Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Mpaka sasa hakuna ulichonikinaisha hata kimoja, na ikiwa itatokea nikaliona, basi mimi ndio wa kwanza kukiri hiyo ni halali yako. Lakini hili la kupewa vibahasha na "source" hata uniambie vipi, haliniingii kabisa.
Tumefikia mahali pa zuri, maadam kila bahasha kwa waandishi kwako ni rushwa, then nakubaliana na wewe, na kwa vile imeanzia toka jikoni, unaonaje haya majina unayoniita mimi ungemwita na yeye?.
 
Mkuu Wacha1, hivi ulidhani wale waandishi wanaosafiri na Obama wanasafiri bure, wanakula bure na kulala bure?. Si wanapewa bahasha nene huko makazini kwao! Wanaotoa hizo pesa za hizo bahasha nene ni kina nani?.

Au unatazama na kusikiliza BBC ukijua ni bure tuu kama sadaka?!. Kila aliye Uingereza anakatwa pesa za kusikiliza na kuangalia BBC, usikilize, usisikilize, utazame, usitazame, unakatwa!.
Pasco,
Usichanganye na kumkonfyusi Wacha1.
Waandishi habari wanaosafiri na Obama katika Air Force 1 hawalipiwi na White House. Wanalipiwa na ofisi zao. Wanapewa fedha za kujikimu na matumizi ya safarini kutoka ofisini mwao. The White House bills their companies/corporations/news agencies when the trip is over. Tofauti na sisi akija hapa Michuzi ameandamana na Kikwete ni wazi kuwa kalipiwa na Ikulu na wala si Daily News. Hiyo ni tofauti kubwa sana na huwezi kuiita hiyo bahasha.
 
5. Jee ni bahasha zipi ni rushwa?.

Baada ya kuzitaja bahasha ni bahasha genuine, sasa nitaziorodhesha bahasha ambazo ni rushwa.
Bahasha ya Kushinikiza Positive Covarage.
Hii ndio bahasha ya kwanza ya rushwa, hutolewa na source ili kuwa entice waandishi wawafanyie favourable covarage. Kwa kawaida bahasha hii inakuwa nene fulani, bahasha hii huandamana na obligation kuwa lazima story itoke. Bahasha hizi za shinikizo la story kutoka hazitolewi kwa waandishi wote, bali to only few selected, na kwa vile bahasha hizi ni rushwa, hutolewa kwa kificho!. Zile bahasha za halali kama za usafiri husainiwa wazi wazi na hukawiwa kila mtu akiona kwa sababu there is nothing to hide, lakini hizi hutolewa kwa kificho, no one will know nani amepokea bahasha na nani hajapokea kutokana mazingira ya usiri. Watoaji wa bahasha hizi wanajua ni rushwa na wapokeaji wanajua ni rushwa!. (to avoid conflict of interest, nawaombeni msiniulize zaidi kuhusu hizi!).
 
Ndugu yangu Pasco nenda tena kasome maana ya rushwa!! Bahasha zote hizi unazoongelea ni rushwa.
 
Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsor ships za Awords mbali mbalin kwa Waandishi, nazo Rushwa?.
Kuna mashirika na taasisi mbalimbali zinatoa fungu fulani kwa waandishi kuandika kuhusu jambo fulani, usually indepth, mfano Tanzania Media Fund, inatoa funding kwa journalist kuandika stories toka vijijini, au investigative stories. Hizi ni bahasha nene zenye kucover usafiri, chakula, malazi, kwa field trip hata za mwezi mzima, nyingine ni attachment mahali kwa muda hadi miezi 6, hizi nazo ni bahasha, jee nazo ni rushwa?. No hizi ni bahasha safi!.

Mashirika/ makampuni au taasisi huweza kugharimia kukundi cha habari kuandika about specific news, hii inaitwa sponsorship mfano TAMWA ON FGM, TGNP dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia, JET thidi ya uharibifu wa mazingira etc. Bahasha nene hotolewa ili waandishi waandike kusu specific topic, hizi nazo rushwa?. Mifano iko mingi, mia kidogo ambapo bahasha hutolewa kwa waandishi genuinely na sio rushwa!. Wale mnaolazimisha kila bahasha kwa mwandishi ni rushwa, nawaombbeni sana mthink twice, tubishane kwa hoja na sio kulazimisha hoja!
 
Pasco,
Usichanganye na kumkonfyusi Wacha1.
Waandishi habari wanaosafiri na Obama katika Air Force 1 hawalipiwi na White House. Wanalipiwa na ofisi zao. Wanapewa fedha za kujikimu na matumizi ya safarini kutoka ofisini mwao. The White House bills their companies/corporations/news agencies when the trip is over. Tofauti na sisi akija hapa Michuzi ameandamana na Kikwete ni wazi kuwa kalipiwa na Ikulu na wala si Daily News. Hiyo ni tofauti kubwa sana na huwezi kuiita hiyo bahasha.
Mkuu Jasusi, what is the diference?, does it matter hiyo bahasha imetoka wapi au it maters mwandishi kawezeshwa kutimiza wajibu wake?. Ninachosema ni kuwa ili waandishi watimize wajibu wao, lazima wawezeshwe, kitendo chochote cha uwezeshaji waandishi, ni bahasha!, ili bahasha hiyo iwe rushwa, inategemea uwezeshwaji huo una lengo gani, kama uwezeshaji huo ni wenye lengo jema, then ndio huu ninauita basha nzuri!, kama uwezeshaji una lengo la kuimfluence news contents, then hiyo ndio rushwa!.

Jasusi, Michuzi akiwa Daily News kawezeshwa na Ikulu/MFA kuja Marekani, kapokea bahasha ili aweze kufanya kazi. Mwandishi wa CCN kawazeshwa na ofisi kuandamana na Obama, kafungashiwa fungu lake, libahasha hilo nene!, sasa utaita rushwa?!. Au hii ya Michuzi ndio rushwa ila ya CNN sio rushwa?.

