Pasco,'
Grants na fellowship si rushwa. Hizi hazitolewi ili mwandishi aandike mazuri tu ya yule anayetoa hiyo pesa. Nilienda Rumbek, Southern Sudan mwaka 2000 kushuhudia "decomissioning of the child soldier." Ofisi yangu ilinilipia nauli na kwa sababu hakukuwepo hoteli huko, UN ikanilipia malazi na chakula kwenye kambi yao. Niliandika ripoti juu ya zoezi hilo ambalo lilikuwa organized na UNICEF. Nilipata interview na Mkurugenzi wa UNICEF na pia nikazungumza na Salva Kiir ambaye ndiye leo rais wa South Sudan. Coverage ya kazi za NGO's ni muhimu for the public na vile vile NGOs zinapenda kupeleka makao makuu ripoti ya coverage ya kazi zao. Hapo ni win win kwa pande zote. Lakini sitakubali BP wanilipie ili niandike story kwamba wamefanya kazi nzuri ya kusafisha ufukwe wa New Orleans baada ya ile oil spill. Ni afadhali niende mwenyewe independently na kama wamefanya kazi nzuri nifikie uamuzi huo bila kushawishiwa na bahasha.
Mkuu Jasusi, tangu nimepandisha hii thread jana, leo sasa ndio kwa mara ya kwanza naanza kufarijika!, hapo kwenye bold its now sasa we go together!, hiyo ndio genuine admission ya kwanza kuwa sio kila bahasha ni rushwa!. Umekubali kuwa grants na fellowships sio rushwa!. Jee grants na fellowships sio rushwa kwa sababu gani ili hali nazo ni bahasha walizokunjiwa waandishi?!. Naamini Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsorships za Awards mbali mbalimbali kwa Waandishi sio rushwa kwa sababu, japo ni bahasha waandishi wanazopewa ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao vizuri, enabling them, emporing them bila kuinfluence wanachoripoti, sasa baada ya kukubaliana kuwa kuna bahasha ambazo waandishi wanashikishwa ni rushwa lakini sii kila bahasha ni rushwa!.
Mkuu Jasusi, bahasha ya kwanza uliokunjiwa ni bahasha ya "usafiri" ambayo ofisi yako unicef ilikukunjia!.Bahasha ni bahasha, haijalishi imetolewa na nani, iwe ni ofisi yako, au wewe uingia kwenye activity code ya Unicef, utazame list ya funders wa hiyo activity code, utazame aliyetoa fedha kwa that specif activity ni nani, na nini malengo yake kwa Unicef ila the bottom line wewe uliwezeshwa ukafika huko S.Sudan!. Ingekuwa Unicef wamekutuma ukafanye positive coverage ili wale donors wa unicef wafurahi waongeze donation, then ingekuwa rushwa!. Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!. Suppose Jasusi ungekuwa unafanyia kazi Daily news, unaujua umasikini wa Daily News!, halafu Save the Childern Fund ya UK wakatangaza grant ya kuwenda kuandika makala kuhusu Child Soldirs wa huko S.Sudan, ukaaply ukapata, ukawezeshwa, jee sasa ndio ingegeuka rushwa kwa sababu aliyetoa bahasha sio Daily News?!.
Bahasha ya pili uliyopokea ni bahasha ya UN, hii ni bahasha ya chakula na malazi, kula bure, kulala bure nayo ni bahasha, jee hii nayo rushwa?. Tunarudi kule kwenye malengo, kama lengo la chakula hicho na malazi ni ili uiripoti kazi nzuri ya UN huko S.Sudan, then ingekuwa rushwa!. Lakini kwa vile S.Sudan sio tuu hakuna hoteli, bali hakuna sehemu safe kama zile container za UN!, hii maana UN wamekupa bahasha ya kufacilitate your safe stay!.
Mkuu Jasusi, lazima nikupongeze kwa sababu you have the guts to say no to BP!, labda sababu ni kumuenzi Ken Saro Wiwa, au package yako ya Unicef ukijumlisha na Hardship Alowance, plus Risk Alowance kufanya kazi eneo hatarishi!, thanks ulikuwa UNICEF, ungekuwa Daily News au Uhuru, the story might not have been the same!. Think about it!.