19 February 2025
New York
Balozi wa Kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa alaani serikali ya DR Congo kwa 'kutumia njia ya kijeshi' katika mzozo wa ndani ya nchi hiyo
View: https://m.youtube.com/watch?v=Urb9VHRkxQ0
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu DR Congo Februari 19, 2025, Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa Ernest Rwamucyo alisema .. mazungumzo ni njia sahihi siyo njia za kijeshi
Balozi Ernest Rwamucyo ameongeza kuwa njia sahihi ni kwa wadau wote walio katika mzozo wa Congo wakae katika meza ya mazungumzo ikiwemo makundi yote wakiwemo M23 ili kupata suluhisho la mgogoro huo wa ndani ya nchi ya Congo kama ambavyo mkutano wa Dar es Salaam wa tarehe 8 February 2025 wa viongozi wa nchi za EAC na SADC Juu ya Mzozo wa Congo ulivyopendekeza..
Rwanda pia imemtaka rais wa DR Congo kuacha mtindo wake wa kukacha mikutano muhimu kama ile ya kikanda ya Dar es Salaam na Addis Ababa juu ya mzozo wa DR Congo. Hivyo kutokuwapo kwa rais wa Congo katika mokutano hiyo Felix Tshisekedi anahujumu na ameua nafasi nzuri ya kutatua mzozo huo kikanda.
Utawala wa Kinshasa umeamua kugawa ovyo silaha kwa silaha kwa vijana na watoto kuchochea zaidi vita vya ndani ya nchi ya Congo, na tunaona hali hiyo imetumiwa kusambaza taarifa potofu za watoto kuuawa wakati ni jeshi la serikali la FARDC kugawa silaha kwa vikundi vya mgambo kwa jina la wazalendo na watoto ambao hawajapitia mafunzo rasmi ya kijeshi wala kuongozwa na mfumo rasmi wa kijeshi umekoleza moto mauaji ya kikabila na matumizi yasiyo sahihi ya silaha zilizozaga ovyo kwa makusudi
Rwanda pia imeshambuliwa na majeshi ya kigeni yaliyopo ndani ya DR Congo na kuua raia 16 wa Rwanda pia mali zao kuharibiwa. Hili jambo linahitaji kulaaniwa na Jumuiya ya Kimataifa
Kuwepo kwa mamluki, askari wa kukodiwa, MONUSCO, SAMIDRC, Majeshi ya Mamluki ya Nje kumefanya eneo hili la Mashariki ya Congo kukosa utulivu kutokana na mchanganyiko wa majeshi haya ya kila aina. Hali hii imekuwa tishio kwa nchi ya Rwanda