Tetesi: 'Waandishi wa Makonda' kwenda Ziarani Koromije

Tetesi: 'Waandishi wa Makonda' kwenda Ziarani Koromije


Kama anazushiwa amefoji vyeti, kwa jinsi anavyopenda makuu angeshawakamata wote wanaomsema. Eti anatafuta watu wa kumsaidia, anazama peke yake!
Kwakuwa hajawakamata mahakama gani imethibitisha kuwa kafoji vyeti?
 
Hivi kweli katika watu million 50 amekosekana hata moja tu wa kuweka ushahidi walau attendance list ya wanafunzi waliosoma Koromije primary au Pamba secondary ili kutuonyesha mwanafunzi aliyesoma pale aliitwa Daudi badala ya Paulo na kwamba Paulo hakuwepo kwenye hayo madarasa!!?



Attendance list inaweza kupikwa mkuu. Necta ndiyo wana kila kitu. Watusaidie kuweka wazi matokeo ya Pamba Sek kwa mwaka anaodaiwa Bashite alisoma hapo na Matokeo ya Paulo Christian M kwa shule aliyosoma...!! Hapo ndipo mzizi wa fitina utakuwa umekatwa...!!

Mbona yule mkurugenzi aliyeteuliwa na kudhaniwa hana master ushahidi ulitolewa faster...!!?? Kwa nini kwa huyu ni kigugumizi hivi...!!??

WACHA MANENO, PELEKA VYETI...!!








Tafakari...!!
 
Wanamchokoza Gwajima na Mange Kimambi tena
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama ni kweli hujamaa hajuwi anacho kifanya kwaiyo anataka kufanya wa Tanzania wote na tasisi zote kuwa ni mabwege yeye ndie mjanja duh au Rais ana nguvu kuliko wana nchi kasahau kuwa alishakimbilia south AFRICA
angekuwa na nguvu angepiga pushup!!!!!!!!!!!
 
Kiongozi wa Mkoa anayesemekana kutumia jina lisilo lake ameandaa ziara ya Waandishi 10 watakaondoka kesho kuelekea Mkoani Mwanza. Waandishi hawa watakuwa na kazi maalumu Jijini Mwanza, katika Sekondari ya Pamba na Kijijini Koromije.

Kulingana na hadidu za rejea za ziara hii, waandishi watakutanishwa na kuongea na ndugu pamoja na walezi wa Kiongozi wa Mkoa na watatembelea Sekondari ya Pamba—Mwanza. Katika Sekondari hii watapata wasaha wa kupewa taarifa mbalimbali kuhusu Kiongozi wa Mkoa na kuongea na uongozi wa Sekondari.

Baadaye waandishi wataelekea Kijijini Koromije ambako watatakiwa kuwahoji watu kulingana na orodha iliyotolewa na Kiongozi wa Mkoa.

Kazi itakamilika kwa kuandaa taarifa katika mifumo mbalimbali ya kieletroniki (maandishi, sauti na video) zitakazolenga kuonyesha kuwa yote yaliyosemwa na kushuhudiwa juu ya Kiongozi wa Mkoa ni uongo. Taarifa kamili kutoka katika ziara hii zitarushwa mitandaoni na kupelekwa kwenye vyombo vya habari.

Lengo la ziara hii si kuibua ukweli bali kutaka kuufanya ukweli uchanganyikiwe kama njia ya kufifisha sakata la “BASHITE” Ifahamike kwamba huu ni muendelezo wa mikakati ya Mwana Kipenzi cha Mfalme baada ya kufurahia keki ya mwaka mmoja madarakani. Nakuuliza; hivi mawaziri waliambiwa wakibainika kufanya sherehe baada ya kuteuliwa watafanywa nini?
Wakimaliza huko kolomije nashauri watumwe TRA kusafisha documents zinazoonyesha gari anazotumia ni za watuhumiwa wa madawa ya kulevya.Halafu wakimaliza TRA nashauri wahack mitandao yote ya kijamii ambayo ina ushahidi wa habari zake wazifutilie mbali. Baada ya hapo wahack akili za watanzania wote Ili wafute kumbu kumbu zetu.
 
Hiyo timu iliyoenda ndo inaongozwa na le mutuz pamoja na steve panya
 
Back
Top Bottom