kwanza kabisa hapo kwenye maeneo matakatifu ya kiislamu yote yapo uarabuni sio kweli, kuna maeneo yapo israel, mengine ya uajemi, mengine yapo hata hapa Tanzania unaweza kudhuru misikiti ya zamani, ni vile tu yale maeneo ya uarabuni yametajwa tangu mwanzo katika Quran na kama Makka ni lazima kwenda kwa muislamu mwenye uwezo ila si kweli hakuna maeneo mengine matakatifu kwa waislamu.
halafu kuhusu kiarabu kuonekana ndio lugha rasmi ya ibada, unapaswa ujue dini zote zilikuwa hivyo huko mwanzo,
na kwamba hadi leo hii wayahudi lugha yao takatifu ni kiebrania hata wakisali husali kwa lugha hiyo, wakatoliki walizungumza na kusali kilatino hadi pale Papa wao aliposema inaruhusiwa kusali lugha ingine, ila ukienda vatican hadi kesho wanatumia kilatini ijapokuwa kuna lugha ya kiitaliani ambayo ndio lugha izungumzwayo maeneo kuzunguka vatican yote,
wahindu hadi kesho kutwa wakisali hawasali kihindi wanasali kwa kutumia lugha ya kale iitwayo sanskrit
na uonapo waislamu wasio waarabu wamevaa hijab ama makanzu jua tu ni kutokana na aya za Quran, ukisoma mafundisho yake utapata kuona vazi la hijab limeelekezwa liwe kama lilivyo, wakati kanzu halina maelekezo ya moja kwa moja, ila linaonekana linaendana sana na maelezo ya stara anayopaswa mtu wa kiislamu wa kiume awe nayo, kama vile kuvaa nguo kuvuka magoti, na kuvaa nguo kufunika kifua , halafu haibani
kuhusu waislamu wote kuwa eti wanalazimika kuwa na utamaduni mmoja sio kweli, waislamu tupo wa aija nyingi, muislamu wa saudi arabia na waafrika wana mitazamo tofauti, muislamu wa malaysia ana mtazamo tofauti na muislamu wa india.
ndio maana hata hapa Tanzania waislamu wa asilo tofauti huwa hawachangamani sana kwasababu wana tofauti kubwa za kitanaduni na kimtazamo wa dunia na dini pia