Pasco,
Hapana. Bahasha si dunia nzima. Mimi nimefanya kazi ya uandishi kwa mashirika mawili makubwa ya Kimarekani. Ilikuwa ni marufuku kupokea bahasha ya aina yeyote ile kutoka kwa mtu, shirika, au kampuni yoyote ile unayoripoti juu yake. It is unethical. Huwezi kuchukua hela kutoka kwa mtu au kampuni unayoripoti juu yake. Hapa Marekani wale waandishi habari wanaofuatana na Obama ambao wana "cover" White House, wakisafiri kwenye Air Force one, kampuni yao hupelekewa bill na White House. Hata waandishi habari wa Uingereza nina hakika hawaruhusiwi kuchukua bahasha. Tulichokuwa tunaruhusiwa ni kuhudhuria luncheon, tuseme kama Thabo Mbeki amekaribishwa kutoa mhadhara kwenye taasisi moja ya Kimarekani, sisi waandishi wa habari tunaohudhuria tunashiriki pia kwenye luncheon hizo au dinner, depending kama ni mchana au jioni, na ofisi zetu zinakuwa na taarifa. Lakini hatuwezi kupokea gratuity yeyote kutoka kwa mbunge, senetor, gavana au CEO tunayekwenda kufanya mahojiano naye. It is illegal and unethical.
Kama hayo yanatokea katika third world usiseme ni duniani kote.