Tanzania tunaishi kwenye object poverty, na media zetu ziko kwenye destitute hazina uwezo wa kumgharimia mwandishi wake aandamane na rais huko Marekani, Ikulu kwa kuujua umuhimu wa ziara hiyo, inagharimia waandishi kwenda Marekani na kuwagharimia, jee hiyo nayo ni rushwa?.
 
Pasco, mwenye wajibu wa kukuwezesha ufanye kazi yako ni mwajiri wako na sio client!! Unapopokea bahasha kutoka kwa mtu anayekupa habari tayari au unayetakiwa kuandika habari zake hiyo ni rushwa hata kama hajashinikiza uandike habari yake. Maana tayari hapo umepata "favour" na reporting yako kwako itakuwa tofauti na ya yule aliyekupa habari bila kukuwezesha!!

Safari za waandishi na Rais kama ni kweli zote zinagharamiwa na Ikulu nazo ni rushwa! Maana waandishi hawatakuwa na "uhuru" wa kuhoji/kuuliza mambo mbali mbali kuhusu ziara hizo. Wao kazi yao itakuwa ni kupiga picha na kuriport kile ambacho kitafurahisha Ikulu, hawatakuwa tofauti na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu!!
 
Bahasha za Kuzuia Habari Kutoka-Hii ni Rushwa!.
Kuna bahasha za kuzuia story fulani isitoke!, hizi ni bahasha zinazotembezwa kwa waandishi ili kuzuia story fulani isitoke ili kulinda maslahi fulani au jina la mtu fulani lisichafuke!. Hii inahusisha kuitwa kwenye tukia na kutake a good care ya waandishi ili wasiripoti kabisa kuhusu tukio fulani!. Hii mara nyingi huusisha ama scandals au black mail. Mfano kigogo mmoja mheshimiwa sana, ameshitakiwa kwa kosa la kufumwa akifanya mapenzi na Changudoa ufukweni. Story hiyo ikitoka itamvunjia heshima sana mzee, hivyo anakata fungu fulani la kutakata la kuwatake care waandishi wote wanaoripoti toka mahakamani ili kesi ya kigogo ikitajwa waipotezee. Au Wafanyakazi wa kiwanda fulani wamegoma, wewe ni mwandishi unakwenda kucoiver story, unaanza na mgomo, ili kubance story, lazima uwatafute na management, ile kufika management, unakuwa well taken care off, uamuzi ni wako, ulinde heshima ya taaluma yako na ulale njaa, ama uuze utu wako jioni ukakae viti virefu, uamuzi huwa ni individual!.
 
Pasco, mwenye wajibu wa kukuwezesha ufanye kazi yako ni mwajiri wako na sio client!! Unapopokea bahasha kutoka kwa mtu anayekupa habari tayari au unayetakiwa kuandika habari zake hiyo ni rushwa hata kama hajashinikiza uandike habari yake. Maana tayari hapo umepata "favour" na reporting yako kwako itakuwa tofauti na ya yule aliyekupa habari bila kukuwezesha!!

Safari za waandishi na Rais kama ni kweli zote zinagharamiwa na Ikulu nazo ni rushwa! Maana waandishi hawatakuwa na "uhuru" wa kuhoji/kuuliza mambo mbali mbali kuhusu ziara hizo. Wao kazi yao itakuwa ni kupiga picha na kuriport kile ambacho kitafurahisha Ikulu, hawatakuwa tofauti na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu!!
Mkuu Limbani, kusema ukweli, hii ni kweli ni kinyume cha maadili ya uandishi kwa sababu kitaingilia objectivity ya story na hivyo kushindwa kumaintain impatiality kwa kuripoti only the bright sides of the events. Nakumbuka mimi nimefundishwa Media Ethics na mwalimu Mkanada Patrick Walsh, akatuambia kule Canada, ni marufuku kwa waandishi hata kukubali offer ya cup of coffe, you have to pay!, hakuna cha mwaliko wa lumcheon wa dinner kwa source!.

Due to umasikini wetu, kama media zetu zinashindwa kwenda tuu hapo Kimanzichana na Chole Samvula kupata story toka kijijini, itakuwa ni safari za nje ya nchi?. Ni kufuatia umasikini huu, sisi Watanzania tunatakiwa kutengeneza our own ethics to suit our situation, kwenye hizo ethis zetu, ndipo tukubali funding the media in good faith, sio rushwa ila to regulate tuu hii funding badala ya kupeana hivi vibahasha huko mikutanoni, huyo source ailete hii pesa ofisini na media ndio iwagawie waandishi wake!.
Kwangu mimi ili kuiita ni rushwa au la, it depends on the motive behind!.
 
Blackmail na Framing ni rushwa mbaya kabisa!

Hii inahusisha waandishi kupata habari mbaya kuhusu vigogo fulani, mwandishi ku solicit money ili kuzuia kumlipua muhusika huyo!. Au umezinyaka picha za utupu za kigogo fulani unamuonyesha na kudai kiasi cha fedha ili uzizichapishe!. Kesi ya rafiki yangu Jerry Muro ili fall kwenye kundi hili!.

Sambamba na blackmail, kama polisi wanaweza kukuisingizia kesi ndivyo waandishi wa habari wanavyeweza kuku frame na kukuandikia habari mbaya za kutunga, mfano wa alichofanyiwa Dr. Salim Ahmedv Salim na gazeti la Mtanzania ili kumbeba JK awe mgombea!,
 
Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsor ships za Awords mbali mbalin kwa Waandishi, nazo Rushwa?.
Kuna mashirika na taasisi mbalimbali zinatoa fungu fulani kwa waandishi kuandika kuhusu jambo fulani, usually indepth, mfano Tanzania Media Fund, inatoa funding kwa journalist kuandika stories toka vijijini, au investigative stories. Hizi ni bahasha nene zenye kucover usafiri, chakula, malazi, kwa field trip hata za mwezi mzima, nyingine ni attachment mahali kwa muda hadi miezi 6, hizi nazo ni bahasha, jee nazo ni rushwa?. No hizi ni bahasha safi!.

