Wabunge 19 ni sawa na watumishi hewa kwa kuwa hawatambuliki kokote

Paulsylvester

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2021
Posts
1,464
Reaction score
3,379
Ndugu zangu watanzania, Salaam

Mimi nawauliza tuu wavuja jasho wa nchi hii tunaonyonywa sana na kitu inaitwa CCM!

Ikiwa kina Mdee na wafuasi wake hawatambuliki popote pale kisheria na hata kikanuni zozote zile za wao kuwepo Bungeni mpaka sasa...!

Kwa maana nyingine, kodi yangu Mimi paulsylvester inalipwa kwa mtu ambaye hayupo kwenye sisitimu yoyote ile, ni sawa na ule wimbo uliovuma kipindi cha msiompenda kwa idadi yenu chache na kupendwa na idadi ya mamilioni ya Watanzania kwa maama ya JPM na wimbo wa wafanya kazi hewa!

Mpaka sasa, kina mdee ni wafanya kazi hewa, kwa kuwa hawatambuliwi kokote kule.

Aidha wanasheria mtupe mwongozo kwamba, kwa nini hao wabunge 19 hewa wako bumgeni?

Vinginevyo, Tunataka katiba kwa nguvu na manjonjo meengi, wakati hatuwezi kuitetea na kuilinda iliyopo na imewatolea nje hao wabunge hewa,

Tukiipata tunayoitaka, ni Nani ataitetea yanapotokea mambo kama haya!

Kwanini tusiite nchi yetu ni ya Kilokole inayotarajia kila kitu Mungu atafanya!?

Au kuna mwenye ziada ya haya?
 
It's an interesting movie, ngoja tule [emoji897], kuna wengine wanazitaka izo nafasi na wengine wanapigania kula yao warudi kwenye system.
Inauma sana mkuu!

Mkuu, uewahi kujiuliza, ni kwa nini watanzania huwa hatuwezi kuzisimamia haki zetu kwa gharama yoyote...?
 
Hivi Tulia anataka nini kifanyike mpaka akiri kwamba kina Mdee hawastahili kuwepo bungeni?

Alitaka mahakama itoe uamuzi wakati sheria tayari ipo wazi, jana mahakama ikatoa uamuzi.

Lakini bado kina Mdee wapo bungeni, hivi unapokuwa na kiongozi wa mhimili unaotunga sheria, halafu mwenyewe hazifuati hizo sheria hii maana yake nini?

Kwanini tumekubali kuwa taifa la wapuuzi kiasi hiki? kwa hili Spika anaonesha wazi hajiamini, anasubiri go ahead toka kwa yule aliyempa huo uspika, hatuna bunge.
 
Supika kakalia kuti KAVU...
Kiuharisia Speaker hawezi kuwafukuza Bungeni hao covid19 kisa tu kasikia fununu kwamba wameshindwa mahakamani. Bali CDM wanalo jukumu la kuchukua mahakamani copy of judgment kisha wakaipeleka kwa speaker officially ndiyo speaker anaweza kufanya uamuzi stahiki. Elewa hilo mkuu acha lawama kwa jambo ambalo halihitaji lawama.
 
Wabongo bhana, siku zote mnapeleka lawama kusiko, Spika anafwata anavyotaka Raisi na Mkuu wa CCM hata yeye mwenyewe Tulia kabla hajawa Spika Ndugai alivyotimuliwa alisema Serikali iko JUU ya Bunge hivyo hakuna cha mambo ya Muhimili.

Hivyo Serikali ndiyo inayotaka hao Wabunge waendelee na pelekeni malalamiko yenu moja kwa moja kwa Serikali na siyo Spika.

Serikali ndio huamua nani afungwe yupi aachiwe, yupi ana kesi ya kujibu yupi hana na siyo Jaji wa Mahakama yoyote ile.

Hata Mbowe aliachiwa na Raisi na siyo Mahakama au jaji, akina Ruge na Muhindi wake waliachiwa na Raisi na siyo Mahakama, …
 
Ndugu zangu watanzania, Salaam

Mimi nawauliza tuu wavuja jasho wa nchi hii tunaonyonywa sana na kitu inaitwa CCM!

Ikiwa kina Mdee na wafuasi wake hawatambuliki popote pale kisheria na hata kikanuni zozote zile za wao kuwepo Bungeni mpaka sasa...!

Kwa maana nyingine, kodi yangu Mimi paulsylvester inalipwa kwa mtu ambaye hayupo kwenye sisitimu yoyote ile, ni sawa na ule wimbo uliovuma kipindi cha msiompenda kwa idadi yenu chache na kupendwa na idadi ya mamilioni ya Watanzania kwa maama ya JPM na wimbo wa wafanya kazi hewa!

