Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Habari!

Huu ndio ukweli ambao sisi wapunzani hatutaki kuusikia

Ila kwa akili tu za kujua kutofautisha sato na kambare, ugali wa na ubwabwa inatosha kufahamu kuwa Halima Mdee na wenzake 18 ambao ni wabunge wa vitu maalumu kutoka CHADEMA wataendelea kuwa wanachama wa CHADEMA mpaka hatua za mwisho karibu na uchaguzi mkuu.

Watahama CHADEMA na kuhamia CCM ili wagombee tena ubunge na kuupata tena.
Hapa kilicho Baki ni kampeni kama iliyomfurusha shotii kwenye kiti hata akatoka nduki
Hilo NENO upo sahihi mkuu Covid 19 wanatumika

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Nawafananisha na like kundi la leprofesor Mzee ya bugurunri na kundi lake la wanacuf mamluki🚶
 
Na mahakama itakapoamua kuimaliza hii kesi 2025, sijui itakuwaje mkuu Quinine?
Itakuwa kama zile kesi za chafuzi 2019/2020 za wanachadema zisizo Isha na zinazowatesa wanachama wengi wa chadema magerezani Kwa kesi bambikizi za chafuzi zilizo ratibiwa na wanachukua chako mapema 🤔
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??

Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Utawabakizaje bungeni bila amri ya mahakama kwa spika!
 
Mfumo uliamua waende bungeni, mfumo unawaweka bungeni na utaendelea kuwaweka bungeni
Wanakuwa ni wabunge wasiokuwa na chama.
Wanalipwa fedha za kodi zetu bila sababu za maana. Kwa nini wasikae nyumbani huku wakisubiri maamuzi ya Mahakama?.

Maamuzi ya hao Covid kufukuzwa Chadema yalikuwa sahihi kwakuwa wameshaonekana wanafanyakazi kwa maslahi ya CCM. Ndio maana leo wabunge wa CCM wameshangilia sana
 
Itakuwa kama zile kesi za chafuzi 2019/2020 za wanachadema zisizo Isha na zinazowatesa wanachama wengi wa chadema magerezani Kwa kesi bambikizi za chafuzi zilizo ratibiwa na wanachukua chako mapema 🤔
Katika hali hiyo basi, ni wajibu wa CHADEMA na waTanzania wengine wote wasiofurahishwa na hali hiyo kuendelea kuyashikia bango na kuyasemea kila mahala. Huu ni unajisi wa HAKI zetu sote.
 
Kwanza huyu Tulia anasubiri simu kutoka Ikulu, hana maajabu yoyote yale, yupo yupo tu kusubiria maelekezo ya Samia na system juu ya hawa covid 19.
Si unajuwa tena anayezindua na kuvunja Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

Anayeipa fedha Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais kwa saini yake ya kupitisha bajeti ya nchi kuwa sheria ili ndipo mafweza yatumike!

Anayemteua Karani Mkuu wa Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

Anayemteua Chief Whip wa Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

Anayemteua Kiongozi wa shughuli za serikali kwy Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

Baghosha!
 
===

===
1652709521811.png
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708
Ndo imetoka tena iyo mpaka 2025 watakuwa wabunge wa Mahakama, wenzao kina Hamad Rashid na wengine
Tanzania hakuna haki, huyu spika ata haendani na speed ya mama samia, huyu bado ni mazalia ya ndugai
 
CHADEMA hamuuwezi muziki wa CCM.... Yaani mnapigwa kisheria na kikatiba bila makelele. Mkiwa jeuri mnakutana na mkono wa dola iliyo chini ya CCM.... Kikao cha Mbowe na Mwenyekiti wa CCM siku moja kabla ya baraza kuu ndo kilikuwa hatima ya hili jambo. Baraza ilikuwa ni kutimiza ratiba tu.
 
Alipowaachia uamsho hakuingilia mahakama?
"Alipowaachia uamsho hakuingilia Mahakama?"

Hahahahaaaaaaaa.... sina mbavu... mkuu.

Tunapaswa kujuwa haya:-

1. Si unajuwa tena anayezindua na kuvunja Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

2. Anayeipa fedha Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais kwa saini yake ya kupitisha bajeti ya nchi kuwa sheria ili ndipo mafweza yatumike!

3. Anayemteua Karani Mkuu wa Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

4. Anayemteua Chief Whip wa Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

5. Anayemteua Kiongozi wa shughuli za serikali kwy Mhimili wa Bunge ni Mhe. Rais!

6. Bosi wa Mhe. Spika kwy Cabinet ni Mhe. Rais. Mhe. Spika ni Ex-officio kwy Cabinet.

7. Bila Mhe. Rais kuupa Mhimili wa Bunge AG Mhe. Spika hawezi kutimiza wajibu wake.

Baghosha!
 
Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
Eleza katiba imevunjwaje? Ibara au kifungu gani cha katiba?........Don't just speak out of nothing...

Au na wewe uko kama mtu mmoja anaitwa mzee Pascal Mayalla ameanzisha uzi akilalamika na kupiga kelele hewani kusema CHADEMA wamevunja katiba yao, wamevunja katiba yao...

Cha kushangaza hata hakwoti ibara au kifungu chochote cha katiba hiyo anachodai kimevunjwa/kiukwa. And I see you just crying and lamenting the same way with no evidence...

But, one BIG FACT remains, that... WAMESHAFUTWA UANACHAMA...!!

Na kwa maoni yangu, CHADEMA wako ktk mstari sahihi na wamechukua hatua sahihi kwa mujibu wa taratibu zao dhidi ya waliokuwa wanachama wao...

Ni haki yao kwenda mahakamani. Lakini wote tunajua hiyo ni "delaying tactic" tu. They know, the action is irreversible...

Mahakamani hawajaenda kupigania "uanachama" wao kwa CHADEMA. Mahakamani wamekwenda kuhakikisha "ubunge" wao na "maslahi ya ubunge" wao hayapotei. That's all. Nothing more. Nothingless....
 
Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Hujui CCM ndio waliomuweka hapo?
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708
Katika kufanya uamuzi wa jambo lolote, kuna vitu viwili vya msingi ambavyo ni;
1. Nia (njema au ovu)
2. Kitendo chenyewe.

Maamuzi ya spika yanatakiwa yatazamwe kwa kuzingatia vitu hivyo hapo juu, pamoja na katiba ya nchi, sheria na kanuni zinazohusika.
Hata hivyo, akili ya kawaida (common sense) ni muhimu katika kuangalia muda na mtiririko wa matukio hadi uamuzi kufanyika.
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA, waendelee kufanya shughuli zao za kibunge hadi Mahakama itakaposikiliza maombi yao ya zuio la muda kuhusu ubunge wao.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji John Mgeta baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Wabunge hao waendelee kuwa Bungeni ama laah, ambapo June 13, 2022 ndio atasikiliza zuio hilo.
#MillardAyoMAHAKAMANI
 
Back
Top Bottom