Mashirika/ makampuni au taasisi huweza kugharimia kukundi cha habari kuandika about specific news, hii inaitwa sponsorship mfano TAMWA ON FGM, TGNP dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia, JET thidi ya uharibifu wa mazingira etc. Bahasha nene hotolewa ili waandishi waandike kusu specific topic, hizi nazo rushwa?. Mifano iko mingi, mia kidogo ambapo bahasha hutolewa kwa waandishi genuinely na sio rushwa!. Wale mnaolazimisha kila bahasha kwa mwandishi ni rushwa, nawaombbeni sana mthink twice, tubishane kwa hoja na sio kulazimisha hoja!
Pasco,'
Grants na fellowship si rushwa. Hizi hazitolewi ili mwandishi aandike mazuri tu ya yule anayetoa hiyo pesa. Nilienda Rumbek, Southern Sudan mwaka 2000 kushuhudia "decomissioning of the child soldier." Ofisi yangu ilinilipia nauli na kwa sababu hakukuwepo hoteli huko, UN ikanilipia malazi na chakula kwenye kambi yao. Niliandika ripoti juu ya zoezi hilo ambalo lilikuwa organized na UNICEF. Nilipata interview na Mkurugenzi wa UNICEF na pia nikazungumza na Salva Kiir ambaye ndiye leo rais wa South Sudan. Coverage ya kazi za NGO's ni muhimu for the public na vile vile NGOs zinapenda kupeleka makao makuu ripoti ya coverage ya kazi zao. Hapo ni win win kwa pande zote. Lakini sitakubali BP wanilipie ili niandike story kwamba wamefanya kazi nzuri ya kusafisha ufukwe wa New Orleans baada ya ile oil spill. Ni afadhali niende mwenyewe independently na kama wamefanya kazi nzuri nifikie uamuzi huo bila kushawishiwa na bahasha.
 
Pasco,
  1. Hustahili kusema hivyo tena wewe ni mwanasheria
  2. Bashasha yoyote ni haramu
  3. Unachozungumza ni mazoea, mazoea hayafanyi haramu kuwa halali. Ukata sio excuse ya kufanya maovu
  4. Wewe mwenyewe umekosa ''moral authority'' debe unalompigia mtu mmoja humu sio bure lazima kuna nguvu ya pesa
  5. Tatizo hatuna watu waliobobea kwenye habari. Watu kama Ulimwengu, Kajubi, Nizar, Ryoba, Kuhenga, kwa viwango vya uandishi wa BBC (English), CNN au Al Jazeera walitakiwa kuwa kwenye fani bado kama reporters au waandishi. Lakini huku wameshatundika madaluga eti wao ni ma columnists na maveteran matokeo yake kina Nzowa, Bashir Mwenda, Orest & CO ndo wako news room wao wanawaza bahasha tu
  6. Pasco waulizeni akina Uli Mwambulukutu, Nizar Visram, Mbaraka Islam au Rajab Ahmed wakueleze uharamu wa bahasha
 
...Sasa kama uwezeshaji huu unaiuta rushwa!, hebu muulize Rais Kikwete huwa anawapa nini wale waandishi wa habari anao safiri nao?!. Kama kweli kila anaetoa bahasha kwa waandishi lazima aende jela, naomba tuanzie na Ikulu, nami jela nitajipeleka mwenyewe bila hata kusubiri kutafutwa!....

Pasco, Ikulu ya sasa naamini sio reference nzuri kwa suala la uadilifu hasa rushwa/ufisadi. Nina imani wewe umekuwepo kipindi cha Mwalimu na baadae Mzee Ruksa na Mjomba Ben...vipi trend ya mambo haya ya bahasha unaionaje? Najua kumetokea mabadiliko makubwa tu ya aina, idadi na namna ya ufanyaji kazi wa vyombo vya habari lakini si vibaya tukajiuliza tu! Hata baada ya kung'atuka Mwalimu ameongea na waandishi wa habari mara kadhaa (nazungumzia miaka ya tisini tu)....je bahasha zilikuwa zinatoka? Kwa nani?

Waliokuwa wanasupport takrima (katika uchaguzi) walikuwa wanajenga hoja kama za kwako. Lakini baadae sote tunajua jambo hili liliharamishwa (pamoja na kuwa bado kwa namna moja ama nyingine bado linafanyika). Maadili/Ethics ni suala tete sana hasa katika nchi zetu hizi.
 
Pasco,'
Grants na fellowship si rushwa. Hizi hazitolewi ili mwandishi aandike mazuri tu ya yule anayetoa hiyo pesa. Nilienda Rumbek, Southern Sudan mwaka 2000 kushuhudia "decomissioning of the child soldier." Ofisi yangu ilinilipia nauli na kwa sababu hakukuwepo hoteli huko, UN ikanilipia malazi na chakula kwenye kambi yao. Niliandika ripoti juu ya zoezi hilo ambalo lilikuwa organized na UNICEF. Nilipata interview na Mkurugenzi wa UNICEF na pia nikazungumza na Salva Kiir ambaye ndiye leo rais wa South Sudan. Coverage ya kazi za NGO's ni muhimu for the public na vile vile NGOs zinapenda kupeleka makao makuu ripoti ya coverage ya kazi zao. Hapo ni win win kwa pande zote. Lakini sitakubali BP wanilipie ili niandike story kwamba wamefanya kazi nzuri ya kusafisha ufukwe wa New Orleans baada ya ile oil spill. Ni afadhali niende mwenyewe independently na kama wamefanya kazi nzuri nifikie uamuzi huo bila kushawishiwa na bahasha.
Mkuu Jasusi, tangu nimepandisha hii thread jana, leo sasa ndio kwa mara ya kwanza naanza kufarijika!, hapo kwenye bold its now sasa we go together!, hiyo ndio genuine admission ya kwanza kuwa sio kila bahasha ni rushwa!. Umekubali kuwa grants na fellowships sio rushwa!. Jee grants na fellowships sio rushwa kwa sababu gani ili hali nazo ni bahasha walizokunjiwa waandishi?!. Naamini Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsorships za Awards mbali mbalimbali kwa Waandishi sio rushwa kwa sababu, japo ni bahasha waandishi wanazopewa ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao vizuri, enabling them, emporing them bila kuinfluence wanachoripoti, sasa baada ya kukubaliana kuwa kuna bahasha ambazo waandishi wanashikishwa ni rushwa lakini sii kila bahasha ni rushwa!.

