Most famously, in the Democratic Republic of Congo, Kabarebe led the war that ousted Mobutu Sese Seko and installed Laurent Kabila in 1997.
James Kabarebe na siasa za DR Congo
TOKA MAKTABA :
James Kaberebe alivyotimuliwa kutoka kuwa kamanda wa majeshi ya Congo chini ya utawala wa Mzee Laurent Kabila na kurudishwa Rwanda ambapo aliteuliwa kuwa mkuu wa Majeshi ya Rwanda,
View: https://m.youtube.com/watch?v=ZJS6iCSk_NI
Marais wa Angola, rais Zimbabwe ya Robert Mugabe, rais Fidel Castro wa Cuba, Yasser Arafat kiongozi wa PLO ya Palestina walitia timu na kufika Kinshasa kumuunga mkono Laurent Kabila huku Rwanda na Uganda kumpinga Laurent Kabila aliyewafukuza James Kabarebe pamoja na majeshi ya Rwanda na Uganda yaliyokuwa Kinshasa. Pia nchi za Marekani, South Afrika chini ya rais Nelson Mandela , Umoja wa Mataifa na wadau wengine walijitwika jukumu la kumkingia kifua Laurent Kabila ..
Uganda na Rwanda zikaamua kumega mapande kinyemela ya Mashariki ya Congo na kujiwekea vikosi humo kwa madai ya kiusalama dhidi ya majeshi ya waasi ya FDLR ya Rwanda na lile la ADF waasi dhidi ya Uganda,...
Mgogoro huu ukapachikwa jina Vita Kuu ya Dunia ya Afrika kutokana na kuhusika kwa majeshi zaidi ya sita ya kiafrika, Cuba, Mamluki , majeshi ya Umoja wa mataifa, mgambo(wazalendo) ...
Tukiruka hadi sasa 2025 kipindi tulichonacho vita ya Mashariki ya Kongo majimbo ya Mashariki ya Kongo tayari yameangukia na kudhibitiwa na majeshi ya waasi huku Uganda na Rwanda wakilaumiwa kuwepo Bunia Ituri, Kivu ya Kaskazini Goma, Kivu ya Kusini Bukavu na waasi wakuipa kwenda hadi Kinshasa ...ni marudio ya Urithi wa Siasa za Kanda za Maziwa Makuu ...