Wabongo wakijisifu ujinga

Wabongo wakijisifu ujinga

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kwenye mada. Umewahi kutana au kusikia wabongo wakijisifu ujinga? Sijui ni kutojua au sijui ni nini? Mi nawakutaga wa hivi.

1. Mi mvivu sana kunywa dawa, yaani si malizagi kabisa. Wamenisema wameacha wenyewe. Hapo anongea kwa sifa. Hajui kuwa kutomaliza dawa kuna madhara makubwa na si jambo la kujisifia.

2. Mwingine utasikia, he, huyo! Mvivu kula kama nini!?. Wanaona kama ni sifa wao au watoto wao wakiwa wavivu kula.

3. Mwingine anaona sifa kuwa na allegy(mzio). Utasikia, kambale silagi kabisa(kwa tone ya sifa). Mwili wangu huu unachagua sana vyakula.

4. Afadhali siku hizi tumeelimika na tumeacha kujisifu kuwa na vitambi. Ila ninaona kama kuna katrend ka kujisifia kuwa na UTi!!.

Ni ujinga gani ulikuta wabongo wanajisifia.
 
Wanajisifu au wanazungumza kana kwamba kulichukulia hilo jambo la kawaida tu?
 
Naeza kukaa siku tatu bila kuoga na vilevile Mimi Nina boxer moja tu
 
Na kuna ile 'yeye anajifanya anajitoa ufahamu, yaani hajui mimi ndiyo kichaa sasa, mpaka kwetu wanafahamu jinsi gani mimi ni kichaa'...!!


Sasa unashindwaaa..!
Kauli ya kwamba Mimi ni kichaa hata Rais wa nchi alishaitoa Jukwaani. Ina maana na yeye alijisifu Ujinga?
 
Yule jamaa anakula sana bigijiii, kama fagasoni
 
Back
Top Bottom