Waasi wa Tigray wapuuza usitishaji wa vita wa Ethiopia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Viongozi TPLF katika jimbo la Tigray wamepuuza tangazo la kusitisha vita lililotolewa na serikali kuu mjini Addis Ababa jana, na wameapa kuendeleza mapambano hadi pale watakawafurusha kikamilifu wanajeshi wa Ethiopia.

Äthiopien I Konfliktregion Tigray
Wanajeshi wa Ethiopia wakipiga doria katika mji wa Mekele (07.03.2021)

Tangazo hilo la TPLF la kukaidi hatua ya serikali ya kusitisha mapigano limekuja usiku wa kuamkia leo, muda mfupi baada ya wapiganaji wa chama hicho kusema wamechukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele. Kabla ya hapo, serikali ya shirikisho la Ethiopia inayoongozwa na waziri mkuu Abiy Ahmed ilikuwa imechukuwa maamuzi ya upande mmoja ya kusitisha mapigano.

Katika tangazo hilo la TPLF, chama hicho ambacho kinachukuliwa na serikali kuu kama cha uasi kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha ukombozi na usalama wa watu wa jimbo la Tigray. Getachew Reda, msemaji wa chama hicho, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa lengo la adui wanayepigana naye ni kulibana jimbo la Tigray na kuhakikisha kuwa watu wake wanasalimu amri, na kuapa kuwa hilo halitowezekana.

Äthiopien l Premierminister Ahmed Abiy
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed

Hamasa miongoni mwa wapiganaji wa TPLF
Katika mazingira hayo ya mafanikio, mmoja wa wapiganaji wa tawi la kijeshi la TPLF, Teheras Tsega Berhan amesema wapiganaji wao wana ari kubwa ya mapambano.

''Vijana wamejawa na hamasa na wanamiminika katika vituo vya mafunzo, kujiunga na mapambano. Adui yetu anazidi kudhoofika, na anashindwa,'' amesema Berhan.

Vita vya Tigray vimekuwa vikiendelea kwa karibu miezi minane, na kwa muda mrefu wapiganaji wa TPLF na viongozi wao walikuwa wanajichimbia vichakani bila kupiga hatua yoyote kubwa.

Lakini wiki iliyopita walianzisha mashambulizi makali wakati serikali ya Addis Ababa ikifanya uchaguzi katika majimbo mengine isipokuwa Tigray.

Äthiopien I Konfliktregion Tigray
Vita vya jimboni Tigray vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu​

Addis Ababa yasisitiza 'inapambana na wahalifu'
Matokeo ya uchaguzi huo bado hayajatangazwa lakini yanatarajiwa kumpa ushindi waziri mkuu Abiy na vyama vinavyomuunga mkono.
Msemaji wa TPLF anadai kuwa kabla ya muda mrefu watakuwa wamemaliza kazi ya kulifurusha jeshi la Ethiopia kutoka jimboni mwao, ili wakaazi wa jimbo hilo waweze kufanya kazi zao kama kawaida.

Serikali kuu ya mjini Addis Ababa haijatoa tamko kuhusu taarifa ya TPLF kuukamata mji wa Makele, na msemaji wake Dina Mufti hata anakanusha kuwepo kwa vita, akisema kinachoendelea ni kupambana na wahalifu.

''Hatusemi kuna vita, tunasema kuna operesheni ya kuhakikisha sheria inaheshimiwa. Mtu anapokiuka sheria ya nchi lazima awajibishwe.''

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amezungumza na pande mbili katika vita hivyo, na kuzikumbusha kuwa hali iliyopo ni ushahidi mwingine kuwa mizozo haisuluhishwi kwa mtutu wa bunduki.

DW Swahili
 
Mpaka kieleweke haiwezekani unaepambana nae ajifanye yey ndio msimamiz wa pambano
 
Waafrika bana shida inayotumaliza ni udini na ukabila. Hao watigray walikula mema ya nchi saivi wakawekwa kando wao wanaona Kama hawajatendewa haki.ila muda wanakula mema ya nchi kwa kigezo kuwa wao wajanja Mara wamesoma huku wakicheza ngoma sijui wao walipenda maendeleo na huku ni kujipendelea kwa viongozi wao kujipelekea maendeleo huku wakididimiza pengine.saivi wanashindwa kuvumilia kuona wengine wakila Kama wao walivyokuwa wakila.
 
Sasa eti wanaidai wameishinda serikali,hivi inakuaje waasi wanaishinda nchi nguvu?

Ethiopia hii ndo inaweza kupigana na Egypt kweli?

