Wababe wa dunia wanaiparamia Afrika, Waafrika wenyewe wanashangilia!!

Wababe wa dunia wanaiparamia Afrika, Waafrika wenyewe wanashangilia!!

Tulikua tunawalaumu mababu zetu enzi za utumwa ila kumbe na sie ni wale wale. Akili ndogo tumejaliwa waafrika daah
Kabisa!

Yaani unakutana na mtu kajipa kibyongo kwa mbwembwe za usomi na madaraka, lakini na yeye ni kibaraka wa hao wababe. Unadhani bila ya msaada wa viongozi wetu wa kale babu zetu wangechukuliwa utumwa kwa yale maelfu ya watu?

Leo hii kina Mangungo wetu ni hawa wanaoitwa waheshimiwa Rais, waziri, mabalozi na wabunge wa nchi zetu za Afrika.
 
Nyonzo bin mvule ni kwa nini waafrika tunaambiwa na mmarekani tupigane halafu sisi tunakubali kupigana?? Kwani sisi waafrika hatuna akili ama uwezo wa kukataa kupigana? Yaani tusipopigana wenyewe kwa wenyewe mmarekani atafanya nini??
Tamaa za wanasisa na uoga,, na hiyo sio tu Africa, hata kule ulaya huoni alivyowashika masikio wanachama wenzie wa NATO pale Ukraine anawalazimisha wapeleke vifaru wakati yeye mpaka leo hajapeleka na ukizingatia Ukraine si mwanachama wa NATO, lkn wanalazimishwa kwa nguvu ya mmarekani,, mfaransa kamshutikia kwa sasa ni kama anamkataa,,, hata waarabu nao wameshaamka wamechoka kuchonganishwa na huyo mmarekani, na ndio maana kwa sasa nchi kama Syria na saudi Arabia wamesaini peace halikadhalika saudia na Yemen vile vile,,, na muda wetu na sisi waafrika kuacha kupigana kisa tu mmarekani,, kila lenye mwanzo lina mwisho na mwisho wake unakaribia,,
 
Nyonzo bin mvule ni kwa nini waafrika tunaambiwa na mmarekani tupigane halafu sisi tunakubali kupigana?? Kwani sisi waafrika hatuna akili ama uwezo wa kukataa kupigana? Yaani tusipopigana wenyewe kwa wenyewe mmarekani atafanya nini??
Kuna mazingira flani yaani hutaki utapigana,unataka utapigana.

Hayo mambo muulize Putin Kwa Sasa atakupa jibu.

Hitler nae,alilazimika kupigana,
 
Kugombewa hakuepukiki maana rasilimali zipo za kutosha ila tatizo watawala wetu hawatambui vipaumbele vya raia wao au kuweka mbele maslahi ya hili bara wanapokutana na hao waviziaji, ni vigumu mno kufahamu wanazungumza na kukubaliana nini na hao mabeberu.
Hata wananchi hawajitambui.
 
Back
Top Bottom