Waasisi wa CCM

Waasisi wa CCM

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Watu watano muhimu sana katika historia ya uasisi wa CCM ni hawa:
1: Mwalimu Julius K. Nyerere
2: Sheikh Aboud Jumbe
3: Sheikh Rashid M. Kawawa
4: Sheikh Thabit Kombo
5: Mhe. Pius Msekwa

Inabidi CCM iwe na utaratibu wa kuwaenzi watu hawa kama waasisi wa taasisis yao.
 
Kulikuwa na Kamati ya watu 20 ya kuandaa Katiba ya CCM.

Wajumbe 10 toka ASP:

1. Sheikh Thabit Kombo.---[Mwenyekiti wa Tume]
2. Ali Mzee.
3.Abdalah Natepe.
4.Seif Bakari.
5.Hamis Hemed.
6.Rajab Kheri.
7.Asia Amour.
8.Hassan Nassor Moyo.
9.Juma Salum.
10.Hamdan Muhiddin.

Wajumbe 10 toka TANU:
1.Peter Abdalah Kisumo.
2.Pius Msekwa.---[Katibu wa Tume]
3.Daudi Mwakawago.
4.Kingunge Ngombale Mwiru.
5.Jackson Kaaya.
6.Peter Siyovelwa.
7.Nicodemus Banduka.
6.Lawi Nangwanda Sijaona.
7.Beatrice Mhango.
8.Basheikh Mikidadi.

Source: www.ccmmusoma.blogspot.com
 
Ni kweli; mchakato wa uanzishwaji wa CCM ulihusisha watu wengi sana, lakini watano muhimu ambao ndiyo nguzo ya mfumo wa CCM tulio naoa leo ni hao watano. Mtu ambaye hapewi credit kubwa ndani ya CCM ni Jumbe, kwani ndiye aliyeweka msukumo sana wa kuwa na chama kimoja pamoja na serikali moja wakati akiwa makamo wa Rais na alikuwa akimwakilisha Nyerere katika majukumu mbalimbali ndani na nje ya nchi kama rais mtarajiwa. Miaka mitano baadaye akashindwana na mfumo kutokana na umaarufu aliojizolea Sokoine na mambo yakawa kama yalivyo leo. Kusingekuwa na Sokoine huenda leo tungekuwa na nchi ya tofauti sana
 
..naelewa nafasi ya Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

..kwanini unadhani Kawawa, Msekwa, na Thabit Kombo, walikuwa muhimu pia?
 
Watu watano muhimu sana katika historia ya uasisi wa CCM ni hawa:
1: Mwalimu Julius K. Nyerere
2: Sheikh Aboud Jumbe
3: Sheikh Rashid M. Kawawa
4: Sheikh Thabit Kombo
5: Mhe. Pius Msekwa

Inabidi CCM iwe na utaratibu wa kuwaenzi watu hawa kama waasisi wa taasisis yao.
Kwanini waasisi wa Tanu sio waasisi wa CCM?
Au CCM inajiita chama Cha Mapinduzi kwa kuwa kimewapindua wazee wa Kariakoo na Mzizima ?
 
..naelewa nafasi ya Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

..kwanini unadhani Kawawa, Msekwa, na Thabit Kombo, walikuwa muhimu pia?
Nasikia Kawawa ndio alikuwa msuka mipango mahiri, hasa mzee akitaka kula totoz < 18
 
..hizo ni siasa chafu baina ya wana-ccm.

..nyerere alilia machozi wakati akielezea jinsi kawawa alivyobebeshwa lawama ambazo alistahili yeye nyerere, au chama na serikali kwa ujumla.
 
..naelewa nafasi ya Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

..kwanini unadhani Kawawa, Msekwa, na Thabit Kombo, walikuwa muhimu pia?
Mkuu nadhani viongozi walioasisi TANU ndio wa kuenziwa, hawa wa CCM ni ''amalgamation''.

Kiongozi kama Msekwa anaenziwa kwa lipi? Huyu ametuachia mfumo hovyo sana wa Bunge.
Ni yeye aliandika miongozo mingi ya kulifanya Bunge lisiwe na meno na kuwa rubber stamp kama ilivyo leo.

Kosa kubwa tunalofanya ni kuangalia wanasiasa.
Siku za nyuma tulikuwa na sherehe za Mashujaa ambazo kwa hakika zilibeba maana yake halisi.

Tarehe ikaondolewa Sept 1, siku hizi hata kuwakumbuka waliojitoa kwa nchi hii kama wale waliolala Bunazi hakuna! Hatuwaenzi akina Kanal Kashmir, akina Walden, Mayunga, n.k.

Lazima kwanza tuwatambue wale walio ' pay the ultimate price''
 
..kweli kabisa.

..Watz hatuitendei haki sikukuu ya mashujaa.
 
