Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Raha ya kusoma ni kwamba kila mtu anafahamu kivyake, yaani huwa hatufanani. Nimemfahamu Ali Muhsin kwamba watarudi kwao Zanzibar kwani wakati huo walikuwa wakimbizi. Ila swala la Afrabia likitokea kwa muktadha alouelezea Dr. Ghassan sio mbaya.Je mnakumbuka kitabu cha Dr. Harith Ghassany aliyeandika kitabu chake cha Kwaheri Ukoloni kwaheri Uhuru, ambacho Mzee wetu Mohamed Said(Yumo humu) alikuwa ni research assistant wa kitabu hicho. Mzee wangu Mohamed Said najua una mengi ya kuzungumzia kitabu kile ambacho kwa kiasi kikubwa kilinifahamisha mengi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.
Hata hivyo, mada yangu ya leo sio kuhusu mapinduzi ya Zanzibar wala Muungano maana kitabu kile kina sentensi nzuri niliyoihifadhi tangu nipate kukisoma "Muungano umeficha siri za mapinduzi" kama nitakuwa nakumbuka vyema. Mapinduzi ya Afrabia yameelezewa vizuri sana katika kitabu kile cha Daktari nguli wa falsafa (PhD)
Katika Chapter ya 18, Dr. Harith ametuwekea Mahojiano yalisajiliwa Cairo mwaka 1975 na hayakufanywa na mwandishi wa kitabu. Mahojiano yalikuwa ya Marehemu Sheikh Ali Muhsin wa mwaka 1975 ambapo
ndio kwanza alipotoka jela ni tafauti na Sheikh Ali Muhsin wa siasa za baadae za Zanzibar katika kipindi cha siasa za vyama vingi.
Ali Muhsin alikuwa waziri wa mambo ya nje ya Zanzibar kabla ya mapinzudi, ambapo baadae alishikiliwa jela Tanganyika kabla ya kuachiwa mwaka 1974.
Katika mahojiano hayo, zaidi ya mara moja Ali Muhsin amezungumza zaidi ya mara moja kuwa "Inna aaidun! Tutarudi" Soma uk 239 & 241
View attachment 2664353
View attachment 2664354
Sijui kuhusu harakati za Afrabia zimefikia wapi, kwa wasiojua, Afrabia ni muungano wa Africa na Arabia, ambao kwenye kitabu wameandika
"Kwa ajili ya Wazanzibari na Watanganyika kwa ujumla wao ili kitabu hichi
kiwawezeshe kuzibadilisha nafsi zao. Waweze kuona fursa za mapenzi na neema zilizopo kwao wao na kwa ndugu na majirani zao wa jadi, na kisha wafanye kazi kwa pamoja katika kujenga Muungano Mpya na uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia—utakaosimama juu ya ukweli na hivyo kuimaliza kabisa mitikisiko na misukosuko ya muda mrefu." Uk Viii
View attachment 2664357
Je, yanayoendelea ni harakati za mapinduzi ya Afrabia?
Sign OLS
Sio bongo tu, dunia mzima, machester city, PSG na Man U na wao wako njiani. Ukienda UK nako london karibu yote ni mali ya warabu. Wenye hela ndio wao kwa sasa kwaiyo tupunguze wivu na tukubali matoke.Waarabu kila mahali🐒🐒🐒View attachment 2665048
Wanakuja ki Biashara, au ulifikiri wanakuja kuwekeza kwenye Bandari kwaajili ya uzuri wa sura zenu?Wageni wote tangu enzi nchi zao zilikuwa vizuri, ila walivamia, kwani unadhani wajerumani, waingereza, wareno, waarabu walivyokuja Afrika ilikuwa ni kwasababu ya maendeleo ya Afrika ukilinganisha na nchi zao au ni kutokana na umuhimu wa Afrika kwa maendeleo yao?
Rwanda na Kongo ni Machaka ya Wahalifu Wa Kimagharibi Kama ilivyo Falme za Kiarabu.Wakati mkiendeleza mawazo ya vitabu vya historia huko DRC na Rwanda wameshaingia mkataba na DPW tayari.
Tatizo ni Wageni kupewa Nchi yetu .Munaendelea kijidhihirisha, Kumbe tatizo ni Uarabu. Wabaguzi wakubwa
Hukuona Mali za Wazungu zikitaifishwa miaka ya sitini baada ya uhuru. ? Hukuona watu wakiandamana kupinga Wazungu kupewa gesi kule Mtwara?. Hukuona Mrema akipinga Wazungu kule Bulyankulu.Huoni migogoro ya Kule kwenye migodi ya wazungu Mara?Siku zote nilisema shida sio mkataba chuki zipo Kwa waarabu tu nikatukanwa.Ila wangepewa Wazungu kusingekuwa na kelele.
Hizi hekaya hazitusaidii zinatuacha na ulofa wetu wa miaka yote. Tunajifanya matajiri wa maadili wakati ni makapuku wa masuala mengine yote ya kimaisha.Rwanda na Kongo ni Machaka ya Wahalifu Wa Kimagharibi Kama ilivyo Falme za Kiarabu.
Dubai ni jiji la raha na starehe za Kila namna . Jiji la kishetani Karika nchi ya Kiislam.
Hata Ulaya ilianza ilipofanikiwa sana ndipo ilipokuja na wazo la kutafuta rasilimali Afrika kupitia mikataba ya kilaghai Kama waliyotuwekea CCM na Serikali yake Kwa DPW
Kama ambavyo Zanzibar ya Raisi Mwinyi inaitesa sana Tanganyika kupitia Raisi Samia......watanganyika bana, munatesa sana na Zanzibar
Kama ambavyo Zanzibar ya Raisi Mwinyi inaitesa sana Tanganyika kupitia Raisi Samia......
Wanasema "What's good for the goose, is also good for the gander"
Tungekuwa hatutaki usawa kama unavyodai hapa, sidhani wazanzibari kama Bakhresa, Mwinyi, Dr Salim na wengine wangeruhusiwa hata kumiliki ardhi huku Tanganyika. Ardhi siyo suala la muungano lakini bado wapemba wengi wanamiliki maelfu ya hekta za ardhi ila sisi watanganyika huwezi kutusikia tunalalamika hata siku moja au kuwafanyia vurugu.wakati Jiwe anachagua baraza la mawaziri ambalo hata mzenj mmoja hakuwemo muliona ni sawa tu, sasa hivi munalia kwa kuwa na wao wamepata ulaji. Tatizo lenu ni kuwa hamutaki usawa, bali munataka always muwe munawanyonya wao. na ndio mana malalamiko yamekuwa mengi.
Tungekuwa hatutaki usawa kama unavyodai hapa, sidhani wazanzibari kama Bakhresa, Mwinyi, Dr Salim na wengine wangeruhusiwa hata kumiliki ardhi huku Tanganyika. Ardhi siyo suala la muungano lakini bado wapemba wengi wanamiliki maelfu ya hekta za ardhi ila sisi watanganyika huwezi kutusikia tunalalamika hata siku moja au kuwafanyia vurugu.
Ardhi ndiyo utajiri mkuu wa Tanganyika, ila tunawapa wazanzibari ruhusu kuja kuishi kwetu....