Mpaka sasa, kina mdee ni wafanya kazi hewa, kwa kuwa hawatambuliwi kokote kule.

Aidha wanasheria mtupe mwongozo kwamba, kwa nini hao wabunge 19 hewa wako bumgeni?

Vinginevyo, Tunataka katiba kwa nguvu na manjonjo meengi, wakati hatuwezi kuitetea na kuilinda iliyopo na imewatolea nje hao wabunge hewa,

Tukiipata tunayoitaka, ni Nani ataitetea yanapotokea mambo kama haya!!

Kwa nini tusiite nchi yetu ni ya Kilokole inayotarajia kila kitu Mungu atafanya!??

Au kuna mwenye ziada ya haya??
Wabunge hao 19 wakiendelea kuwepo bungeni; wewe wanakunyonya kitu gani kulinganisha na kazi wanayoifanya? Kwani wakiondolewa wakawekwa wengine hawatalipwa?🤭

Halafu kuhusu kila kitu kutegemea Mungu atafanya ukweli ni kuwa kila jambo liko controlled na Mungu iwe ktk nchi iliyoendelea au lah

Usipende kutaja jina la Mungu bure
 
Hivi Tulia anataka nini kifanyike mpaka akiri kwamba kina Mdee hawastahili kuwepo bungeni?

Alitaka mahakma itoe uamuzi wakati sheria tayari ipo wazi, jana mahakama ikatoa uamuzi.

Lakini bado kina Mdee wapo bungeni, hivi unapokuwa na kiongozi wa mhimili unaotunga sheria, halafu mwenyewe hazifuati hizl sheria hii maana yake nini?

Kwanini tumekubali kuwa taifa la wapuuzi kiasi hiki? kwa hili Spika anaonesha wazi hajiamini, anasubiri go ahead toka kwa yule aliyempa huo uspika, hatuna bunge.
Exactly...
 
Mahakama haijatoa uamuzi bali yanahitajika tu marekebisho
 
Kwani ni lazima unionyeshe jinsi ulivyo.??
🤭kwa taarifa yako kinachoendelea hapo ni kuwa wabunge waliopo wanapigania kubaki na chama chako kinapigania wawapeleke wa kwao kwa maslahi binafsi.

Hii ngoma ngumu.. msiihusishe CCM ktk mambo ya hovyo. Hayo ni makosa yenu wenyewe watu wa ufipa kufanya mambo bila kuzingatia utaratibu na HAKI
 
Wabunge hao 19 wakiendelea kuwepo bungeni; wewe wanakunyonya kitu gani kulinganisha na kazi wanayoifanya? Kwani wakiondolewa wakawekwa wengine hawatalipwa?🤭

Halafu kuhusu kila kitu kutegemea Mungu atafanya ukweli ni kuwa kila jambo liko controlled na Mungu iwe ktk nchi iliyoendelea au lah

Usipende kutaja jina la Mungu bure
Ultimalizia vizuri kaka, ila ulikoanzia ni utopolo tupu!

Lakini uelewe pia, Mungu anaheshimu mapatano yetu kama nchi kwa kutaweka kwenye katiba, na kwa maana hiyo, Mungu anataka pia akili zetu zitatue changamoto zetu mkuu
 
🤭kwa taarifa yako kinachoendelea hapo ni kuwa wabunge waliopo wanapigania kubaki na chama chako kinapigania wawapeleke wa kwao kwa maslahi binafsi.

Hii ngoma ngumu.. msiihusishe CCM ktk mambo ya hovyo. Hayo ni makosa yenu wenyewe watu wa ufipa kufanya mambo bila kuzingatia utaratibu na HAKI
Ungejua unayebishana naye ni.... Usingeleta habari za ufipa
 
Badala upinzani uungane na kushirikiana kutoa hii SISIEM madarakani , huu ni wakati wa kujenga chama na kuunda mikakati ya kuchukua Dola.

ila nasikitika kuona ndo wako buzy kubomoana.

HII NCHII HAKUNA UPINZANI WENYE TIJA NA AKILI WALIOPO NI WAJINGA TU
 
Chezeeni tu jasho la wanyonge..hakuna marefu yasiyo na ncha...ni suala la muda tu...
Hawa sisiem wanatuchezesha kama midori yaani, watu zaidi ya M60, tunachezeshwa na watu wachache

Kila njia inaukomo wake!
 
Back
Top Bottom