Wabongo wampiga Majungu Lulu Diva

Wabongo wampiga Majungu Lulu Diva

Hao wabongo waache upumbafu na waondoe matope kichwani. Huyo Diva angejenga nyumba ya nani? Kazaliwa peke yake kwa mama yake, hana ndugu wala baba, anaishi na mama yake aliyekuwa mgonjwa miaka mitano kasoro kiasi kwamba anahitaji uangalizi wa karibu. Ameishi na mama yake mwenyewe na uko kwao kijijini ni ujombani kuna wajomba kibao wanasubiri ajenge nyumba kisha waishi wao.

Unajua kuna wabongo wana akili za kizamani. Kwahiyo Wahindi wanaoishi NHC hawana hela au ni wajinga, cost benefit analysis haimruhusu Lulu Diva kujenga pale.

Unajenga nyumba ili wakija kuzika waipige picha? Unamjengea mtu unayeishi nae na hakuna siku atakaa kwenye hiyo nyumba. Hao wabongo wanadhani Lulu Diva ni mjinga alikuwa hajui ule ugonjwa hauna kurudi nyuma. Hawajui stress za kuuguza mama ukiwa mtoto wa pekee yani huna hata ndugu wa kushauriana nae wala baba hayupo. Tena kwa miaka minne plus
😍
 
Ikiwa mtu anakuwa na ratiba walau ya kwenda kusalimia kwao na akakaa siku mbili au tatu vyovyote vile atawaza au hata kutamani awe na chumba kimoja anaweza kuja kupumzika. Kuuguza kupo ila hajazaliwa na kukua ndo akaanza kuuguza for good. Wanaotetea hapa wengi ndo hawa masuti njiani nyumbani kunguni tele. Inauma sana si vijana tu wa leo ila hata watu wazima kusahau walipotoka. Unaposema sijui kwa mjomba mara bibi mzaa mama jiulize kwao ni wapi. Kwanin leo tunaona kumbukizi za nyumba hata watu maarufu kwamba nikizaliwa hapa nikakulia hapa hatimaye akaanza maisha kwingine? Vyovyote vile wabongo tunapenda show off nyingi sana kumbe nyumbani ulikozaliwa ni nyumba za tembe! Tokweni na mapovu kama yote ila nyumbani ni nyumbani.
 
Amezikwa pale kwa sababu ndio alikozaliwa. Narudia point yangu, kujenga nyumba kisa watakuja kuzika siku mbili na kuondoka ni matumizi yasiyo ya lazima. After that hiyo nyumba haitakuwa na matumizi tena kwako. Watu hawajengi jengi tu
Unazikwa ulikozaliwa au ulikoolewa! Kama Ni wabondei sawa wao waako tayari kuuza mashamba Wai Julie maiti waizike. If that is the case, then it is Ok
 
Amezikwa pale kwa sababu ndio alikozaliwa. Narudia point yangu, kujenga nyumba kisa watakuja kuzika siku mbili na kuondoka ni matumizi yasiyo ya lazima. After that hiyo nyumba haitakuwa na matumizi tena kwako. Watu hawajengi jengi tu
Uko sahihi if that is the case...kuzikwa alikozaliwa
 
Hakua na mamlaka ya kuamua azikwe wapi. Angekua na mamlaka asingeenda huko ujombani labda. Mwili wa mbondei hauzikwi ugenini kirahisi eti ndio mila zao.
Lulu kamuuguza mama yake akamfia,amewapelekea maiti yao wakaiangalie na kuzika. Aachwe huyo binti. Huwezi ukajenga nyumba ujombani wakati ukitaraji kufurahisha watakaoenda misibani.
Mbona sijaona anayelalamika kwanini hakumhudumia mama yake?
Kama Ni Mbondei, then it is Ok. Wabondei usipime na maiti! Wakorofi Sana na bila kumuhudumia mgonjwa
 
Kuna wakati huwa nawaelewa sana wachaga kuhusu kujenga kwao, kurudi kwao kila mwaka na kujali maisha ya kijijini kwao.

Lawama za watu kwa Lulu Diva zimelenga kuonyesha kuwa wasanii wengi wa Tz wanaishi maisha ya kuigiza, hawana msaada wowote kwa jamii zao na ni mafukara wanaoishi mjini kiujanja ujanja.

Haijarishi hapo ni kwa bibi, ujombani au kwa binadamu yake Lulu Diva, lakini sote tunajua hapo ni kwao na ndio maana mzazi wake amepelekwa kuzikwa! Pangekuwa ni mahali penye nyumba na mazingira ya maana, picha zingekuwa zimejaa Instagram akiwa anaposti akiwa msibani kwa ufahari.

Tukubali jambo moja tu, hili la Lulu Diva liwe fundisho kwetu sote.

Mnalazimisha ajenge mnajua kuuguza ilivyo gharama nyie
Hao wajomba zake walitakiwa wajenge na sio lulu diva
 
Kuna wakati huwa nawaelewa sana wachaga kuhusu kujenga kwao, kurudi kwao kila mwaka na kujali maisha ya kijijini kwao.

Lawama za watu kwa Lulu Diva zimelenga kuonyesha kuwa wasanii wengi wa Tz wanaishi maisha ya kuigiza, hawana msaada wowote kwa jamii zao na ni mafukara wanaoishi mjini kiujanja ujanja.

