Kuhusu siku ya mashujaa wewe unazungumzia mambo ta kitaifa, mimi nazuingumza CCM kama taasisi ya kisiasa kama ilivyo CHADEMA, UDP na vyama vingine. CCM inatokana na muungano wa TANU na ASP(ingawa hukuitaja) CCM isingekuwapeo kama vyama hivyo visingekubali kuuangana. Hao watu watano niolowataja ndio nguzo kubwa sana iliy;ofanikisha muungano wa vyama hivyo, na hivyo kuzaliwa CCM.
Iwapo Msekwa kama spika alivuruga, bado haimondolei credit kuwa wakati akiwa Katibu mtendaji wa CCM alifanikisha muungano wa TANU na ASP na hivyo kuzaliwa kwa CCM. Hata hivyo utendaji wa Msekwa kama spika pia sikubaliani nawe kwa kiasis fulani, kwani Msekwa alikuwa ndiye spika wa kwanza kuongoza bunge lenye wabunge wa upinzani na aliwa-accomodate sana mpaka kukubali kiapo cha ubunge pia kibadilishwe.
Mwisho ni kwamba historia hujengwa na watu; wawe wanasiasa, askari au wanasayansi na kadhalika. Unaweza usimkubali mtu lakini akawa ni nguzo ya historia isiyoweza kubadilika. Mpaka leo sote tunajua kuwa aliyeanzisha vita ya pili ya dunia ni Hitller hata kama hatukubalini kabisa na itikadi yake lakini hatuwezi kubadilisha ukweli huo.
1. Mkuu nimetaja neno ''amalgamation' ya CCM nikijua msomaji ataelewa ni kutokana na TANU na ASP
2. Nikamzungumzia Msekwa kwa maana kwamba katika mfumo wa chama kimoja watu hawapewi heshima kwa michango yao,nikawataja akina Walden , Kashmir n.k. kwasababu hao walikuwa ni watumishi nje ya CCM
3. Nikaeleza kuhusu Msekwa na hili nalisema tena, ni mmoja wa watu waliotuachia mfumo mbaya , mbovu na usio na heshima wa Bunge. Kipindi cha Msekwa Bunge lilikuwa rubber stamp tu na ndilo limetuzalia haya mambo ya ndiyooo bila hata kusoma nyaraka.
Spika aliyerudisha hadhi na heshima ya Bunge ni hayati Sitta kiasi wananchi walikiamini chombo hicho kabla ya kuangukia kwa wanafunzi wa Msekwa akina Makainda walioturudisha enzi za Msekwa na kupokelewa na akina Ndugai.
Hao hawapaswi kulaumiwa, mtu aliyeharibu Bunge ni Pius Msekwa na hili atabaki nalo na kwenda nalo.
Ndiyo maana pamoja na kuongoza Bunge kwa muda mrefu bado heshima yake katika jamii inachuja sana ukilinganisha na wenzake kama kina Butiku, Warioba, Salim, Msuya n.k.
Ni kwa mantiki hiyo ya kisiasa nikasema kuwa hakuna sababu za kuenziwa hata na vyama vyao, ubovu waliousababisha CCM ikiwa chama umetugharimu sote hata tusioendekeza vyama.
Nikasema muhimu tuwakumbuke watu waliojitoa 'pay the ultimate price'' .
Mbona tumesusa sherehe za mashujaa, halafu tunawatafuta huko CCM tena akina Pius!