Mkuu Jasusi, bahasha ya kwanza uliokunjiwa ni bahasha ya "usafiri" ambayo ofisi yako unicef ilikukunjia!.Bahasha ni bahasha, haijalishi imetolewa na nani, iwe ni ofisi yako, au wewe uingia kwenye activity code ya Unicef, utazame list ya funders wa hiyo activity code, utazame aliyetoa fedha kwa that specif activity ni nani, na nini malengo yake kwa Unicef ila the bottom line wewe uliwezeshwa ukafika huko S.Sudan!. Ingekuwa Unicef wamekutuma ukafanye positive coverage ili wale donors wa unicef wafurahi waongeze donation, then ingekuwa rushwa!. Nataka tufike mahali tukubaliane kuwa ili bahasha iwe ni rushwa, lazima iwe na malengo ya kuimfluence, lakini bahasha genuine yenye malengo ya uwezeshaji, sio rushwa!. Suppose Jasusi ungekuwa unafanyia kazi Daily news, unaujua umasikini wa Daily News!, halafu Save the Childern Fund ya UK wakatangaza grant ya kuwenda kuandika makala kuhusu Child Soldirs wa huko S.Sudan, ukaaply ukapata, ukawezeshwa, jee sasa ndio ingegeuka rushwa kwa sababu aliyetoa bahasha sio Daily News?!.

Bahasha ya pili uliyopokea ni bahasha ya UN, hii ni bahasha ya chakula na malazi, kula bure, kulala bure nayo ni bahasha, jee hii nayo rushwa?. Tunarudi kule kwenye malengo, kama lengo la chakula hicho na malazi ni ili uiripoti kazi nzuri ya UN huko S.Sudan, then ingekuwa rushwa!. Lakini kwa vile S.Sudan sio tuu hakuna hoteli, bali hakuna sehemu safe kama zile container za UN!, hii maana UN wamekupa bahasha ya kufacilitate your safe stay!.

Mkuu Jasusi, lazima nikupongeze kwa sababu you have the guts to say no to BP!, labda sababu ni kumuenzi Ken Saro Wiwa, au package yako ya Unicef ukijumlisha na Hardship Alowance, plus Risk Alowance kufanya kazi eneo hatarishi!, thanks ulikuwa UNICEF, ungekuwa Daily News au Uhuru, the story might not have been the same!. Think about it!.
 
Ukanjanja na changamoto inayoukabili uandishi nchini
Na Prudence Karugendo

Zimekuwepo juhudi za makusudi zinazodaiwa ni za kutaka kuilinda taaluma ya uandishi zinazoonekana kufanywa na wana taaluma wakereketwa. Wanataaluma hao wanaona kwamba ni kama taaluma yao inaingiliwa. Majina mbalimbali ya kibaguzi yamebuniwa yakiwalenga wanaodaiwa kuivamia fani. Yanatajwa majina kama makanjanja, makanjakanja nakadhalika, bila shaka mengine yako mtamboni yanaundwa.

Binafsi nakubaliana na hoja ya kuwepo kwa taaluma ya uandishi na umuhimu wa kuiheshimu taaluma hiyo. Kinachonipa utata, na mahali ninapotofautiana na wanataaluma, ni katika namna taaluma hiyo inavyopaswa kulindwa. Sikubaliani na wanaotaka taaluma hiyo ilindwe kwa mabavu na vitisho dhidi ya wale wasiotakiwa ambao kwa namna moja au nyingine ndio wanaoonekana kuivamia taaluma, japo wao wanajiweka karibu kutokana na mapenzi yao kwenye taaluma hiyo na hivyo kuamua kuiunga mkono.

Ili taaluma iheshimike haina budi kujilinda yenyewe kwa wana taaluma kuonyesha kile kinachoifanya ikaitwa taaluma, ambacho kwa tafsiri nyingine kinapaswa kiwe nje ya upeo wa wale wasio na taaluma. Mathalan, maadishi yenye kufikirisha ambayo si kila mmoja mwenye kuelewa kuandika anaweza kuyarukia na kujaribu kuyaandika.

Kinyume chake wana taaluma ya uandishi wanashindwa kukifanya kile ambacho kingeifanya taaluma yao ikaheshimika na kuogopeka, badala yake wanafanya mambo ambayo kila mmoja anajiona ana uwezo nayo. Kwa hilo wa kujilaumu ni wana taaluma ya uandishi wenyewe. Wanapaswa wajiulize kwa nini taaluma nyingine hazivamiwi? Badala ya wana taaluma kutumia ujuzi wa kitaalamu kuihami taaluma yao wanaishia kupiga piga makelele ya kuvamiwa kwa kutaka kuishawishi dola itunge sheria ya kuwalindia taaluma yao. Wana taaluma wameshindwa kuilinda taaluma, wanataka ilindwe na sheria na bunduki (?).

Kushindwa huko kwa wana taaluma kutumia njia za kitaalamu kuilinda taaluma yao kunaifanya taaluma ya uandishi kubaki kama haina mwenyewe, na matokeo yake ni kila mtu mwenye kujiona ana uwezo wa kuandika kushawishika kujiingiza kwenye taaluma hiyo kwa vile wahusika wanakuwa hawawezi kujitofautisha na wasio wahusika.