Screenshot_20210629-210315.png

Screenshot_20210629-210340.png
 
Hawa watu ni jeuri sana, kwa sasa wamesema wanajiandaa kuishambulia Eritrea. Ila nilijiuliza ni kwa nini Serikali ya Addis Ababa iliungana na Eritrea kupambana na hawa watu sijapata majibu.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Kwamba hako kajimbo 1 ndio nchi 2 zinashindwa kufanya oparesheni kuwafyeka hao wanamgambo wote?

Kweli hizo nchi ziko broke
 
Waafrika bana shida inayotumaliza ni udini na ukabila. Hao watigray walikula mema ya nchi saivi wakawekwa kando wao wanaona Kama hawajatendewa haki.ila muda wanakula mema ya nchi kwa kigezo kuwa wao wajanja Mara wamesoma huku wakicheza ngoma sijui wao walipenda maendeleo na huku ni kujipendelea kwa viongozi wao kujipelekea maendeleo huku wakididimiza pengine.saivi wanashindwa kuvumilia kuona wengine wakila Kama wao walivyokuwa wakila.
Kama unasimanga kabila fulani hiviTanzania
 
Mkuu fuatilia huo mzozo wa Tigray.afrika matatizo yetu yanafanana mkuu.
Huo no mtizamo wako kumbuka pia mind huwa inaona like ulichopanga kukiona.
Kwani Unajua yale mauaji ya Rwanda I e genocide source yake ukweli.
Unajua Nigeria kinachotokea ni Nini. Yaani afrika is the same so hata nikiongea ukaona kuwa nasimanga kabila fulani tz ni kuwa lazima uone ivyo Mana uko tz na unaijua vyema.
Don't bias your mind to understand things
 
Pole Boss. Nawaza Sera ya Majimbo Ya CHADEMA. Ingetawala Tanzania, Sasa hivi tungekuwa na majeshi ya Majimbo.

Huko Nigeria pia majimbo yanatafunana.
 
Yaani afrika kinachotumaliza ni ukabila na udini hebu imagine na mkoloni alitumia silaha iyo iyo kutumaliza mkuu.
Labda Sera ya majimbo ufanikiwe yaani kila kitu kiishie huko huko kwenu jimboni Ila Sasa hela serikali zitatoka wapi.tukipata mikopo jamaa anakimbiza jimboni mwake kufanya maendeleo haohao wanaanza kutukuna majimbo mengine kuwa ni wazembe walichunga na kucheza ngoma ndo Mana hawana maendeleo na huku yule mtu aliyepo huko central kabisa akapeleka kujenga shule, hospital,umeme,maji, roads huko kwao na majimbo mengine hayana kitu kabisa.
Hebu imagine unakuta wote labda ni kabila moja ,Ila wewe chifu unashirikiana na labda mjerumani kumpiga mwenzako chifu wa kabila lako.
Mkimmaliza huyo mjerumani kukumaliza wewe inakuwa ni easy anakutawala. Ndo tulivyotawaliwa mkuu.
Yaani nikiwa kiongozi kitu Cha kwanza ku discourage ni dini ama udini na ukabila.
Yaani mtwara atasomea Arusha na ku discourage watu wa kabila moja kuoana kabisa.yaani ni udikteta kabisa kwa Mambo hayo.
Hata Argentina walimaliza kabisa tatizo la blacks nchini mwao kwa kuwaua ama through intermarriage
 
Pole Boss. Nawaza Sera ya Majimbo Ya CHADEMA. Ingetawala Tanzania, Sasa hivi tungekuwa na majeshi ya Majimbo.

Huko Nigeria pia majimbo yanatafunana.
Unakosea ... sera ya majimbo ni kama tu TAMISEMI kwamba halmashauri zijisimamie zenyewe with limited influence ya Chamwino.

Masuala ya ulinzi ni chini ya serikali kuu n.k ila kuna mamlaka na mapato kadhaa yanaamuliwa kwa ngazi ya jimbo. Hta sasa devolution ipo ila sio kwa level ya jimbo.

Ningeshauri usome kitabu kipya cha Lissu kimechambua vzuri hii sera na kutumia katiba ya Kenya kipindi cha Uhuru.
 
Haha. Ideally. Lakini practical imeleta vurungu sehemu nyingi Africa. Huwezi kuwa na autonomy goverment Africa utegemee utulivu. Jimbo lazima litakua na ukabila pia. Huwezi tenganisha Jimbo la Ziwa na Usukuma mathalani.

Jimbo linaweza kuja na bylaw mfano Ethiopia Oromia in by law Kila kampuni ndani ya Oromia lazima iajiri 80% ya wanyakazi. Kiza zaa Kiko Adis Ababa. Pale ni Oromia ila katika jiji Hilo wa Oromo ni 20% Sasa Wanataka wafanyakazi wote katika jiji Wawe wa Oromo by 80% . Hope umenielewa.
 
Back
Top Bottom