Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
Mbowe awe mhuni kuchezea kodi za wananchi kipuuzi ivyo uku nchi ikiwa na serikali na vyombo vyakisheria.aise mbona ulichokiandika hakiendani.
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi

Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi

Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
Na pia ili Mbowe chama chake ki savive
 
kuna idadi ya wabunge wa upinzani inahitajika kwenye kamati za utawala bora ili kupata euros za european union za kuendesha bunge sasa mwaka 2020 waliiba kupitiliza kwa hiyo covid 19 wanatumika kudanganyia wazungu kwamba kuna upinzani bungeni na demokrasia
Hilo NENO upo sahihi mkuu Covid 19 wanatumika

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708
Tukutane 2025 ndio mahakama itatoa uamzi 😆😆😆😆
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??

Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Hawakwenda mahakamani
 
Tanzania ina wasomi wa hovyo sana, kuna Mtu anajiita P atakuja na kukwambia mambo ya voices from within, tokea lini nchi ikaendeshwa na voices from within? au utasikia kila kitu kihahusisha KARMA- KARMA ni katiba ya nchi au chama? Alafu anajinasibu ni mawili nguli wa sheria- ni aibu kwa wasomi wa Tanzania.
Kwenye kifo cha Magu ulikuwa unademka kwamba ni karma ila hapa hutaki kuamini kma ni karma?
 
Hakika sasa naanza kuamini Uwepo wa Wabunge 19 waliofukuzwa na Chama chao na kukosa SIFA ya kuwa Wabunge kwa Mujibu wa KATIBA KATIBA ambayo VIONGOZI WALIAPA KUILINDA kuna MASLAHI MAKUBWA kwa CCM
Haiwezekani WABUNGE wasio na SIFA waendelee Kulipwa MISHAHARA na POSHO ambazo ni KODI za Wananchi.
MAHAKAMA haijatoa ZUIO inakuwaje SPIKA anasubiri Mahakama imalize Kusikiliza Shauri lao.
NCHI hii VIONGOZI walioapa KUILINDA KATIBA ndio hao WANAOICHEZEA KATIBA watakavyo.


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Chadema tulizeni mshono, kazi yenu ya kuwafukuza uanachama mmeshaimaliza
 
Huwa najiuliza maswali mengi sipati majibu.. hivi CCM inafaidika vp na hao wabunge 19? Kwanini mnahubiri maridhiano wakati nyie hampo tayari? Mnaturudisha nyuma Sana. Achanane na siasa za kukomoana tusonge mbele.
Kwani wewe wakifukuzwa au kuendelea kuwa wabunge unafaidika na nini?

Ni wabunge wa Kambi ya upinzani Bungeni.
 
Hili nililijua toka mwanzo, ndio maana nikawa nashangaa Mbowe anafuata nini ikulu kila mara tena mwenyewe?!
Asiende ikulu kwani dhalimu yupo?

Si alishaondoka? Na mungu wenu aliwasaidia kuwaondolewa utawala wa kidhalimu bila kumwaga damu?
 
Wameshafukuzwa, kesi inaweza ikachukua kama miaka 2 hivi halafu watashindwa.
 
Back
Top Bottom