Haitoshi kuilinda taaluma kwa kutaja tu muda ambao mtu anakuwa ameutumia kuisotea taaluma husika au mrundikano wa shahada. Kinachotakiwa ni kuonyesha mabadiliko katika taaluma kwa kuifanyia vitu ambavyo hasiye mwana taaluma atajionea aibu kuisogelea taaluma ya watu. Hapa nchini ni wana taaluma wangapi wanafanya hivyo?

Wapo watu ambao naamini kwamba wanaendelea kuilinda taaluma ya uandishi bila kutumia mabavu pamoja na kwamba watu hao hawapo tena duniani, ingawa kulingana na mpangilio wa madai yanayotolewa na watetezi wa taaluma wa kipindi hiki, watu hao wanaweza wakaonekana nao hawakuwa wana taaluma kwa vile wasingeweza kutaja miaka waliyotumia wakiisotea taaluma hiyo ya uandishi wala kuonyesha vyeti vya kuwatambulisha kama wana taaluma.

Mmoja wa watu ninaoamini kuwa bado wanailinda taaluma ya uandishi ni marehemu Shaaban Robert. Uandishi wa mzee yule, ambao mwingine aliufanya zaidi ya miaka 50 iliyopita, bado mpaka sasa unailinda taaluma ya uandishi kwa kumfanya kila mtu aliye makini asiweze kujipendekeza kuwa anaweza kuimudu taaluma hiyo. Wala Shaaban Robert hatumii majivuno, vitisho na majigambo katika kuilinda taaluma yake. Yeye anaiwezesha taaluma kujionyesha uadhimu na uzito wake na kisha yenyewe kujijengea heshima.

Uandishi wa Shaaban Robert wa kuonya, kuhadharisha, kukanya, kusifia pamoja na kuelimisha, bila kukosa kuhabarisha kwa namna ya pekee ni kielelezo tosha cha uadhimu wa taaluma ya uandishi na manufaa inayoyachangia katika jamii.

Aina ya uandishi wa Shaaban Robert inawafanya watu kuitamani taaluma ya uandishi. Hii ni kwa sababu wapo watu wanaotumia aina ya uandishi wake kama mwongozo wa maisha yao. Hivyo ndivyo taaluma inavyopaswa kuinufaisha jamii. Na papo hapo jamii inajenga heshima kwa taaluma hiyo kwa wanajamii kuamini kwamba si wote wenye uwezo wa kufanya kama alivyofanya yeye. Kwa mantiki hiyo sitegemei kama zingekuwepo kelele za kutaka taaluma ya uandishi iheshimiwe. Yenyewe ingekuwa inajitosheleza.

Mtu mwingine aliyeitumia taaluma ya uandishi kuinufaisha jamii ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere. Tangu kabla ya uhuru wa Tanganyika, alipoingia kwenye harakati za kutafuta uhuru, alitumia zaidi taaluma ya uandishi na kuifanya silaha yake kuu katika mapambano yale. Tunakumbuka alivyonusurika kwenda jera baada ya kudaiwa kuwakashfu wakoloni akiwa mhariri wa gazeti la chama cha TANU. Hata baada ya uhuru bado Nyerere aliendelea kuitumia taaluma hiyo kuwaelimisha wananchi juu ya maana ya nchi kuwa huru. Tunafahamu machapisho aliyoyatoa, sina haja ya kuyataja hapa. Na alipokuwa ameisha staafu uongozi bado Mwalimu aliendelea kujikita katika taaluma ya uandishi na kuitumia kufikisha nasaha zake kwa jamii. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 pale lilipoibuka kundi la wabunge la kuidai serikali ya Tanganyika, Mwalimu alitumia taaluma ya uandishi kuutuliza mzuka huo. Aliandika vitabu viwili kwa mkupuo navyo vikawafanya wabunge wale kufyata mkia. Ni taaluma ya uandishi iliyofanya kazi.

Ingekuwa sasa hivi si ajabu Mwalimu angetakiwa aonyeshe vyeti vya uandishi kwanza na wale wanaoamini kwamba taaluma hii ni mali yao, kabla ya maandishi yake hayajakubalika kwa wana taaluma. Na nisingeshangaa kama naye angekumbwa na jina la ukanjanja.

Nataka nieleweke, nilichokilenga hapa ni uandishi kama waleta hoja wanavyopendelea kuliweka. Maana najua kuna watakaonibadilikia wakidai kwamba kinachopaswa kulengwa ni uandishi wa aina fulani, mfano uandishi wa habari. La uandishi wa habari linaeleweka ila kwa makusudi kabisa wameamua kulipanua suala hilo ili liweze kuwameza wote wanaojihusisha na uandishi kwa lengo la kutaka kuwadhibiti. Ndiyo maana hata mimi hoja zangu nikawa nazielekeza kwenye uandishi kwa ujumla.

Kwa mtizamo wangu, wapo baadhi ya waandishi ambao wangependa kuihodhi taaluma ya uandishi, bila shaka kwa kutaka iwanufaishe wao tu bila jamii kuambulia chochote. Hawa ndio wanaowaona wale wanaojitokeza kuipanulia wigo taaluma hiyo kama wavamizi katika fani. Huko ndiko mashambulizi yanayoongozwa na majina yenye kila dalili za matusi, kama hilo la makanjanja, yanakoanzia, lakini bila wenyewe kuyaweka bayana manufaa yanayotokana na wale wasio makanjanja katika jamii yetu.

