mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 340
- 359
Zikiwa zimesalia saa kadhaa mkutano wa baraza kuu la Chadema Kuanza,wabunge 19 wa bunge la Jamhuri ya Muungano wanaotokana na Chama hicho wamewasili maeneo jirani na kunapofanyika mkutano huu hapa Mlimani City.
Awali kulikuwa na sintofahamu ikiwa watahudhuria mkutano huo,walioalikwa kwa barua Rasmi za Chama zikiwatambua kuwa wanachama tofauti na kauli za awali kuwa si wanachama wa Chama hicho.
Wakati wabunge hao wakiwa maeneo haya ya Mlimani City,mjadala ulioanza usiku wa Jana na unaoendelea Sasa ni kama wabunge hao wahojiwe mbele ya baraza hilo,au wakahijiwe vyumbani ambapo tayari vyumba vitatu vimetemgwa kwa ajili hiyo.
Baadhi ya wajumbe wanaeleza ni muhimu wakahijiwa hadharani kila mmoja asikie kuliko kuitwa Chumbani na wajumbe kuja kupewa taarifa ya mahojiano hayo,huku kukiwa na taarifa za awali kuwa wabunge hao wameshafutwa uanachama na kinachosubiriwa ni baraza kuu kuhalalisha Jambo hilo.
Hisia hizo zinachangiwa zaidi na amaelezo ya John Mrema Mkuu wa Itifaki na mambo ya Nje Chadema wakati akizungumza na vyombo vya habari kuwa uamuzi umeshafanyika,na kinachosubiriwa ni kutangazwa.
Kauli ya Mrema inatakwa kupoka uamuzi wa baraza kuu hali iliyozua sintofahamu miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho
Kwa Sasa viongozi wakuu tumekubaliana kuwatumia influence wa Chama kushawishi katika mitandao ya kijamii juu ya uamuzi huu ikiwa ni njia ya kuwaandaa wanachama kutohoji Jambo hilo kuamuliwa nje ya baraza kuu
Stay Tune