Peter Nyanje
Member
- Jan 15, 2012
- 43
- 18
Kwa kuwa na mimi ni mwandishi, naomba nitoe mchango wangu katika hili, pasco anaweza kuja kujibu pia kwa maana limeelekezwa kwake.Kwanini Rais Mstaafu Mkapa alikuwa hawakubali nyie waandishi wa Habari wa Tanzania,
Utusaidie na hilo Pasco
Jambo kubwa lililomfanya Mkapa awadharau waandishi wakati ule ni kushindwa kukutana na mwandishi ambaye alimuuliza maswali magumu ambayo yangemlazimisha atoe majibu na masuala nyeti. Kusema kweli, waandishi wengi, huwa hawajiandia vya kutosha wakati wanapokwenda kufanya mahojiano na mtu, matokeo yake, huuliza maswali mepesi, ambayo ni rahisi kuyafikiria. Mkapa aliwalinganisha waandishi hao na akina Tim Sebastiani ambao walikuwa wakifanya utafiti wa masuala nyeti kabla hawajakutana naye kiasi cha kumuuliza maswali ambayo yalimuudhi kweli kweli Mkapa.