Unaousema n ukwel mkuu
Ila wababa tuache kulea watoto kikauzu badala yake tubadirike hasa wakat huu ambao ulimwengu unaenda kasi unalea mtoto kwa mifumo ya miaka 1980 wakat dunia inehama huko
Mtoto anakupigia simu anataka kujua nyumban mnaendeleaje wewe unajibu kifupi na hauoneshi kufurah kuwa mtoto kakupigia
Ila ukimpigia mama anaonesha furaha anakueleza mambo muhimu kuhusu nyumban
Unategemea mtoto atampenda au atampigia Nani simu kila wakat pale anapohtaj kujua Jambo fulani
.....wazazi hasa wakiume tubadilike....
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app
Binafsi naona kuna cases nyingi katika hili.
Binafsi sikulelewa na baba, nimekuwa nikiwa simjui. Nimekuja kufahamiana naye baada ya kuhitimu kidato cha sita. Kwahiyo sina bond yoyote na baba.
Ila nilipokutana naye nilijihisi kusamehe tu ili maisha yaendelee, nikiamini sasa atachukua majukumu yake kama baba kumbe hana hata huo muda.
Hii ni special case kwangu na kwa wengine wenye case kama yangu na wale waliotelekezwa.
Ila pia, mimi ni mtoto wa kiume naona, ukiachana na kina baba makatili kwa watoto, wapo wanajitahidi sana kujali familia zao.
Tatizo huwa linaanzia kwenye kuweka duscipline ya watoto, mara nyingi hapa ndio kina mama huwa wanakaa pembeni ili kukwepa lawama.
1- Mtoto akienda kucheza akachelewa kurudi nyumbani, baba anampa adhabu au sometimes anamwambia hakuna kula. Tena mnakubaliana vizuri na mama yake, kumbe mama yake kaficha chakula huko jikoni anampatia baadaye baba hajui.
Mtoto anakuwa akijua baba ndio mbaya.
2- Mtoto kumwomba baba pesa kidogo labda nauli ya shule, baba akasema hana. Mama anatoa anampa mtoto huku akimlaumu baba.
Katika mazingira ya hivi, ni rahisi kwa mtoto kuwa na bond kubwa sana kwa mama kuliko mama. Na bond hii huwa ni kubwa mpaka kwa ndugu wa mama.
Mara nyingi undugu wa upande wa mama ndio huwa una nguvu sana kuliko upande wa baba.
Mimi nina Anko wangu, hata akiwaomba wanaye elfu 10 lazima wampigie simu mama yao kwanza. Bila ya mama kutoa go-head anaambulia patupu.