Kuhusu siku ya mashujaa wewe unazungumzia mambo ta kitaifa, mimi nazuingumza CCM kama taasisi ya kisiasa kama ilivyo CHADEMA, UDP na vyama vingine. CCM inatokana na muungano wa TANU na ASP(ingawa hukuitaja); CCM isingekuwapeo kama vyama hivyo visingekubali kuuangana. Hao watu watano niolowataja ndio nguzo kubwa sana iliyofanikisha muungano wa vyama hivyo, na hivyo kuzaliwa CCM.

Iwapo Msekwa kama spika alivuruga, bado haimondolei credit kuwa wakati akiwa Katibu Mtendaji wa TANU alifanikisha muungano wa TANU na ASP na hivyo kuzaliwa kwa CCM. Hata hivyo utendaji wa Msekwa kama spika pia sikubaliani nawe kwa kiasis fulani, kwani Msekwa alikuwa ndiye spika wa kwanza kuongoza bunge lenye wabunge wa upinzani na aliwa-accomodate sana mpaka kukubali kiapo cha ubunge pia kibadilishwe.

Mwisho ni kwamba historia hujengwa na watu; wawe wanasiasa, askari au wanasayansi na kadhalika. Unaweza usimkubali mtu lakini akawa ni nguzo ya historia isiyoweza kubadilika. Mpaka leo sote tunajua kuwa aliyeanzisha vita ya pili ya dunia ni Hitller hata kama hatukubalini kabisa na itikadi yake lakini hatuwezi kubadilisha ukweli huo.
 
Kuhusu siku ya mashujaa wewe unazungumzia mambo ta kitaifa, mimi nazuingumza CCM kama taasisi ya kisiasa kama ilivyo CHADEMA, UDP na vyama vingine. CCM inatokana na muungano wa TANU na ASP(ingawa hukuitaja) CCM isingekuwapeo kama vyama hivyo visingekubali kuuangana. Hao watu watano niolowataja ndio nguzo kubwa sana iliy;ofanikisha muungano wa vyama hivyo, na hivyo kuzaliwa CCM.

Iwapo Msekwa kama spika alivuruga, bado haimondolei credit kuwa wakati akiwa Katibu mtendaji wa CCM alifanikisha muungano wa TANU na ASP na hivyo kuzaliwa kwa CCM. Hata hivyo utendaji wa Msekwa kama spika pia sikubaliani nawe kwa kiasis fulani, kwani Msekwa alikuwa ndiye spika wa kwanza kuongoza bunge lenye wabunge wa upinzani na aliwa-accomodate sana mpaka kukubali kiapo cha ubunge pia kibadilishwe.

Mwisho ni kwamba historia hujengwa na watu; wawe wanasiasa, askari au wanasayansi na kadhalika. Unaweza usimkubali mtu lakini akawa ni nguzo ya historia isiyoweza kubadilika. Mpaka leo sote tunajua kuwa aliyeanzisha vita ya pili ya dunia ni Hitller hata kama hatukubalini kabisa na itikadi yake lakini hatuwezi kubadilisha ukweli huo.

1. Mkuu nimetaja neno ''amalgamation' ya CCM nikijua msomaji ataelewa ni kutokana na TANU na ASP

2. Nikamzungumzia Msekwa kwa maana kwamba katika mfumo wa chama kimoja watu hawapewi heshima kwa michango yao,nikawataja akina Walden , Kashmir n.k. kwasababu hao walikuwa ni watumishi nje ya CCM

3. Nikaeleza kuhusu Msekwa na hili nalisema tena, ni mmoja wa watu waliotuachia mfumo mbaya , mbovu na usio na heshima wa Bunge. Kipindi cha Msekwa Bunge lilikuwa rubber stamp tu na ndilo limetuzalia haya mambo ya ndiyooo bila hata kusoma nyaraka.

Spika aliyerudisha hadhi na heshima ya Bunge ni hayati Sitta kiasi wananchi walikiamini chombo hicho kabla ya kuangukia kwa wanafunzi wa Msekwa akina Makainda walioturudisha enzi za Msekwa na kupokelewa na akina Ndugai.

Hao hawapaswi kulaumiwa, mtu aliyeharibu Bunge ni Pius Msekwa na hili atabaki nalo na kwenda nalo.

Ndiyo maana pamoja na kuongoza Bunge kwa muda mrefu bado heshima yake katika jamii inachuja sana ukilinganisha na wenzake kama kina Butiku, Warioba, Salim, Msuya n.k.

Ni kwa mantiki hiyo ya kisiasa nikasema kuwa hakuna sababu za kuenziwa hata na vyama vyao, ubovu waliousababisha CCM ikiwa chama umetugharimu sote hata tusioendekeza vyama.

Nikasema muhimu tuwakumbuke watu waliojitoa 'pay the ultimate price'' .
Mbona tumesusa sherehe za mashujaa, halafu tunawatafuta huko CCM tena akina Pius!
 
