Wababe hawa wa mwaka 2015 watasaidia kupindua meza Oktoba 2020?

Wababe hawa wa mwaka 2015 watasaidia kupindua meza Oktoba 2020?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakisiwa kuwa ndiyo uchaguzi utakaokuwa na changamoto zenye hisia na usio lelemama.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kuna mambo yalifanyika kwenye kutuma na kupokea matokeo ya sehemu flani zilizoonekana kumbeba mgombea mmoja na baadae kura kuyumbishwa na kurekebishwa upya kwenye poll centre ya chama.

Kama namuona Nape, January, Kinana kwa mbaali mzee Edo wakishea strategic experience zile zile walizocheza nazo ili kupindua meza siku chache zijazo hata kama wamekaa meza moja ya chakula na mbabe wa vita.

Hii inaweza kuwa hisia kali ambayo kwa mfumo wa sasa hawawezi kuwa hadharani au kupigiana simu ili "kuyajenga" kufikia hadhima nzito ambayo wanaweza kuiita "ya mustakabali wa Taifa".

Wananchi wapole, wenye hofu, waoga, wapenda raha nk kazi yao ni moja tu, kupiga kura na kurudi nyumbani ila mpango na jukumu la kumpata atakayewaongoza lina watu maalum.
 
Back
Top Bottom