Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #121
Tumefikia mahali pa zuri, maadam kila bahasha kwa waandishi kwako ni rushwa, then nakubaliana na wewe, na kwa vile imeanzia toka jikoni, unaonaje haya majina unayoniita mimi ungemwita na yeye?.Mpaka sasa hakuna ulichonikinaisha hata kimoja, na ikiwa itatokea nikaliona, basi mimi ndio wa kwanza kukiri hiyo ni halali yako. Lakini hili la kupewa vibahasha na "source" hata uniambie vipi, haliniingii kabisa.
Pasco,Mkuu Wacha1, hivi ulidhani wale waandishi wanaosafiri na Obama wanasafiri bure, wanakula bure na kulala bure?. Si wanapewa bahasha nene huko makazini kwao! Wanaotoa hizo pesa za hizo bahasha nene ni kina nani?.
Au unatazama na kusikiliza BBC ukijua ni bure tuu kama sadaka?!. Kila aliye Uingereza anakatwa pesa za kusikiliza na kuangalia BBC, usikilize, usisikilize, utazame, usitazame, unakatwa!.
5. Jee ni bahasha zipi ni rushwa?.
Baada ya kuzitaja bahasha ni bahasha genuine, sasa nitaziorodhesha bahasha ambazo ni rushwa.
Bahasha ya Kushinikiza Positive Covarage.
Hii ndio bahasha ya kwanza ya rushwa, hutolewa na source ili kuwa entice waandishi wawafanyie favourable covarage. Kwa kawaida bahasha hii inakuwa nene fulani, bahasha hii huandamana na obligation kuwa lazima story itoke. Bahasha hizi za shinikizo la story kutoka hazitolewi kwa waandishi wote, bali to only few selected, na kwa vile bahasha hizi ni rushwa, hutolewa kwa kificho!. Zile bahasha za halali kama za usafiri husainiwa wazi wazi na hukawiwa kila mtu akiona kwa sababu there is nothing to hide, lakini hizi hutolewa kwa kificho, no one will know nani amepokea bahasha na nani hajapokea kutokana mazingira ya usiri. Watoaji wa bahasha hizi wanajua ni rushwa na wapokeaji wanajua ni rushwa!. (to avoid conflict of interest, nawaombeni msiniulize zaidi kuhusu hizi!).
Mkuu Jasusi, what is the diference?, does it matter hiyo bahasha imetoka wapi au it maters mwandishi kawezeshwa kutimiza wajibu wake?. Ninachosema ni kuwa ili waandishi watimize wajibu wao, lazima wawezeshwe, kitendo chochote cha uwezeshaji waandishi, ni bahasha!, ili bahasha hiyo iwe rushwa, inategemea uwezeshwaji huo una lengo gani, kama uwezeshaji huo ni wenye lengo jema, then ndio huu ninauita basha nzuri!, kama uwezeshaji una lengo la kuimfluence news contents, then hiyo ndio rushwa!.Pasco,
Usichanganye na kumkonfyusi Wacha1.
Waandishi habari wanaosafiri na Obama katika Air Force 1 hawalipiwi na White House. Wanalipiwa na ofisi zao. Wanapewa fedha za kujikimu na matumizi ya safarini kutoka ofisini mwao. The White House bills their companies/corporations/news agencies when the trip is over. Tofauti na sisi akija hapa Michuzi ameandamana na Kikwete ni wazi kuwa kalipiwa na Ikulu na wala si Daily News. Hiyo ni tofauti kubwa sana na huwezi kuiita hiyo bahasha.
Mkuu Jasusi, what is the diference?, does it matter hiyo bahasha imetoka wapi au it maters mwandishi kawezeshwa kutimiza wajibu wake?. Ninachosema ni kuwa ili waandishi watimize wajibu wao, lazima wawezeshwe, kitendo chochote cha uwezeshaji waandishi, ni bahasha!, ili bahasha hiyo iwe rushwa, inategemea uwezeshwaji huo una lengo gani, kama uwezeshaji huo ni wenye lengo jema, then ndio huu ninauita basha nzuri!, kama uwezeshaji una lengo la kuimfluence news contents, then hiyo ndio rushwa!.
Jasusi, Michuzi akiwa Daily News kawezeshwa na Ikulu/MFA kuja Marekani, kapokea bahasha ili aweze kufanya kazi. Mwandishi wa CCN kawazeshwa na ofisi kuandamana na Obama, kafungashiwa fungu lake, libahasha hilo nene!, sasa utaita rushwa?!. Au hii ya Michuzi ndio rushwa ila ya CNN sio rushwa?.
Tanzania tunaishi kwenye object poverty, na media zetu ziko kwenye destitute hazina uwezo wa kumgharimia mwandishi wake aandamane na rais huko Marekani, Ikulu kwa kuujua umuhimu wa ziara hiyo, inagharimia waandishi kwenda Marekani na kuwagharimia, jee hiyo nayo ni rushwa?.
Mkuu Limbani, kusema ukweli, hii ni kweli ni kinyume cha maadili ya uandishi kwa sababu kitaingilia objectivity ya story na hivyo kushindwa kumaintain impatiality kwa kuripoti only the bright sides of the events. Nakumbuka mimi nimefundishwa Media Ethics na mwalimu Mkanada Patrick Walsh, akatuambia kule Canada, ni marufuku kwa waandishi hata kukubali offer ya cup of coffe, you have to pay!, hakuna cha mwaliko wa lumcheon wa dinner kwa source!.Pasco, mwenye wajibu wa kukuwezesha ufanye kazi yako ni mwajiri wako na sio client!! Unapopokea bahasha kutoka kwa mtu anayekupa habari tayari au unayetakiwa kuandika habari zake hiyo ni rushwa hata kama hajashinikiza uandike habari yake. Maana tayari hapo umepata "favour" na reporting yako kwako itakuwa tofauti na ya yule aliyekupa habari bila kukuwezesha!!
Safari za waandishi na Rais kama ni kweli zote zinagharamiwa na Ikulu nazo ni rushwa! Maana waandishi hawatakuwa na "uhuru" wa kuhoji/kuuliza mambo mbali mbali kuhusu ziara hizo. Wao kazi yao itakuwa ni kupiga picha na kuriport kile ambacho kitafurahisha Ikulu, hawatakuwa tofauti na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu!!
Pasco,'Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsor ships za Awords mbali mbalin kwa Waandishi, nazo Rushwa?.
Kuna mashirika na taasisi mbalimbali zinatoa fungu fulani kwa waandishi kuandika kuhusu jambo fulani, usually indepth, mfano Tanzania Media Fund, inatoa funding kwa journalist kuandika stories toka vijijini, au investigative stories. Hizi ni bahasha nene zenye kucover usafiri, chakula, malazi, kwa field trip hata za mwezi mzima, nyingine ni attachment mahali kwa muda hadi miezi 6, hizi nazo ni bahasha, jee nazo ni rushwa?. No hizi ni bahasha safi!.
Mashirika/ makampuni au taasisi huweza kugharimia kukundi cha habari kuandika about specific news, hii inaitwa sponsorship mfano TAMWA ON FGM, TGNP dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia, JET thidi ya uharibifu wa mazingira etc. Bahasha nene hotolewa ili waandishi waandike kusu specific topic, hizi nazo rushwa?. Mifano iko mingi, mia kidogo ambapo bahasha hutolewa kwa waandishi genuinely na sio rushwa!. Wale mnaolazimisha kila bahasha kwa mwandishi ni rushwa, nawaombbeni sana mthink twice, tubishane kwa hoja na sio kulazimisha hoja!
...Sasa kama uwezeshaji huu unaiuta rushwa!, hebu muulize Rais Kikwete huwa anawapa nini wale waandishi wa habari anao safiri nao?!. Kama kweli kila anaetoa bahasha kwa waandishi lazima aende jela, naomba tuanzie na Ikulu, nami jela nitajipeleka mwenyewe bila hata kusubiri kutafutwa!....