Majuzi mwandishi mmoja mkongwe hapa nchini alikuwa anajaribu kunipa darasa la uandishi baada ya mimi kuwa nimemchokoza. Alisema kwamba mwandishi anapaswa kuwa kama mwamuzi wa mchezo, kwamba hapaswi kuhukumu nani ashindwe ila kuuachia mchezo wenyewe ndio utoe hukumu. Akasema kwamba mwandishi anatakiwa kutoa kitu jinsi kilivyo bila dalili za upendeleo hata kama anao upande anaoupendelea. Nilipomuuliza juu ya waandishi wanaokiuka kanuni hiyo wakati wakijidai kuwa mahiri katika fani, akasema yeye sasa anatamani kufanya kazi katika vyombo vya ughaibuni maana kwa hapa nchini watu hawaambiliki. Kwa maana hiyo inaonyesha kwamba yanayofanywa na waandishi wa hapa nchini mengi hayaungi mkono, na si ajabu anawaona wale wanaowaita wenzao makanjanja ndio makanjanja wenyewe ila hasemi kwa kubanwa na kanuni za taaluma anazoonekana kuziheshimu na kuzizingatia, anaiachia jamii itoe hukumu.

Zimetafutwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasakama hao makanjanja, ila ukweli ni kwamba kudorora kwa taaluma ya uandishi hapa nchini kunachangiwa zaidi na baadhi ya wana taaluma kukubali kuzianika wazi bei zao, kitu kilichoifanya taaluma ipimwe thamani yake kulingana na inavyotaka kutumiwa. Watumiaji ndio wamebaki wameishikilia thamani nzima ya taaluma Kwa hapa kuwasakama makanjanja ni kuwaonea.

Mwandishi anayeandika kwa maelekezo ya kumchafua mtu fulani au kumpamba mtu fulani tayari anakuwa ameishabandika alama ya bei yake usoni mwake. Na kamwe siwezi kuamini kama anafanya hivyo kwa malengo ya kuboresha taaluma. Dhahiri huko ni kuiua taaluma. Thamani ya taaluma inabaki mikononi mwa wale wanaotaka kuitumia taaluma kwa manufaa yao. Hivi kweli waandishi wa aina hii wanataka tuamini kwamba wanapowashambulia wanaowaita makanjanja wanakuwa wamedhamiria kwa dhati kuisafisha taaluma yao? Ni kitu gani cha kutufanya tusiwaone wao kuwa ndio makanjanja?

Tumewashuhudia wahariri kadhaa, ambao baadhi yao ndio vinara wa kuushambulia unaoitwa ukanjanja, ama wakitishiwa kuburuzwa mahakamani au wakati mwingine kulazimika kuomba misamaha nje ya mahakama kutokana na vyombo wanavyovihariri kutowatendea haki baadhi ya watu, kama vile kuwakashfu, kuwapaka matope nakadhalika, ili kuzifurahisha nafsi fulani ambazo zinakuwa zimewatuma au kuwanunua. Katika hali hiyo nani anayo haki ya kusimama na kumnyooshea mwingine kidole kuwa ni kanjanja? Kwa nini ukanjanja usionekane kuanzia hapo?

Hii inapaswa itukumbushe kwamba vita inapokuwa ngumu wasio na fani ya kijeshi hulazimika kuingia katika mapambano hata kama ni kwa kutumia silaha duni kama manati, ili kujaribu kuokoa jahazi. Wanaoitwa makanjanja inabidi tuwatambue kwa kukiona kile kinachofanywa na wasiokuwa makanjanja na kiwe kimejitofautisha, vinginevyo siuoni ubora unaowasababishia watu viburi vya kuwapachika wenzao majina ya ajabu ajabu.

Inabidi tujenge utamaduni wa kuifanya taaluma ya uandishi kujisimamia, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeijengea heshima inayoistahiki.

prudencekarugendo@yahoo.com

0784 989 512
 
Dhana ya ukanjanja na uhuru wa wanahabari
Na maggid mjengwa

RAIS Jakaya Kikwete alikuwa ziarani Ulaya miezi ya karibuni. Nikiwa Iringa niliweza kufuatilia habari za ziara ya Rais kupitia mtandao. Mathalan, Rais wetu alipokuwa nchini Denmark, niliweza kuingia kwenye tovuti ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Hapo nikasoma taarifa zote muhmu juu ya mgeni wake aliyekuwa akimsubiri siku hiyo, Rais Jakaya Kikwete.

Ikawekwa wazi kwenye tovuti ile, kuwa wanahabari na hususan wapiga picha wanakaribishwa saa fulani kwenda kupiga picha ya Waziri Mkuu na mgeni wake kabla ya wao wawili kuingia kwenye chumba cha mazungumzo ya faragha.

Ukaandikwa muda pia, pale wanahabari walipokaribishwa kwenye mkutano wa viongozi hao wawili na wanahabari. Muhimu kwa wenzetu hawa ni kwa mwanahabari husika kufika sehemu ya tukio katika muda uliopangwa akiwa na vitambulisho vyake. Kanuni yao ni wa aliyewahi anaingia kama nafasi ipo, na wa mwisho kufika anabaki nje kama nafasi zimejaa au kama atasababisha usumbufu wakati shughuli inaendelea.
Nilichokielezea hapo juu ni tofauti kubwa na nchi zetu hizi. Katika nchi zetu hizi Kiongozi Mkuu hata Waziri tu, atapenda awaite wahariri wa habari kuongea nao, na wahariri nao wanaona faraja kubwa kufanyiwa hivyo bila kudadisi ni kwanini waandishi wengine wasiruhusiwe kwenda kukutana na mkubwa ilihali ni hao wenye kuwafikia wananchi na kisha kupeleka habari zao na kuhaririwa na wahariri.

Mhariri anaweza kuwa ni mtu anayekaa kwenye chumba chenye kiyoyozi wakati wote wakati mwandishi mtafuta habari anaoga vumbi la mjini na vijijini afanyapo kazi yake. Huyu anaweza kuwa na maswali mazuri na pengine muhimu sana yenye kujengeka kwenye uhalisia. Maswali yatakayomsaidia hata kiongozi husika kuweza kuelewa hali halisi.

Naam. Dunia imebadilika pia. Hizi si zama tena za serikali za nchi kutunga sheria za kuwanyima au kuwapunguzia raia wao haki ya kupokea na kutoa taarifa mbalimbali. Kadri tunavyokwenda njia za kupata na hata kutoa habari zinaoongezeka.