Ghafla chama kiko mikononi kwa mwamba,mbabe wa vita,simba wa yuda ,malaika mkuu,jiwe doctor
 
Hoja zako zote, hata kama kweli uko sahihi, hazina uhusiano kabisa na uasisi wa CCM! I am sorry!
 
..naelewa nafasi ya Mwalimu Nyerere, na Mwalimu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

..kwanini unadhani Kawawa, Msekwa, na Thabit Kombo, walikuwa muhimu pia?
Mtu wa muhimu sana (TOP) katika uundwaji wa CCM alikuwa ni Jumbe. Nyerere, Kombo na Kawawa umuhimu wao unatokana na influence waliyokuwa nayo kwenye jamii katika kukubali au kukataa uunganishaji wa vyama vya TANU na ASP. Umuhimu wa msekwa unakuja kwa vile yeye kama katibu mtendaji wa TANU wakati huo ndiye aliye ratibu utaratibu mzima wa uunganishaji wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba ya chama, nembo ya chama na design ya bendera ya chama.
 
Ghafla chama kiko mikononi kwa mwamba,mbabe wa vita,simba wa yuda ,malaika mkuu,jiwe doctor
Chuki zenu kwa JPM haziwezi kufanikiwa hata mfanye nini kwa sababu sio Watanzania peke yao wanaotambua mambo makubwa anayofanya. Ulimwengu mzima unatambua kwamba JPM ni no nonsense president. Kipindi cha miaka mitano tu Tanzania ina-finance miradi mikubwa ambayo hapo awali walikuwa wanakinga bakuli. Hata uchaguzi wetu tu tulikuwa tunakinga bakuli.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mapato ya Serikali wakati wa JMK tulikuwa tupo taabai lakini alipokuja JPM just to mention a few; Mapato Bandari kwa siku billion 5 na ushee, Madini mapato yameongezeka mara dufu na yanaendelea kupaa. Watanzania tuache unafiki hakuna mtu ambaye hana kasoro lakini JPM kwa miradi ya kimkakati pamoja na Hospitali zilizojengwa zinatufanya Watanzania kufikiria vizuri zaidi nini tunahitaji ili tuweze kufika kwenye maendeleo na sio kuwa kichekesho kwa kizazi kijacho.

BTW out of topic for various reasons.
 
Mtu wa muhimu sana (TOP) katika uundwaji wa CCM alikuwa ni Jumbe. Nyerere, Kombo na Kawawa umuhimu wao unatokana na influence waliyokuwa nayo kwenye jamii katika kukubali au kukataa uunganishaji wa vyama vya TANU na ASP. Umuhimu wa msekwa unakuja kwa vile yeye kama katibu mtendaji wa TANU wakati huo ndiye aliye ratibu utaratibu mzima wa uunganishaji wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba ya chama, nembo ya chama na design ya bendera ya chama.
Spot on Kichuguu. Jumbe alikuwa na makando kando yake na alikuwa hafahamu kwamba Seif Sharrif alikuwa ni adui yake wakati ule kwa sababu kama sikosei ndiye aliyevujisha mipango yake.
 
Chuki zenu kwa JPM haziwezi kufanikiwa hata mfanye nini kwa sababu sio Watanzania peke yao wanaotambua mambo makubwa anayofanya. Ulimwengu mzima unatambua kwamba JPM ni no nonsense president. Kipindi cha miaka mitano tu Tanzania ina-finance miradi mikubwa ambayo hapo awali walikuwa wanakinga bakuli. Hata uchaguzi wetu tu tulikuwa tunakinga bakuli.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mapato ya Serikali wakati wa JMK tulikuwa tupo taabai lakini alipokuja JPM just to mention a few; Mapato Bandari kwa siku billion 5 na ushee, Madini mapato yameongezeka mara dufu na yanaendelea kupaa. Watanzania tuache unafiki hakuna mtu ambaye hana kasoro lakini JPM kwa miradi ya kimkakati pamoja na Hospitali zilizojengwa zinatufanya Watanzania kufikiria vizuri zaidi nini tunahitaji ili tuweze kufika kwenye maendeleo na sio kuwa kichekesho kwa kizazi kijacho.

BTW out of topic for various reasons.
We umefanya kipi cha maana kipindi hiki toka huko
 
Spot on Kichuguu. Jumbe alikuwa na makando kando yake na alikuwa hafahamu kwamba Seif Sharrif alikuwa ni adui yake wakati ule kwa sababu kama sikosei ndiye aliyevujisha mipango yake.
CCM hawampi credit ya kutosha Jumbe lakini ndiye aliyekuwa mtu wa mmuhumu sana nambari moja katika uundwaji wa CCM. Hamad alikuwa mtu mwenye tamaa ya madaraka siku zote za maisha yake na matokeo yake yalikuwa ni kuwafarakanisha Jumbe na Nyerere akitegemea kuwa ndiye angeweza kujaza nafasi ya Jumbe.!!
 
Back
Top Bottom