Waasi wa M23 watamani kufika Kinishasa, Je ipi nafasi ya Tanzania kuinusuru DRC Congo isihanguke

Waasi wa M23 watamani kufika Kinishasa, Je ipi nafasi ya Tanzania kuinusuru DRC Congo isihanguke

Waasi wa 23 wanasema lengo lao ni kufika Kinshasa na kuiangusha serikali ya Tshisheked, je wataweza.

JE IPI nafasi ya Tanzania km nchi yenye nguvu ya kijeshi afrika mashariki na rafiki wa kiuchumi na Congo.
Wajinusuru wenyewe

Taifa tajiri sana duniani wanapigana Halafu sisi masikini ambao kutwa kucha tunalalamika Hali ngumu tutumie pesa kidogo tulizonazo kwenda nje ya mipaka?
 
Tanzania haiusiki na maswala ya ndani ya Kongo. Kongo ni nchi kubwa inapaswa kuwa na uwezo kuweza kuwadhibiti hao M23. Angalia ukibwa wa DRC na angalia hao M23 kieneo wanachopigania ni Goma na Kivu, iweje hao M23 wachache waweze kuwakimbiza wananchi wengi na nchi kubwa kama DRC?

Hivi hao wananchi wa DRC hata kwa marungu na mapanga wakiamua wanawasgindwa hao M23? Yani sielewi hata nini kinaendelea kwenye nchi hiyo mpaka wanasaidia na nchi jirani?

Na sielewi hizo nchi jirani zinalinda nini hahuko hadi hao M23 wanaweza kuchomoza vichwa na kukimbiza watu mkoa mzima?
 
Hao M23 si waiteke kivu yote tu then wajiwekee mipaka wailinde huku wakipambana kuwa Taifa kamili...kinshasa wanaenda kufanya nini?Hawatodumu huko kinshasa.
 
Endapo watanzania tutaruhusiwa kuwapiga hao M23 basi tuzingatie maslahi yetu.
If you have the ability to do something do not do it for free.
 
Tanzania haiusiki na maswala ya ndani ya Kongo. Kongo ni nchi kubwa inapaswa kuwa na uwezo kuweza kuwadhibiti hao M23. Angalia ukibwa wa DRC na angalia hao M23 kieneo wanachopigania ni Goma na Kivu, iweje hao M23 wachache waweze kuwakimbiza wananchi wengi na nchi kubwa kama DRC?

Hivi hao wananchi wa DRC hata kwa marungu na mapanga wakiamua wanawasgindwa hao M23? Yani sielewi hata nini kinaendelea kwenye nchi hiyo mpaka wanasaidia na nchi jirani?

Na sielewi hizo nchi jirani zinalinda nini hahuko hadi hao M23 wanaweza kuchomoza vichwa na kukimbiza watu mkoa mzima?
Vita ya kongo mashariki ni complicated sana na ziko nadharia na mitizamo tofauti tofauti, wapo wanao angalia kupitia miwani ya kihistoria kuanzia mkutano wa Berlin 1884, mipaka iligawanywa bila kujali makabila hivyo watusi wa Kivu wako pia Rwanda ila wanabaguliwa na serikali ya kongo na kulazimishwa warudi Rwanda bila kujali kuwa ni wakongo kitaifa na kiuraia.Hapa tatizo ni serikali ya Felix Tshiksedi. Hivyo watusi chini ys M23 wanadai kujilinda na maisha yao. Pili sababu za kiuchumi eneo hili ni tajiri kwa madini muhimu duniani hivyo serikali.ya kongo inalitaka sana kuliuza kwa makampuni ya nje yachimbe kwa uhuru kwa kuwaondoa watusi wa eneo hilo, mataifa makubwa nayo yanachochea vita vya wenyewe ili iwe rahisi kujichotea madini kwa urahisi.Tatu nchi majirani kama Rwanda na Uganda yananufaika na uporaji wa madini hayo hivyo kutoa support kwa M23 ikbidi washinde vita na kuiondoa serikali iliyoko madarakani au kujitenga na kuanzisha nchi yao ambayo hatimaye iangukie kwenye himaya ya nchi hizi, tatu inasadikiwa upo mkataba wa Lomera uliosainiwa kati ya DRC enzi za Kabila kumega kipande hicho cha mashariki kwa Rwanda na Uganda kwa kusaidia kumwondoa madarakani Mobutu, hilo lilifanyika lakini Kabila aliwageuka na kuwaondoa Banyamulenge kwenye serikali yake na hapo Uganda na Rwanda wakasala na ndipo wakaanzisha movement ya kuunga mkono M23 inayosumbua hadi leo. Sababu ziko nyingi mchanganyiko.
 
Juzi nimeona kwenye Official page ya Facebook ya JWTZ, wakisema Wanaenda Congo kuokoa Raia na Mali zao....!
 
Watanzania mnapenda sana kuingilia mambo ya ndani ya taifa lingine,ambayo kimsingi hayawahusu.Hivi hamkujifunza kitu kwenye mgogoro wa Biafra kule Nigeria na aibu aliyopata Mwl Nyerere?

Mgogoro wa Congo unapaswa kupata suluhu kwa njia ya mazungumzo sio bunduki.
 
Well said

Tuachane na mambo ya watu
 
Back
Top Bottom