Leo katika nchi yetu tunajadili muswaada wa uhuru wa habari. Sambamba na hilo tunajadili kushuka kwa viwango vya kitaaluma ikiwemo maadili ya taaluma husika. Tunazungumzia dhana ya ukanjanja, kwa maana ya waandishi wa habari wa mitaani wasio na elimu ya taaluma hiyo na pengine wenye elimu ya chini hata ya kiwango cha darasa la saba. Ni kundi hili lililozalisha dhana ya ukanjanja kwenye habari. Ni dhana inayopaswa kuangaliwa kwa mapana zaidi.

inaposoma habari zinazoandikwa na hao wanaoitwa makanjanja, hata kama baadhi hazikidhi viwango, mimi simwoni kanjanja kama tatizo, yeye ametuma kazi yake, na gazeti lina mhariri wa kupitia kazi hiyo, hivyo basi, tatizo ni chombo cha habari kutokuwa na wahariri makini, vinginevyo na mhariri naye ni kanjanja.

Katika kutafuta jawabu la tatizo hili hapa nitajaribu kujenga hoja ya msingi, nikiamini huenda itakuwa ni sehemu ya kupata majibu ya ufumbuzi wa tatizo lililopo. Niliwahi kujienga hoja hii huko nyuma, lakini nitafanya hivyo tena ili kuwakumbusha wadau wa habari kiwemo mwananchi wa kawaida umuhimu wa jambo hili.

Mbali ya kuwepo na umuhimu wa kuwa na Baraza la Habari, vyama vya waandishi wa habari, vilabu vya waandishi wa habari na kadhalika, ambayo kimsingi tunavyo sasa, nashauri wadau wa sekta ya habari wajenge hoja zitakazoifanya serikali ifikirie uwezekanao wa kufanya lifuatalo:

Kuangalia uwezekano wa kuanzisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari. Ruzuku kwa vyombo vya habari itasaidia katika uendeshaji wa vyombo hivyo, usambazaji wa habari na taarifa ikiwemo mafunzo ya waandishi. Katika hali ya sasa, tumeanza kuona dalili za ukiritimba wa kibisashara katika sekta ya habari.

Hofu yangu ni kwa baadhi ya vyombo vya habari na hata wanahabari ambao wana umuhumu mkubwa katika katika kuchangia ustawi wa nchi vikashindwa kuhimili ushindani huu, na wanahabari hao wakashindwa pia kufanya kazi katika mazingira hayo. Ni dhahiri kuwa baadhi ya vyombo hivyo vya habari vitakufa na wanahabari hao pia watakufa kiuandishi. Tuchague kati ya kuipigania ruzuku kwa vyombo vya habari au kufa. Hilo la mwisho likitokea si jambo la siha kwa taifa lililodhamiria kujenga misingi imara ya demokrasia.

Mathalan, katika nchi ya Sweden serikali inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuchangia kuimarisha misingi ya kidemokrasia ya nchi hiyo. Serikali ya Sweden imepanga bajeti ya dola za kimarekanai milioni 500 kila mwaka kama ruzuku kwa vyombo vya habari ili isaidie katika kuviendesha, usambazaji na kuhimili ushindani. Kuna mifano mingi ya nchi zenye kutoa ruzuku za namna hii kwa vyombo vyao vya habari.

Kwa upande wetu Tanzania, Serikali ingeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa utaratibu wa kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari na namna ya kuratibu mgawanyo huo wa ruzuku. Hakika, wanahabari ni mhimili wa nne katika utawala; mingine ni Serkali, Bunge, na Mahakama. Tuweke mkazo juu ya majukumu na wajibu wa vyombo vya habari katika kujenga na kuimarisha demokrasia. Taifa lolote la kisasa haliwezi kupiga hatua za maana za maendeleo bila ya vyombo huru vya habari. Vyombo huru vya habari ni vile vyenye kufanya kazi kwa umakini na bila kuingiliwa katika kazi zao ikiwemo kununuliwa ili kufanikisha maslahi binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu, hivyo basi, kuhatarisha maslahi ya umma.

Ni kwa kupitia vyombo vya habari wananchi hupata taarifa muhimu wanazohitaji kabla hawajafikia maamuzi kama raia, iwe katika masuala ya uchaguzi na hata mahala pa kazi na kwenye shughuli za baada ya kazi kama vile michezo.

Mwanahabari makini huumpa raia nyenzo zenye kumwezesha kuelewa mazingira anamoishi na hata kuielewa dunia anayoishi. Nyenzo hizo huwapa pia raia uwezekano wa kuchukua maamuzi ya ni upande upi waaegemee katika masuala mbali mbali ya kijamii. Unadishi ulio bora huvichua madhambi, makosa na kuonyesha mifano iliyo bora na ya kuigwa na wanajamii. Jamii ni vema iweze kuwaamini wanahabari, kwamba wanahabri hawa hawawezi kununuliwa kama bidhaa, kutiwa mifukoni na kusahau maslahi ya taifa.

Vyombo vya habari viwe na uwezo wa kutoa habari au taarifa zilizo sahihi na zenye kuangalia pande zote. Vyombo vya habari vijengewe uwezo wa kuchapisha au kutangaza kile kinachostahili kuchapwa au kutangazwa ili kuepuka kuvitumia vyumba vya habari kama sehemu ya kupelekea ujumbe wa matangazo ya biashara au propaganda.

Hivyo basi, kuna haja ya kuvipa ruzuku vyombo hivi vya habari ili viendelee kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi na kwa kuzingatia maadili Bila shaka, wapiga filimbi tunawahitaji, Lakini, Je, inakuwaje pale timu moja ya mpira inapoingia uwanjani na kushuka na mpiga filimbi na washika vibendera wawili kwenye basi walimosafiria?

Haiyumkini mwandishi wa Kitanzania, akashiriki msafara wa mheshimiwa kwa gharama za mheshimiwa kisha akaandika habari zisizomjenga mheshimiwa! Kwa baadhi ya waandishi, kama ilivyo kwa watendaji wengine, safari ni uhai, huingiza senti mifukoni.

