Kwa hiyo kwa ufupi hawa M23 wao wanataka kuipindua serikali au wanataka kujitenga kwenye hicho kieneo kidogo chenye madini muhimu?Vita ya kongo mashariki ni complicated sana na ziko nadharia na mitizamo tofauti tofauti, wapo wanao angalia kupitia miwani ya kihistoria kuanzia mkutano wa Berlin 1884, mipaka iligawanywa bila kujali makabila hivyo watusi wa Kivu wako pia Rwanda ila wanabaguliwa na serikali ya kongo na kulazimishwa warudi Rwanda bila kujali kuwa ni wakongo kitaifa na kiuraia.Hapa tatizo ni serikali ya Felix Tshiksedi. Hivyo watusi chini ys M23 wanadai kujilinda na maisha yao. Pili sababu za kiuchumi eneo hili ni tajiri kwa madini muhimu duniani hivyo serikali.ya kongo inalitaka sana kuliuza kwa makampuni ya nje yachimbe kwa uhuru kwa kuwaondoa watusi wa eneo hilo, mataifa makubwa nayo yanachochea vita vya wenyewe ili iwe rahisi kujichotea madini kwa urahisi.Tatu nchi majirani kama Rwanda na Uganda yananufaika na uporaji wa madini hayo hivyo kutoa support kwa M23 ikbidi washinde vita na kuiondoa serikali iliyoko madarakani au kujitenga na kuanzisha nchi yao ambayo hatimaye iangukie kwenye himaya ya nchi hizi, tatu inasadikiwa upo mkataba wa Lomera uliosainiwa kati ya DRC enzi za Kabila kumega kipande hicho cha mashariki kwa Rwanda na Uganda kwa kusaidia kumwondoa madarakani Mobutu, hilo lilifanyika lakini Kabila aliwageuka na kuwaondoa Banyamulenge kwenye serikali yake na hapo Uganda na Rwanda wakasala na ndipo wakaanzisha movement ya kuunga mkono M23 inayosumbua hadi leo. Sababu ziko nyingi mchanganyiko.
Na ikiwa watajitenga wataweza kujitenga, maana kuipindua serikali inaweza kuwa ngumu kwao licha ya wao kuwa wamesala sana, unadhani wanaweza kuwa kama South Sudan? na Je mipaka yao itaishia wapi ni hiyo Goma na kivu tu au watatafuata eneo jingine kwa njia hiyo hiyo ya vita?
Mi nadhani hata kama watafuata mipaka ya lini, hao hawatakubali kuondoka kwenda Rwanda, ingawa Rwanda inawapa support kivita, lakini wao hawawezi kukubali kuporwa ardhi na wakakubali kuiacha na kwenda kuishi Rwanda. Na ikitokea itakuwa kama Israel na palestina, watapigana milele.
Lakini kitu kisicho niingia akilini, inawezekanaje hao M23 waweze kuisumbua Nchi kama DRC?
Maana ukiangalia kwenye ramani kieneo wanacho ishi na kupigania ni hasa Kivu ,na Goma, wao ni wangapi kwa idadi na wana ujuzi kiasi gani na silaha wanazipata wapi kwa njia gani, wanalipiaje, na Je logistically, hao M23 wanawezaje kuwa na nguvu kuliko Jeshi la nchi nzima ya DRC?
Tizama DRC inasaidiwa na South Africa, Kenya,Tanzania, na Malawi.
Na bado M23 wanaweza kupigana hadi kuifanya DRC inapiga mayowe dunia nzima, inakuwaje hapo?