereza anakatwa pesa za kusikiliza na kuangalia BBC, usikilize, usisikilize, utazame, usitazame, unakatwa!.
 
Ningekuwa nawategemea kuomba viza, labda ningeogopa!, mama nina viza za miaka mine mine hii ni ya tatu!, bi mkubwa yuko kule, so US is my second home!. Mnamuogopa sana Obama?!.
 
Pasco,
Nimeipenda story ya Business Times. Sote katika fani hii tunatakiwa kuwa hivyo. Hudhuria press conference, kimbia ofisini na andika story yako to meet the deadline.

Huyo alinyimwa bahasha hakungoja! alikatiwa kitu kidogo na Pasco kabla ya vibahasha, mbona hujamalizia?
 
Kwa darsa nitakusikiliza, ila nakuomba na wewe, nikikufikisha mahali ukaelewa kuwa sio kila bahasha ni rushwa, nakuomba ukubali, usiwe king'ang'anizi!
 
Ningekuwa nawategemea kuomba viza, labda ningeogopa!, mama nina viza za miaka mine mine hii ni ya tatu!, bi mkubwa yuko kule, so US is my second home!. Mnamuogopa sana Obama?!.

Hata akiwa wapi, wewe ni mla rushwa na mgawa rushwa ni mtu hatari sana kwenye jamii, na kama mama anayasoma haya nadhani saa hizi matumbo yanamkatika lakini kuna msemo "nyoka hazai kinyonga" inawezekna hii tabia ya kufanya maovu na kujitetea na kutetea maovu ipo kwenye damu. Hata ujitetee vipi leo umejiumbuwa, mwenyeewe.

Lunyungu inabidi nimpe hongera nyingi sana kwa kukutukunyuwa mpaka ukabwabwaja hapa.
 
Kwa darsa nitakusikiliza, ila nakuomba na wewe, nikikufikisha mahali ukaelewa kuwa sio kila bahasha ni rushwa, nakuomba ukubali, usiwe king'ang'anizi!

Mpaka sasa hakuna ulichonikinaisha hata kimoja, na ikiwa itatokea nikaliona, basi mimi ndio wa kwanza kukiri hiyo ni halali yako. Lakini hili la kupewa vibahasha na "source" hata uniambie vipi, haliniingii kabisa.
 
Sasa hiyo ndio hadithi ya bahasha safi, that is total corruption, no more no less. Samahani sana lakini huo ni uozo unaojisifia hapo juu. Sina hata la kusema! Jamani Pasco kumbe ni bigger problem than I thought!

Jamaa is a disaster mi nashangaa hata mnavyopoteza muda kubishana nae,hamtaelewana hata mpaka kesho,dizaini yuko kama mlokole flani hivi,akishaingiza kitu kichwani ni ngumu kukitoa....kila la kheri mnaohangaika nae!
 
Swali dogo kwako, rushwa ni fedha yoyote kwenye bahasha haijalishi ni kwa malengo yepi au rushwa ni fedha inayotolewa kwa malengo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…