Haijarishi hapo ni kwa bibi, ujombani au kwa binadamu yake Lulu Diva, lakini sote tunajua hapo ni kwao na ndio maana mzazi wake amepelekwa kuzikwa! Pangekuwa ni mahali penye nyumba na mazingira ya maana, picha zingekuwa zimejaa Instagram akiwa anaposti akiwa msibani kwa ufahari.

Tukubali jambo moja tu, hili la Lulu Diva liwe fundisho kwetu sote.

Mbona husemi pia liwe fundisho kwetu sote jinsi Lulu alivyomuuguza Mama yake kwa miaka 5 hadi kamfia akiwa peke yake bila msaada wa hao ndugu mnaotaka awajengee nyumba ?
 
Mlowajengea nyumba bibi zenu rusheni hizo nyumba tuone sio kumsema lulu tu

Siyo tu bibi zao,unakuta wanamsimanga Lulu wakati wao hata Wazazi wao bado wanaishi nyumba za kupanga.

Huyu Binti anahitaji pongezi,kuuguza karibu miaka 5 tena ugonjwa unajua haponi na bado akapambana hivyo hivyo,anahitaji pongezi na si kubezwa.Kuna watu humu utakuta hata kutuma pesa ya panadol kwa Wazazi wao ni mtihani,lakini hapa JF ndiyo wanaongoza kumsimanga Lulu.
 
Nimemuuguza baba for over ten yrs, mama for more than 20!

Hakuna excuse kwa kutokujenga nyumbani wengi wanaotetea vijijini kwao kutakua na tatizo, haiwezekani vijijini tupatelekeze kisa tupo mjini hapana lazima tuelezane ukweli tubadilike na sio huyo binti pekee wapo watu wengi na nyumbani haupatengenezi kwa ajili ya msiba tu hapana hata kwenda mapumziko
 
Hakuna excuse kwa kutokujenga nyumbani wengi wanaotetea vijijini kwao kutakua na tatizo, haiwezekani vijijini tupatelekeze kisa tupo mjini hapana lazima tuelezane ukweli tubadilike na sio huyo binti pekee wapo watu wengi na nyumbani haupatengenezi kwa ajili ya msiba tu hapana hata kwenda mapumziko

Hivi kwa umri wa Lulu na kuuguza Mama yake kwa miaka mitano ukilinganisha na kipato chake,ungekuwa wewe ungeweza kweli? Mnaongea hapa wakati pengine wewe hapo uko kwa mid 40’s umekaa kazini or kwa biashara zako kwa zaidi ya 20 yrs,unataka huyu Binti ambae ndiyo kwanza anajikusanya kimaisha anakutana na changamoto ya kuuguza Mama yake,afanye yale wewe umeyafanya kwa zaidi ya 20yrs.Hii si sawa.
 
Hivi unakumbuka alivyotangaza kuwa mahari yake ni millioni 200..ndio maana watu wanakomaa nae...

Point nyepesi sana hii wala haireflect uhalisia tunaouongelea hapa,nakuuliza ni wapi huyu Binti kafake maisha,kama angefake wewe ungeweza kuona hata hiyo nyumba ya Bibi yake?
 
Kwanini alikwenda kumzika huko? facts of our case are not in consonant with the actions after death! UKIJUA UTAMZKA HUKO UJOMBANI, BASI patengeneze angalau kwa nyumba ya tope iliyopigwa lipu, au usimzike huko after all wamemtelekeza, sasa why kumzika huko....
Tatizo la nyinyi mnaokulia kwenye pesa kila kitu mnakikuta mna shida sana. Nyie mnafikiri alikuwa hawazi hayo? Hivi ugonjwa ukifika kwenye nyumba yako unaweza anza kuwaza kujenga kwanza sehemu ya kumzika akifa au utahangaika na matibabu?

Kwenye maisha mahitaji ni mengi na yote muhimu ila tunayapa kipaumbele cha umuhimu na ndio maana mengine tunajikuta yametokea ya kutokea hata kabla hatujayafikia na kuyatimiza.


Tuseme Lulu akiwa anaanza kushika pesa anamuahidi mama yake kumjengea nyumba halafu haijatimia hata miezi anaanza kuugua kwa miaka mitano mbele. Unafikiri ile ndoto ya kumjengea mama yake inakuwepo tena? Bila shaka hapo ni matibabu ndio yanakuwa kichwani mwake. Kwenye matibabu watu wanauza hadi nyumba zao na mtu anakufa na unaenda kufikia kwenye hizo nyumba ili kumsitiri ndugu yako.

Huyu binti ameyabeba majukumu kama mwanaume. Kwenye hii dunia yuko peke yake anahitaji faraja. Na hili unaweza kuona wakati anashukuru kwa waliofika kumzika mama yeke. Sio utamaduni wa kiafrika kabisa mwanamke kutoa shukrani hasa mtu ambeye ni mfiwa kabisa. Kunakuwa na utaratibu ndugu mmojawapo anasema neno kwa niaba ya familia. Lakini yeye alisimama. Na hii inaweza muathiri kiakili pakubwa na kwa muda mrefu. Walikuwa wapi wakina Idriss Sultan ndugu zake? Wajomba walikuwa wapi kumzuia asiongee?

Hana cha kulaumiwa ametimiza sehemu yake mengine ni blaablaa tu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom