Mkuu Pasco, kwanza hongera kwa maelezo yako mazuri. Mimi naomba unisaidie kitu kimoja. Wapo waandi wa habari za uchunguzi ambao nao hulazimika kutoa bahasha kutoka mifukoni mwao ili wapate habari. Hiyo nayo ni rushwa? Ama sawa kufanya hivyo.
Mkuu Jumakidogo, kwanza asante kunipa hongera, na asante kuibua hii issue ya 'rushwa halali', justified corruption!. Katika sekta zote za uandishi wa habari, uandishi wa habari za uchunguzi ndio mgumu kuliko fani zote, sisi waandishi tunaitana 'wapiganaji', na wale wakongwe au wahariri tunawaida 'makamanda' hivyo waandishi wanaondika habari hizi za uchunguzi wanapaswa kuitwa "makomandoo" ndio maana waandishi kama Jerry Muro wanamiliki bastola na pingu kihalali!.
Undishi wa habari za uchunguzi kwanza unahitaji kipaji maalum, mwandishi husika lazima awe na 'sharp nose for news' kuweza kutambua habari zaidi ya habari ili afanya investigative journalism. Lazima awe na "curiosity" ya ziada kubaini some hidden agendas, lazima awe jasiri na uwezo wa subra ya hali ya juu pamoja na uvumilivu na ustahimilivu ili kupata anachokitaka!.
Mashirika yote ya kijasusi hata TISS yetu inatoa rushwa kwa watu wanaitwa ma "informer" wake wenye jukumu la kutafuta taarifa zozote nyeti. Hawa ma informer ili wapate taarifa hivyo most of the times, wanatoa rushwa ili kuzipata taarifa hizo, hizi ni rushwa halali!. Sasa mwandishi wa habari za uchunguzi, sio tuu ana risk maisha yake, bali pia sometimes hulazimika kutoa chochote ili kupata unachokitaka, hiyo rushwa sometimes ofisi itakurudishia ukiweza ku account for au sometime inakula kwako!.
Wakati wa yale mauaji ya Zanzibar ya January 200I, nilikwenda kucover kwa media fulani, polisi ikatangaza kuwa walitumia risasi za moto baada ya kutumia rubber bullets kutozaa matunda!, ikanibidi nimpe kidogodogo polisi fulani incharge wa amoural ya polisi Zanzibar kumuomba anionyeshe rubber bullet inafafanaje! Huyo polisi akanithibitishia Zanzibar hawana rubber bullets!. Wakati wa press conference ya polisi Zanzibar, nikaomba nionyeshwe hiyo rubber bullets inafafanaje, au tuonyeshwe vishina vya hizo risasi bandia zilizotumika, polisi wakang'aka sio jukumu la polisi kuwaonyesha raia silaha, hizo ni siri za jeshi!.
Jioni ile nikaripoti kuwa japo polisi Zanzibar wamedai kutumia risasi bandia, wameshindwa kuonyesha uthibitisho wowote wa uwepo wa risasi hizo, hivyo story ika conclude kuwa polisi wa Zanzibar wamewamiminia risasi za moto waandamanaji Zanzibar na kuua 22!.
Kesho yake nilishikwa na kutiwa ndani Mwembemadema for two good days!.
Kwenye bahasha za uwezeshaji, nimeitaja TMF kutoa fungu kwa waandishi ili waandike habari za uchunguzi na habari za vijijini na nikasisitiza bahasha hizi sio rushwa!.
Vyombo vya habari vya Tanzania vinakabiliwa na ukata wa kufa mtu, baada ya Mzee wa vijisenti kuthibitika ana vile vinjisent, ingekuwa ni nchi za wenzetu vijana wa kazi wangeibuka na investigative story yenye inside out!. Huku tunabiri tuu press conference, semina, warsha na makongamano only!