Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Baitul haram iliyopo Makka ndiyo nyumba ya mwanzo duniani kujengwa kwa ajili ya kumuabudu Mungu (Allah).
Nyumba hii iiinuliwa kuta zake kwa mara nyengine na nabii Ibrahim na mwanawe Ismaili.Katika historia ndefu ya nyumba hii ni kwamba imewahi kupitia mikononi mwa makafiri na washirikina.
Mwaka aliozaliwa mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ambao unatajwa ni mwaka 572 kwa kalenda ywaroma nyumba hiyo ilikuwa ikiangaliwa na babu yake mtume swalaLlaahu alayhi wa sallam.Watu hasa waarabu walikuwa wakitoka miji mbali mbali kuja kufanya ibada zao kwenye nyumba hiyo.
Mfalme wa Yemen aitwaye Abraha aliona wivu kwamba watu wote hao wanakwenda kuabudu Makka kwenye nyumba hiyo na kuacha kwenda kuabudu kwenye jengo alilojengwa yeye kwa madhumuni kama hayo.Hivyo akaamua kwenda kulivunja jengo hilo.
Abraha akatoka na jeshi lake kubwa la tembo na siku alipokaribia kufika Makka akapeleka ujumbe kwa kiongozi wa Makka anayeangalia msikiti huo ambaye ni Abu Muttalib,babu yake mtume SAW.
Abu Muttalib akajaribu kurudisha ujumbe ili kumsihi Abraha asitekeleze azma yake ya kuivunja alkaaba lakini akakataa na kuelezea nia yake kwa mkazo ya kuingia mjini hapo kwa kazi iiyomleta.
Kuona hivyo na kwa kujua ukubwa wa jeshi la Abraha na udhaifu aliokuwa nao bila maandalizi yoyote,,mzee Abu Muttalib akajisemea nyumba ile ni ya Mwenyezi Mungu na yeye ndiye atakayeilinda.Akaongozana na watu wake na kukimbilia milimani jirani na Makka.
Kweli jeshi la Abraha likaendelea na safari na kweli wakakutana na mlinzi wa nyumba hiyo asiyeshindwa na jeshi lolote lile duniani.Wakatumwa ndege waliobeba vijiwe vitatu vitatu,kila kimoja mguuni na kimoja mdomoni vikiwa na majina ya askari wa Abraha.Vijiwe hivyo vilikuwa ni udongo kutoka jahannam.Kila kimoja kikampiga askari aliyekusudiwa na kubaki kama kinyesi.
Hizi ndege za kivita za kisasa fikra yake inapatikana kwenye uislamu na imetokea kwenye Quran suratul Fiil ambayo imeeleza maangamizi hayo ya jeshi la Abraha.
Tukirudi kwa waarabu wa leo,tutaona kuwa wamependa sana wafananishwe na babu yake mtume rehma na amani zimshukie,lakini hawafanani kabisa.
Mwenyezi Mungu amewapa silaha zote na neema za kuweza kuilinda masjidul aqswa na kuwalinda wapalestina dhidi ya jeshi la mayahudi chini ya Netanyahu na wasiuliwe kama kuku kwa njia dhalili za kuwategeshea chakula.
Allah hutenda kwa mipango yake na kwa muda anaopenda.Kwa sisi binadamu tunaoumizwa na hali mbaya inayowakabili wapalestina hasa wa Gaza,tukiwa tukiwa waislamu na wa dini nyengine na wa makabila tofauti.
Tungepewa uchaguzi wa nini kifanyike basi tungeona adhabu ambayo ililipata jeshi la Abraha na kumhifadhi babu yake mtume SAW ,basi adhabu kama ile imuendee Netanyahu na jeshi lake sawa na waarabu wote ambao wamekaa kimya wakiangalia akinamama na watoto,wazee kwa vijana wa Gaza wakiangamizwa mbele ya macho yao.