Wabongo wampiga Majungu Lulu Diva

Wabongo wampiga Majungu Lulu Diva

Nyumba ya mama yake ya kijijini kwao Muheza ndio chanzo cha Madongo , wadai ni duni kuliko bata alizokuwa anakula DSM .

Hii ni baada ya wasanii wengi kuhudhuria mazishi ya mama yake aliyefariki hivi karibu jijini DSM , wanadai mbona nyumba yake ya Dar ina viwango vya kuridhisha kuliko kwao , ambako kunaonekana kulitelekezwa ?

Natoa wito kwa WASANII WA KIBONGO kukumbuka makwao wanapofanikiwa kimaisha , wasisubiri Aibu .

View attachment 2053960
Kuanza kujenga nyumbani kabla ya kwako hasa kwa sisi wenye vipato vya kati ni kosa la kiufundi ambalo linaweza kukugharimu mno.
 
Kwanini alikwenda kumzika huko? facts of our case are not in consonant with the actions after death! UKIJUA UTAMZKA HUKO UJOMBANI, BASI patengeneze angalau kwa nyumba ya tope iliyopigwa lipu, au usimzike huko after all wamemtelekeza, sasa why kumzika huko....
Amezikwa pale kwa sababu ndio alikozaliwa. Narudia point yangu, kujenga nyumba kisa watakuja kuzika siku mbili na kuondoka ni matumizi yasiyo ya lazima. After that hiyo nyumba haitakuwa na matumizi tena kwako. Watu hawajengi jengi tu
 
Mnaozaa ili mje msaidiwe jifunzeni...kwenye hili swala mchaga atabaki kuwa juu daima, mchaga hawezi kubali alikotokea pawe pa hovyo unless na yeye anaishi hovyo
 
Kuna wakati huwa nawaelewa sana wachaga kuhusu kujenga kwao, kurudi kwao kila mwaka na kujali maisha ya kijijini kwao.

Lawama za watu kwa Lulu Diva zimelenga kuonyesha kuwa wasanii wengi wa Tz wanaishi maisha ya kuigiza, hawana msaada wowote kwa jamii zao na ni mafukara wanaoishi mjini kiujanja ujanja.

Haijarishi hapo ni kwa bibi, ujombani au kwa binadamu yake Lulu Diva, lakini sote tunajua hapo ni kwao na ndio maana mzazi wake amepelekwa kuzikwa! Pangekuwa ni mahali penye nyumba na mazingira ya maana, picha zingekuwa zimejaa Instagram akiwa anaposti akiwa msibani kwa ufahari.

Tukubali jambo moja tu, hili la Lulu Diva liwe fundisho kwetu sote.
 
Kwanini alikwenda kumzika huko? facts of our case are not in consonant with the actions after death! UKIJUA UTAMZKA HUKO UJOMBANI, BASI patengeneze angalau kwa nyumba ya tope iliyopigwa lipu, au usimzike huko after all wamemtelekeza, sasa why kumzika huko....

Hivi nyie mnajua stress za kuuguza? sio kuuguza wiki 1 au mwezi
 
Hakua na mamlaka ya kuamua azikwe wapi. Angekua na mamlaka asingeenda huko ujombani labda. Mwili wa mbondei hauzikwi ugenini kirahisi eti ndio mila zao.
Lulu kamuuguza mama yake akamfia,amewapelekea maiti yao wakaiangalie na kuzika. Aachwe huyo binti. Huwezi ukajenga nyumba ujombani wakati ukitaraji kufurahisha watakaoenda misibani.
Mbona sijaona anayelalamika kwanini hakumhudumia mama yake?

Yaani
 
Kuanza kujenga nyumbani kabla ya kwako hasa kwa sisi wenye vipato vya kati ni kosa la kiufundi ambalo linaweza kukugharimu mno.

Tena sio nyumbani tu alipozikwa mama ake lulu ni kwa Mama wa mama yake Mama lulu

Haya hao wanaopiga midomo wamewajengea mabibi wa mama zao?
 
Nyumba ya mama yake ya kijijini kwao Muheza ndio chanzo cha Madongo , wadai ni duni kuliko bata alizokuwa anakula DSM .

Hii ni baada ya wasanii wengi kuhudhuria mazishi ya mama yake aliyefariki hivi karibu jijini DSM , wanadai mbona nyumba yake ya Dar ina viwango vya kuridhisha kuliko kwao , ambako kunaonekana kulitelekezwa ?

Natoa wito kwa WASANII WA KIBONGO kukumbuka makwao wanapofanikiwa kimaisha , wasisubiri Aibu .

View attachment 2053960
Bila shaka watakuwa bavicha.
Maana akili zao hazitofautiani na wa Tigray
 
Kujenga ujombani yataka moyo sana.

Mpaka linakuja swala la kujenga kwa bibi maana yake ni kwamba kwanza babu na bibi walishindwa kujenga nyumba nzuri, pili, wazaliwa wa pale wameshindwa kujenga kwa miaka si chini ya 40, halafu wanatarajia kijana mwenye umri wa miaka 25-30 afanye maajabu kwa kujenga nyumba iliyoshindikana kujengwa kwa miaka Kati ya 40-60.

Halafu kijana huyohuyo awalishe wajomba, awahudumie wazazi na bado ajenge maisha yake Ili asiwe masikini kama wajomba.
 
Wamuache amalize kuomboleza
Screenshot_20211223-113841_1.jpg
 
Back
Top Bottom