Waandishi washambuliwa Ngorongoro huku Mbunge akihusishwa katika tukio hilo

Waandishi washambuliwa Ngorongoro huku Mbunge akihusishwa katika tukio hilo

Kuna mambo yanakera sana sana, mnajifungasha huko mnapewa perdiems na marupurupu kwenda kuwarubuni wananchi wa Ngorongoro!

Mwandishi wa habari tangu Lini akawa muelimisha Jamii? Why tunaingilia KAZI za watu? Tamaa mbaya saaana, haya mmevuna mlichokipanda.

View: https://twitter.com/MariaSTsehai/status/1691549136854597643?t=PECXdHbXKn_hmz38HK12-Q&s=19View attachment 2718672View attachment 2718673View attachment 2718673View attachment 2718674

Lingeuwawa tu funza hilo.
 
Kulazimishwa kutelekeza Utamaduni wako, Maeneo yako ikiwemo maeneo walipozikwa Mababu, Mabibi, Wajomba, Shangazi, Watoto, wajukuu katika eneo lako,ili kuja kumpisha Mwarabu kwa jina la Uwekezaji ni karaha.

Wamasai wameteswa na Serikali yao ikishirikiana na waarabu mpaka wamehamishwa kwa Nguvu kubwa sana. Kisa? "Uwekezaji"
Kilichotokea kule ni angamizo la Kabila la watu wa Wamasai.

Wana haki ya kuwa na hasira hizo hadi,(nadhani) kuwatwanga.
Sasa bado Tanganyika, mmewaachia huko kwa Wamasai(they set precedent) na hawatarudi nyuma, ngojeni wasaini zile thelathini zingine tuone hawa Waandishi watatufikisha wapi.
 
Duh pole sana waandish. Sio enduren.ni endulen hapo kama unaenda ormekeke. Hao jamaa sime nje nje.sidai ashenalee
 
Wamewaweza kweli kwa sababu waandishi wa habari wa sasa wanataka kuifurahisha serikali na kamwe hawaandiki ukweli.
 
Naona Wamaasai wameamua kulinda ardhi yao kama ilivyokuwa kwa mashujaa wa Unyanyembe au chifu Mukwanyivika...

Hii iwe funzo hata kwa viongozi wetu ya kwamba rasilimali za nchi ni za kulindwa at all costs
 
Ee Mungu turehemu waja wako tunakusihi, yote haya ni matokeo ya kukuasi wewe kwa tamaa za kitambo tu za kuwaza anasa na mali za dunia hii na kupelekea mafarakano miongoni mwetu.
SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WA CRISDA RODRIGUEZ KITANDANI

Kabla ya kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 40 kutokana na kuugua maradhi ya saratani ya tumbo, mbunifu na mwandishi maarufu duniani Mrembo Crisda Rodríguez aliandika maneno haya akiwa kitandani na kuyahifadhi kwenye diary yake ndogo:

1. Nilikuwa na gari la gharama kubwa zaidi duniani katika karakana yangu lakini sasa inabidi nitumie kiti cha magurudumu.

2. Nyumba yangu inauza kila aina ya nguo zenye chapa, viatu, na vitu vya thamani, lakini sasa mwili wangu umefungwa kwa kitambaa kidogo nilichopewa na hospitali.

3. Nina pesa nyingi benki. Lakini sasa sinufaiki na kiasi hiki.

4. Nyumba yangu ilikuwa kama ngome lakini sasa ninalala katika vitanda viwili hospitalini.

5. Kutoka hoteli ya nyota tano hadi hoteli ya almasi. Lakini sasa hivi mimi hutumia muda katika hospitali kuhama kutoka maabara moja hadi nyingine

6. Nimetoa saini za mamia ya watu lakini safari hii kumbukumbu za matibabu ni sahihi yangu.

7. Nimekuwa na vinyozi saba wa kurekebisha nywele zangu, lakini sasa - sina hata unywele mmoja kichwani mwangu.

8. Kwenye ndege ya kibinafsi, naweza kuruka popote, lakini sasa ninahitaji usaidizi wawili ili kutembea hadi lango la hospitali.

9. Ingawa kuna vyakula vingi, sasa mlo wangu ni vidonge viwili kwa siku na matone machache ya maji ya chumvi usiku.

10. Hii nyumba, gari hili, ndege hii, samani hii, benki hii, sifa na umaarufu kupita kiasi, hakuna hata kimoja chenye manufaa kwangu. Hakuna kati ya haya kitakachonipumzisha. "Hakuna kitu halisi isipokuwa kifo."

Mwisho wa siku, utajiri mkubwa zaidi kwenye maisha ya binadamu ni afya njema yake.

