changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Timu kupata nafasi ya kuanzia raundi ya pili huwa inatokana na idadi ya wanachama wa CAF watakaoshiriki michuano ya CAF interclub.Round ya pili inategemea rank timu 10 kwenye rank ndio zinaanzia round ya pili. Hivyo kama 4 zitaenda shirikisho Yanga itaingia kwenye timu 10 za kuanzia round ya pili.
Kwenye hatua ya awali, zinatakiwa timu ziwe 64 ili zikichezwa mechi zibakie timu 32 zitakazocheza raundi ya pili, ila kinachotokea ni kwamba wanachama wengine wanaweza kushindwa kushiriki michuano ya CAF kutokana na sababu mbalimbali kama miundombinu, ukosefu wa fedha, n.k na ndio maana ikifikia pazia jipya la michuano CAF hutoa fursa kwa mashirikisho wanachama wa CAF kusajili vilabu vyao vitakavyoshiriki michuano ya CAF ngazi ya vilabu kisha baada ya usajili wanapata kujua ni timu ngapi zitashiriki klabu bingwa na ngapi zitashiriki kombe la shirikisho.
Baada ya kujua, wanaangalia kama zimetia timu 64 au zimepungua au zimezidi. Kama zimepungua timu 64, hapo wanaangalia kuna upungufu wa timu ngapi. Mfano kuna timu 58 ndio zinashiriki hapo kuna pungufu wa timu 6 hivyo hizo timu 6 zitaanzia moja kwa moja hatua ya pili.
Kwahiyo inakuwa 58-6 = 52
Timu 52 zitacheza hatua ya awali na kisha timu 26 zitafuzu na 26 zitatoka. Timu 26 zitakazofuzu zitajumlisha na zile 6 zilizopelekwa raundi ya pili moja kwa moja na kutimiza jumla ya timu 32.
Hivyo nafasi ya kuanzia hatua ya pili haipo guarantee kuwa ni lazima timu 10 bali hutegemea idadi ya timu zinazoshiriki michuano.
Msimu wa 2018/2019
Timu zilikuwa 57 kutoka kwa wanachama 46 hivyo timu 7 pekee ndio zilianzia hatua ya pili
Msimu wa 2019/2020
Timu zilikuwa 61 kutoka kwa wanachama 49 hivyo ni timu 3 pekee ndio zilizopata nafasi ya kufuzu moja kwa moja hatua inayofuata
1) Tp Mazembe
2)Es Tunis
3) Wydad
Hadi Al Ahly mwenyewe huo msimu alianzia hatua ya awali kabisa.