Kuna wakati huwa nawaelewa sana wachaga kuhusu kujenga kwao, kurudi kwao kila mwaka na kujali maisha ya kijijini kwao.
Lawama za watu kwa Lulu Diva zimelenga kuonyesha kuwa wasanii wengi wa Tz wanaishi maisha ya kuigiza, hawana msaada wowote kwa jamii zao na ni mafukara wanaoishi mjini kiujanja ujanja.
Haijarishi hapo ni kwa bibi, ujombani au kwa binadamu yake Lulu Diva, lakini sote tunajua hapo ni kwao na ndio maana mzazi wake amepelekwa kuzikwa! Pangekuwa ni mahali penye nyumba na mazingira ya maana, picha zingekuwa zimejaa Instagram akiwa anaposti akiwa msibani kwa ufahari.
Tukubali jambo moja tu, hili la Lulu Diva liwe fundisho kwetu sote.