Kama umejaaliwa kuwa na afya njema japo kwa kiasi kidogo, furahia maisha yako kwa hata kwa chochote kidogo ulichonacho. Kuna watu wanatamani kuinunua afya yako kwa gharama yeyote ile kama ingewezekana, kwa sababu kwa tafsiri sahihi kwako dhidi ya wewe unayemiliki furaha itokanayo na afya yako, wewe ni tajiri mno.
 
Mkurugenzi wa Gazeti la Jamvi la Habari Habibu Mchange na waandishi wa habari wapatao sita wamevamiwa na kundi la Vijana wa kimasai na kujeruhiwa vibaya walipokuwa wakifanya mahojiano na wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kijiji cha Endureni wilayani Ngorongoro ni Denis Msacky, Ferdinand Shayo. Akizungumza na Jambo TV ndugu Habib Mchange amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Mhe. Emanuel Oleshangai kuratibu mashambulizi hayo ambapo.

Jambo TV imefanikiwa kuzungumza na Mbunge Oleshangai kuhusiana na tuhuma za kuratibu mashambulizi hayo kwa wanahabari ambapo amekanusha vikali kuhusika na uhalifu huo huku akisema hana sababu ya kuratibu mashambulizi kwa wanahabari hao.

Oleshangai amesema Endureni ni kijijini kwake na aliwaona hao waandishi wa habari wakiwa mnadani wakiwakusanya watu kwa ajili ya kuzungumza nao huku yeye na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CCM wakila nyama na baadae akaondoka kurejea nyumbani kwake.

Oleshangai amesema alipofika nyumbani kwake ndio alipata taarifa ya kutokea kwa fujo hizo hivyo hahusiki nazo.

============

Wana bahati wangewaua kabisaa wasaliti kama hao. Waandishi makanjanja kama hao wanao tumika na Dp world mimi nasema muwapige tuu popote wakijitokeza kuleta urongo wao. Taifa limevamiwa yenyewe yanapewa bahasha kuzurula kushabikia uvamizi wa waarabu.
 
Mimi nasikitika tu ni kwa nini Maulid Kitenge hakuwemo kwenye huo msafara?
 
Kuna mambo yanakera sana sana, mnajifungasha huko mnapewa perdiems na marupurupu kwenda kuwarubuni wananchi wa Ngorongoro!

Mwandishi wa habari tangu Lini akawa muelimisha Jamii? Why tunaingilia KAZI za watu? Tamaa mbaya saaana, haya mmevuna mlichokipanda.

View attachment 2718701View attachment 2718702
Situliambiwa wananchi waliobaki Ngorongoro wa naomba kuhamishwa? Imekuweje tena?

Nilidhani udalali ni bandari tu kumbe mpaka maisha ya watu kuna mashetani yanajifanya kudalalia? hii nchi imelaaniwa.
 
Sometimes huwa nafikilia sana kunapotokea matukio flani kama lile la kuhamishwa wamasai na baadhi yetu kuona nafasi ya kwenda kuwahoji ni haki na wajibu.

Hata kama ni haki na huru bado kuna haja hasa kabla ya ku8ngia maeneo hayo kufanya upembuzi yakinifu kupima hali ya upepo.
 
Mkurugenzi wa Gazeti la Jamvi la Habari Habibu Mchange na waandishi wa habari wapatao sita wamevamiwa na kundi la Vijana wa kimasai na kujeruhiwa vibaya walipokuwa wakifanya mahojiano na wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kijiji cha Endureni wilayani Ngorongoro ni Denis Msacky, Ferdinand Shayo. Akizungumza na Jambo TV ndugu Habib Mchange amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Mhe. Emanuel Oleshangai kuratibu mashambulizi hayo ambapo.

Jambo TV imefanikiwa kuzungumza na Mbunge Oleshangai kuhusiana na tuhuma za kuratibu mashambulizi hayo kwa wanahabari ambapo amekanusha vikali kuhusika na uhalifu huo huku akisema hana sababu ya kuratibu mashambulizi kwa wanahabari hao.

Oleshangai amesema Endureni ni kijijini kwake na aliwaona hao waandishi wa habari wakiwa mnadani wakiwakusanya watu kwa ajili ya kuzungumza nao huku yeye na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CCM wakila nyama na baadae akaondoka kurejea nyumbani kwake.

Oleshangai amesema alipofika nyumbani kwake ndio alipata taarifa ya kutokea kwa fujo hizo hivyo hahusiki nazo.

============

"Watetezi" wa haki za binadamu mbona siwasikii kwenye hili?
 
Back
Top Bottom