Mbowe awe mhuni kuchezea kodi za wananchi kipuuzi ivyo uku nchi ikiwa na serikali na vyombo vyakisheria.aise mbona ulichokiandika hakiendani.Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
Aisee!.
Mama na JPM kumbe ni kitu kimoja.
Wadhaifu ni wote wasio na maadili na bahati mbaya wamepewa majukumu makubwa ya kulitumikia taifa na wanalipwa Kwa utumishi huo.Chadema wameshindwaje kutetea nafasi zao 19 za ubunge?
Je Chadema ni chama dhaifu?
Katiba ndiyo dhaifu!Chadema wameshindwaje kutetea nafasi zao 19 za ubunge?
Je Chadema ni chama dhaifu?
Na pia ili Mbowe chama chake ki savivecovid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi
Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
Hilo NENO upo sahihi mkuu Covid 19 wanatumikakuna idadi ya wabunge wa upinzani inahitajika kwenye kamati za utawala bora ili kupata euros za european union za kuendesha bunge sasa mwaka 2020 waliiba kupitiliza kwa hiyo covid 19 wanatumika kudanganyia wazungu kwamba kuna upinzani bungeni na demokrasia
Tukutane 2025 ndio mahakama itatoa uamzi 😆😆😆😆Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.
=====
Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.
Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.
Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.
Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.
Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.
Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.
Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.
Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.
Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.
Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.
Pia, Soma;
=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum
=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi
=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708
Hawakwenda mahakamaniHivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?
Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??
Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??
Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??
Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??
Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??
Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Ulikuwo.kwenye list fake ya mwenyekiti 🤣🤣🤣🤣Upumbavu mtupu, CCM imeharibu hii nchi
Zitto ilienda hadi miezi 24Wengi mpo gizani, kesi hii ikichukuwa muda mrefu ni miezi mitatu tu, muulize ofisa wa mahakama yeyote unayemjuwa.
Kwenye kifo cha Magu ulikuwa unademka kwamba ni karma ila hapa hutaki kuamini kma ni karma?Tanzania ina wasomi wa hovyo sana, kuna Mtu anajiita P atakuja na kukwambia mambo ya voices from within, tokea lini nchi ikaendeshwa na voices from within? au utasikia kila kitu kihahusisha KARMA- KARMA ni katiba ya nchi au chama? Alafu anajinasibu ni mawili nguli wa sheria- ni aibu kwa wasomi wa Tanzania.
Kwani wewe wakifukuzwa au kuendelea kuwa wabunge unafaidika na nini?Huwa najiuliza maswali mengi sipati majibu.. hivi CCM inafaidika vp na hao wabunge 19? Kwanini mnahubiri maridhiano wakati nyie hampo tayari? Mnaturudisha nyuma Sana. Achanane na siasa za kukomoana tusonge mbele.
Asiende ikulu kwani dhalimu yupo?Hili nililijua toka mwanzo, ndio maana nikawa nashangaa Mbowe anafuata nini ikulu kila mara tena mwenyewe?!
Kwani aliepo madarakani ni yule dhalimu wako?Maamuzi ya mahakama yataendana na utashi wa serikali.
Asiende ikulu kwani dhalimu yupo?
Si alishaondoka? Na mungu wenu aliwasaidia kuwaondolewa utawala wa kidhalimu bila kumwaga damu?