Wababe wa dunia wanaiparamia Afrika, Waafrika wenyewe wanashangilia!!

Wababe wa dunia wanaiparamia Afrika, Waafrika wenyewe wanashangilia!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Ukiangalia kwa undani utaona kuwa mataifa yaliyoendelea kiuchumi na yale yenye uchumi wa Kati, yote kwa pamoja yanapigana vikumbo kuigombania Afrika.

Siyo kama mshirika wa kimaendeleo bali kama soko na chanzo cha malighafi katika kuendeleza chumi zao.

Wakati wababe hao wa Dunia wakipigana vikumbo, waafrika wenyewe wako bize sana kushangilia na kushadadia nani ana ushawishi zaidi Afrika kuliko mwingine.

Muda si mrefu kunaweza kuzuka vita Afrika ya kupigana kundi moja dhidi ya jingine kwa misingi ya kundi lipi linamuunga mkono mbabe gani wa dunia.

Afrika tumelaaniwa!!??
 
Kugombewa hakuepukiki maana rasilimali zipo za kutosha ila tatizo watawala wetu hawatambui vipaumbele vya raia wao au kuweka mbele maslahi ya hili bara wanapokutana na hao waviziaji, ni vigumu mno kufahamu wanazungumza na kukubaliana nini na hao mabeberu.
 
Watawala wetu wamekwama kwenye mtego kwamba kuna wanyonyaji wema na wabaya. Kwa ivo wao kila mara hukubaliana na wanyonyaji wanaowaona kwa wakati huo kwamba ni wanyonyaji wazuri. Swali la kujiuliza jee iko siku na Afrika nao watakuwa ni wababe dhidi ya mabara mengine?
 
Hoja nzuri. Jee ni nani wa kuikomboa Afrika Kifikra?? Na fikra zipi ambao zinaifanya Afrika kuwa tegemezi kwa mabara mengine??
Elimu kwa vijana wa hili bara ndio suluhisho la ukombozi wa kifikra..........naamini kizazi kijacho cha hili bara kitaleta mabadiliko makubwa sana, sidhani kama watakubali kuwa watumwa wa kihistoria na kuendelea kuwa duni.
 
Elimu kwa vijana wa hili bara ndio suluhisho la ukombozi wa kifikra, naamini kizazi kijacho cha hili bara kitaleta mabadiliko makubwa sana, sidhani kama watakubali kuwa watumwa wa kihistoria na kuendelea kuwa duni.
Elimu yetu tulitegemea kuipata toka kwa wasomi wetu, jee vyuo vyetu vina elimu toka kwenye misingi ya uafrika wetu ama tumerithi masomo toka kwa hao hao wababe yasiyofanana na uhalisia wa bara letu?
 
Mmarekani huyu anaesabisha ndugu zetu wa Congo wanakufa huku yeye akijibebea dhahabu, au unamzungumzia mmarekani yule aliefadhili uasi wa jonas savimbi wa unita kule angola na kupeleka maelfu ya waafrika wenzetu kupoteza maisha huku yeye akichota madini au mmarekani yupi?
Dunia kwa sasa ni China vs America

Ukitaka udhurumiwe chagua China
Ukitaka kufaidika chagua America
 
Nyonzo bin mvule ni kwa nini waafrika tunaambiwa na mmarekani tupigane halafu sisi tunakubali kupigana?? Kwani sisi waafrika hatuna akili ama uwezo wa kukataa kupigana? Yaani tusipopigana wenyewe kwa wenyewe mmarekani atafanya nini??
 
Usitujumlishe wote,,, sie wabongo hata tuambiwe tuandamane hakuna atakae tokea, sembuse kupigana..... Cc makamanda na kimambi
 
Dunia kwa sasa ni China vs America

Ukitaka udhurumiwe chagua China
Ukitaka kufaidika chagua America
Katika washirika muhimu wa Marekani barani Afrika nchi yako ni miongoni mwao hiyo faida mbona hatuja wahi kuiona?
 
Katika washirika muhimu wa Marekani barani Afrika nchi yako ni miongoni mwao hiyo faida mbona hatuja wahi kuiona?
Chuki yako ya dini imekujaa kichwani
 
Usitujumlishe wote,,, sie wabongo hata tuambiwe tuandamane hakuna atakae tokea, sembuse kupigana..... Cc makamanda na kimambi
Kwa nini unaleta hoja za kivichekesho kwenye mambo muhimu yanayohitaji fikra jadidi? Hivi unadhani kama suala la zile harakati za Lindi zisingedhibitiwa leo hali ingekuwaje?

Yaani wewe hii mada umeona imetaja nchi? Huko nje hatutambuliki kwa hivi vijiinchi vyetu bali tunatambulika kama Afrika.
 
Tulikua tunawalaumu mababu zetu enzi za utumwa ila kumbe na sie ni wale wale. Akili ndogo tumejaliwa waafrika daah
 
Back
Top Bottom