Bila kupepesa macho wala kutikisa kichwa Wabongo tumejariwa unafiki tena wa Hali ya juu.
Hii ni juu ya tukio lililo tokea leo maeneo ya Uoanga huko Dar es salaam.
Ukiangalia comment za wadau juu ya tukio hilo wanaliingiza kwenye mambo mawili tofauti.
Mosi ikiwa ni siasa na pili ikiwa ni uzembe wa Polisi kitu ambacho sicho.
Imagine police walivyo jitahidi kadiri ya uwezo wao wewe mtu ambae upo mbali na tukio unakuja kuanza kuwashutumu polisi eti ni wazembe mara wangemoiga miguuni au mikononi ili wapate kumhoji, hivi mpaka mtu ajitoe hivyo na wewe upige miguu au mikono harafu uende kichwa kichwa unajua kuna nani nyuma yake? Je, kama yeye ni chambo utajuaje?
Hapo ndo anakuja mtu ambaye hata mazoezi ya Mgambo yalimushinda anaanza kumlaumu police.
Watanzania tujitafakari ukiwa sehemu ya tukio ni hali tofauti na aliye JF hivyo kama hujui kausha siyo uanze kulaumu tu.
Pia swala la kuhusisha mara ni mwana chama wa chama fulani kwa kutoa piacha akiwa amevalia sare na kuonyesha kadi ya chama na mbaya zaidi kila mtu anatoa kuwa jamaa wa chama hiki mwingine chama kile.
Kwani tukio analifanya binafsi kama mtu au kama mwanachama? Basi wabongo tujitafakari.
Na pia wengine wameanza kutoa yao eti jamaa alikuwa na ugonjwa wa akili angekuwa timamu asinge fanya hivyo, sawa siwezi wapinga sababu sina uhakika kwa hilo.
Je, siku hizi machizi wanavamia kwa kutumia silaha harafu wanachukua silaha yaani kichaa ametarget hayo yote kweli? Labda ni kweli ila kwa nini tunasema kana kwamba tunaujua ukweli.
Wabongo mjitafakari.
Unakuta hata mwalimu aliye soma kuchambua sentensi kwa njia ya matawi nae analeta porojo hapa eti walikosea, sasa wewe hao ndo wenye taaluma zao waache.
"No research no right to speak kindly be informed" ni hayo tu.
Povu ruksa