Waanzilishi wa jukwaa la GigSpace wawaasa vijana kutumia fursa za teknolojia ya mtandao

Waanzilishi wa jukwaa la GigSpace wawaasa vijana kutumia fursa za teknolojia ya mtandao

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Ofisa Mtendaji Mkuu na mbunifu wa jukwaa la Gigspace, Ashura Babi, akiwa na mwanzilishi mwenza, Steve Mawalla, wamesema waliamua kuanzisha jukwaa hilo kwa ajili ya kuwaongezea na kuwafungulia vijana pamoja na wafanyakazi fursa pia za ajira kupitia mtandaoni.

Akizungumza katika mahojiano na Nipashe, Ashura, alisema waliona changamoto za watu kupata ajira baada ya kuhitimu masomo inakuwa kubwa, hivyo wakaamua kuanzisha jukwaa hilo ambalo linakuwa linaunganisha mfanyakazi na kampuni binafsi.

“Lengo kuu la jukwaa ni kuunganisha mfanyakazi ambaye ana kazi, ila anakuwa anafanya kazi akiwa huru mtandaoni pamoja na wale ambao hawana ajira wanajisajili kwa fani zao na tunawaunganisha na kampuni za kibiashara na wanatimiza malengo ya maisha yao kwa kujisajili kupitia tovuti ya Gigspace,” alisema Ashura.

Ofisa huyo alisema kuwa kwa kutumia mtandao huo, kampuni nyingi ambazo zitakuwa zinafanya kazi ndani ya jukwaa hilo zitakuwa zinalipa kodi ya serikali kwa makato ambayo ni nafuu, lakini pia ulipwaji wa wafanyakazi unakuwa ni wa kiwango ambacho siyo umiza kwa kampuni za biashara na wafanyakazi hao.

Steve Mawalla, muanzilishi mwenza wa jukwaa hilo, alisema kuwa watu wengi wanaingia mtandaoni kutafuta taarifa ambazo hazina tija na manufaa kwao, lakini kupitia jukwaa hilo wakiingia watapata taarifa ambazo zitawasaidia na kutumia fursa zilipo.

“Katika jukwaa letu kuna fanikama vile wauhasibu, wasanifu majengo, wahandisi, wanahabari, wanasheria, na watunga sera za kibiashara,” alisema Mawalla.

Mawalla alitolea mfano kwa wanawake ambao wameolewa na baadhi wamesoma na wana ujuzi mzuri, lakini wako nyumbani wanalea watoto bila kujua kuwa wana fursa ya kujiingizia kipato kwa kutumia jukwaa hilo la mtandaoni.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom