Mkuu Ndallo, waandishi uchwala ni wale wanaojifanya waandishi lakini sii waandishi chochote si lolote na wapo wa aina mbili. Aina ya kwanza ni wale waliovamia fani baadaye wakajikuta hawawezi bali wanang'ang'ania uandishi huku wanachoandika hakina mashiko. Waandishi uchwala wa pili ni wale ambao walikuwa waandishi wakajikuta hawana kazi hivyo kuvizia matukio mbalimbali kuwinda bahasha for survival, hawa ndio huitwa makanjanja!.
Mkuu Pasco, wakati nasubiri kusikia habari za bahasha halali na haramu naomba nianzie kwa hoja yako hapo juu.
Uandishi ni taaluma kama zingine tena imefikia mahali pa kuitwa mhimili wa nne. Nadhani si rahisi kukuta kila mtu anajiita Mwanasheria, Daktari au Engineer. Makundi haya yanalinda taaluma zao kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla. Sasa waandishi wa habari wanafanya nini kuzuia makanjanja!!!! Hivi huoni kuwa waandishi wenye kalamu ndio walitakiwa waongoze na wengine wafuate na sio kinyume chake!
Pili, kuna kitu tukubaliane na nawaomba radhi waandishi watakao kereka lakini siombi radhi kwa hoja. Ni wazi kuwa waandishi wetu wamedumaa katika kujifunza ima kutoka kwa wenzao au kwa wao wenyewe. Ukifuatilia uandishi wa habari wa nchi za wenzetu utagundua sisi bado kabisa. Mfano, habari zinaandikwa kama taarifa ya karani na hakuna analysis, details au observation. Ni habari tu fulani kasema fulani amekwenda wapi. Yaani ni reporters na sio journalist.
Tatu hakuna ufuatailiaji wa habari na wala kutoa usuli (feedback). Leo nikiwauliza waandishi wa habari wa Tanzania yule mtoto aliyeokotwa akilelewa na nyani amefikia wapi hakuna jibu.
Hakuna anayefuatailia kujua kile aliachoandika juzi kimefikia wapi.
Hata hizo habari sensational basi hawazifuatilii. Ukimuuliza mwandishi wa habari nchini, ile tume ya kikwete iliyohusu IGP, AG, PCCB chief imetoa taarifa au imefikia wapi hakuna mwenye jibu n.k
Mnadhani watu wanataka kusikia siasa tu bila kujua kuwa yapo mambo mengi madogo madogo lakini yanaigusa jamii sana.
Kuna mwandishi waliwahi kaundika kuhusu kufuliwa kondomu kunakoitwa 'kifanyio' kule shinyanga tena kwa biashara.
Kwangu mimi ilikuwa ni habari kubwa sana kuliko data za IMF ambazo mwananchi hawezi kuzitafsiri achilia mbali kuwa anaishi nazo kila uchao akipigika na njaa. Hili la kondomu ni muhimu kwake kwani halisubiri mwaka 2030 Tanzania itakapoipuku Kenya Kiuchumi
Niseme tu kuwa waandishi wa Tanzania sio creative na hili mnatakiwa mlifanyie kazi. Ninashangaa mzungu anakuja kutoka marekani na kuniandikia habari za maisha ya manzese au bustani ya mungu kule Iringa wakati kila siku watu wanapita na kuona maua.
Lakini pia lazima muwe na curiosity ya mambo. Waandishi wangapi wanajua kuhusu umuhimu wa mbuga ya Tarangire na chatu wanaopanda miti au simba wanaopanda miti?
Mngekuwa makini, mashirika kamaTANAPA wangewapa kazi za kuandika documentary n.k na siku kusubiri bahasha zisizo na uhakika.
Sehemu ya matatizo yenu ni kutotaka kujifunza, kutokuwa na passion na professional kunakopelekea kukosa curiosity.