Hivyo basi, najenga hoja ya kuwepo kwa utaratibu wa ruzuku ili kumpa uhuru zaidi mwanahabari, ili kuhakikisha kunawepo na uwingi wa fikra huru na uhai kwa vyombo vya habari na wanahabari. Kwa maslahi ya taifa.
 
Mkuu Pasco, kwanza hongera kwa maelezo yako mazuri. Mimi naomba unisaidie kitu kimoja. Wapo waandi wa habari za uchunguzi ambao nao hulazimika kutoa bahasha kutoka mifukoni mwao ili wapate habari. Hiyo nayo ni rushwa? Ama sawa kufanya hivyo.
 
Bahasha za Usafiri, Lunch na free bies nazo ni rushwa, jee wakati gani ni Rushwa?.

Kwa mliofuatilia pale mwanzo nilisema, bahasha ya usafiri ikitolewa kwa lengo la kuwawezesha waandishi kufika eneo la tukio bila kuingilia wataripoti nini, hiyo sio rushwa, ila bahasha hiyo hiyo inapotolewa kwa kuitwa hivyo hivyo usafiri kwa lengo la positive covarage, then bahasha hiyo ni rushwa!. Baada ya taarifa uchavuzi wa mazingira ya mto Tigiti, Barrick waliandaa ripoti yao positive na kuwagharimia waandishi na walioandika Barick ilichotaka!. Hiyo provision ya usafiri kwa waandishi uliofanywa na Barric kweli ni ku facilitate ili kupata positive coverage, hivyo unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa na rushwa, na unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa sio rushwa!. The deviding line is very thin ndio maana sishangazwi na wale wanaoona kila bahasha ni rushwa!.

Vivyohivyo offer za lunch, dinner na vijizawadi zawadi, kuna wakati ni rushwa na kuna wakati sio rushwa!. Ukienda semina warsha au kikao, wajumbe wote wakapowa sitting allowances zao, wote mkala lunch, au zile event, waalikwa wote wanapewa vijizawadi na waandishi wakiwemo, then sio rushwa, lakini waandishi mkiitwa mahali, hakuna event yoyote, mkapigwa lunch ya nguvu na baada ya hapo mkapewa bahasha ya transport haka kama hujapewa news yoyote, hiyo ni rushwa!.
 
Swali dogo kwako, rushwa ni fedha yoyote kwenye bahasha haijalishi ni kwa malengo yepi au rushwa ni fedha inayotolewa kwa malengo?.

Bahasha yoyote unayopewa na "source" haijalishi unaibatiza jina, malengo wala shabaha ipi ni rushwa tu.
 
Bahasha za Usafiri, Lunch na free bies nazo ni rushwa, jee wakati gani ni Rushwa?.

Kwa mliofuatilia pale mwanzo nilisema, bahasha ya usafiri ikitolewa kwa lengo la kuwawezesha waandishi kufika eneo la tukio bila kuingilia wataripoti nini, hiyo sio rushwa, ila bahasha hiyo hiyo inapotolewa kwa kuitwa hivyo hivyo usafiri kwa lengo la positive covarage, then bahasha hiyo ni rushwa!. Baada ya taarifa uchavuzi wa mazingira ya mto Tigiti, Barrick waliandaa ripoti yao positive na kuwagharimia waandishi na walioandika Barick ilichotaka!. Hiyo provision ya usafiri kwa waandishi uliofanywa na Barric kweli ni ku facilitate ili kupata positive coverage, hivyo unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa na rushwa, na unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa sio rushwa!. The deviding line is very thin ndio maana sishangazwi na wale wanaoona kila bahasha ni rushwa!.

Vivyohivyo offer za lunch, dinner na vijizawadi zawadi, kuna wakati ni rushwa na kuna wakati sio rushwa!. Ukienda semina warsha au kikao, wajumbe wote wakapowa sitting allowances zao, wote mkala lunch, au zile event, waalikwa wote wanapewa vijizawadi na waandishi wakiwemo, then sio rushwa, lakini waandishi mkiitwa mahali, hakuna event yoyote, mkapigwa lunch ya nguvu na baada ya hapo mkapewa bahasha ya transport haka kama hujapewa news yoyote, hiyo ni rushwa!.

Jana nilikwambia ntakupa darsa kidogo, na hili swali ni zuri kukuanzia hiyo dars kuhusu rushwa maana linahusu "lunch" au kula, pata darsa kidogo:

Hupaswi kupokea chochote cha ziada, kiwe kwa jina lolote kutoka kwa aliyekutuma mwajiri wako (source).

Kulikuwa kuna kisa cha wakusanyaji zakat (zakat collectors), wakati wa Mtume Muhammad (SAW) waliokwenda kuwafata watoa zakat na huko walipokwenda kukusanya zakat, walipewa zakat na zawadi, waliporudi kuleta makusanyo, wakatoa zakat kama walivyoikusanya na kubaki na zawadi, na walipoulizwa hivyo mbona hamvitoi, wakasema hizi ni zawadi tulizopewa, wakaambiwa, "hapana" ingekuwa hamjatumwa kukusanya zakat hizo zawadi mngepewa na hao? zote zikachukuliwa na kuingizwa "Beit L'mal" (hazina). Hapo utaona kuwa Uislam unakataza hata zawadi utazopewa na "source".

Pasco, hapo hauna ujanja wa kuchakuwa "ukweli ukidhihiri uongo hujitenga" wewe ni mpokea, mla na mgawa rushwa kwa kukiri mwenyewe, na hilo linakufanya uwe katika kundi la ufisadi, tena kama mwana habari unakuwa ni mtu hatari sana katika jamii. Hutufai hata kidogo, wewe na wenzako wote wanaopekea vibahsha vya "source" hakuna excuse utakaileta ikahalalisha hii dhambi kwa jamii.
 
Back
Top Bottom