Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imetakiwa kuhakikisha kuwa waandishi ambao maombi yao yamekamilika na kuthibitishwa wanapatiwa vitambulisho kwa wakati, kwani kumekuwa na malalamiko kuhusu ucheleweshaji mkubwa katika utoaji wa vitambulisho hivyo.
Aidha, kumeelezwa kuwa ubora wa vitambulisho hivyo ni wa chini, kwani baadhi vimeanza kufutika maandishi na picha hata kabla ya muda wa miaka mitatu, jambo linalohatarisha utambulisho wa waandishi mbele ya mamlaka na wadau wa sekta ya habari.
Waandishi wameshauri bodi hiyo kuboresha mfumo wa utoaji na ubora wa vitambulisho ili viwe na uimara wa kudumu muda mrefu bila kuharibika mapema.