Mkuu Jasusi, tangu nimepandisha hii thread jana, leo sasa ndio kwa mara ya kwanza naanza kufarijika!, hapo kwenye bold its now sasa we go together!, hiyo ndio genuine admission ya kwanza kuwa sio kila bahasha ni rushwa!. Umekubali kuwa grants na fellowships sio rushwa!. Jee grants na fellowships sio rushwa kwa sababu gani ili hali nazo ni bahasha walizokunjiwa waandishi?!. Naamini Bahasha za Grants/ Followships/Scholarships na Sponsorships za Awards mbali mbalimbali kwa Waandishi sio rushwa kwa sababu, japo ni bahasha waandishi wanazopewa ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao vizuri, enabling them, emporing them bila kuinfluence wanachoripoti, sasa baada ya kukubaliana kuwa kuna bahasha ambazo waandishi wanashikishwa ni rushwa lakini sii kila bahasha ni rushwa!.Pasco,'
Grants na fellowship si rushwa. Hizi hazitolewi ili mwandishi aandike mazuri tu ya yule anayetoa hiyo pesa. Nilienda Rumbek, Southern Sudan mwaka 2000 kushuhudia "decomissioning of the child soldier." Ofisi yangu ilinilipia nauli na kwa sababu hakukuwepo hoteli huko, UN ikanilipia malazi na chakula kwenye kambi yao. Niliandika ripoti juu ya zoezi hilo ambalo lilikuwa organized na UNICEF. Nilipata interview na Mkurugenzi wa UNICEF na pia nikazungumza na Salva Kiir ambaye ndiye leo rais wa South Sudan. Coverage ya kazi za NGO's ni muhimu for the public na vile vile NGOs zinapenda kupeleka makao makuu ripoti ya coverage ya kazi zao. Hapo ni win win kwa pande zote. Lakini sitakubali BP wanilipie ili niandike story kwamba wamefanya kazi nzuri ya kusafisha ufukwe wa New Orleans baada ya ile oil spill. Ni afadhali niende mwenyewe independently na kama wamefanya kazi nzuri nifikie uamuzi huo bila kushawishiwa na bahasha.
Swali dogo kwako, rushwa ni fedha yoyote kwenye bahasha haijalishi ni kwa malengo yepi au rushwa ni fedha inayotolewa kwa malengo?.
Bahasha za Usafiri, Lunch na free bies nazo ni rushwa, jee wakati gani ni Rushwa?.
Kwa mliofuatilia pale mwanzo nilisema, bahasha ya usafiri ikitolewa kwa lengo la kuwawezesha waandishi kufika eneo la tukio bila kuingilia wataripoti nini, hiyo sio rushwa, ila bahasha hiyo hiyo inapotolewa kwa kuitwa hivyo hivyo usafiri kwa lengo la positive covarage, then bahasha hiyo ni rushwa!. Baada ya taarifa uchavuzi wa mazingira ya mto Tigiti, Barrick waliandaa ripoti yao positive na kuwagharimia waandishi na walioandika Barick ilichotaka!. Hiyo provision ya usafiri kwa waandishi uliofanywa na Barric kweli ni ku facilitate ili kupata positive coverage, hivyo unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa na rushwa, na unaweza kuwafacilitate waandishi ikawa sio rushwa!. The deviding line is very thin ndio maana sishangazwi na wale wanaoona kila bahasha ni rushwa!.
Vivyohivyo offer za lunch, dinner na vijizawadi zawadi, kuna wakati ni rushwa na kuna wakati sio rushwa!. Ukienda semina warsha au kikao, wajumbe wote wakapowa sitting allowances zao, wote mkala lunch, au zile event, waalikwa wote wanapewa vijizawadi na waandishi wakiwemo, then sio rushwa, lakini waandishi mkiitwa mahali, hakuna event yoyote, mkapigwa lunch ya nguvu na baada ya hapo mkapewa bahasha ya transport haka kama hujapewa news yoyote, hiyo ni rushwa!.