Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na CHADEMA washiriki kikao cha Bunge leo

Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na CHADEMA washiriki kikao cha Bunge leo

Kwani ruzuku ni fedha za CCM?
Mazafanta!
Ruzuku ni Fedha kodi za waTz, wakiwemo CCM,CDM na wengine...!
Shida hapa uhalali wa Ruzuku kuliwa kigenge cha wachache na uharamu wa wanaosababisha ije unatokea wapi....! Kama umeamua kususa SUSA mwanzo mwisho sio huu usanii..!
 
Sasa hao walikata rufaa ya nini kama tayari wanakimbilia bungeni wakati rufaa yao haijasikilizwa.

Hapo sasa ndipo baraza kuu likae na liwafukuze kabisa ndio waje wawe wabunge wa mahakama. Iweje leo Magufuli awang'ang'anie wakati alisema wapinzani ndio wanazuia maendeleo.!
 
Hapa swali la Ester bulaya linajibiwa wanawatetea watanzania shida iko wapi?

Wanawatetea watanzania kwenye bunge la ccm! Tumeshawadelete, wao wavute posho zao kwenye hilo bunge kibogoyo la wamwaga damu. Lakini Kwa sasa hawana mvuto tena na wala cdm hawatambui.
 
Ruzuku mbona haikataliwi...!
Mwisho wa kufikiri?
Wale wabunge 19 wa Viti Maalumu wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), asubuhi hii wamefika na kuendelea na kikao cha Bunge kilichoanza leo Jumanne, Februari 2, 2021 Jijini Dodoma.

Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.
Wabunge hao ambao ni pamoja na Halima Mdee na Ester Bulaya, wametinga mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

Hata hivyo kabla ya kuanza kikao cha Bunge, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Wenye ulemavu, Jeniste Mhagama aliwaomba watoke nje kwanza.

Spika Job Ndugai ameomba wabaki nje kwanza na baada ya dua ameanza kuwaita akianza na wabunge watano wa kuteuliwa, kisha wakaingia wabunge watano wa ACT.

Mwisho waliitwa wabunge 19 wa Chadema wakiongozwa na Ester Matiko na Cesilia Pareso.

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya hawakuwa miongoni mwa walioingia mapema leo.
View attachment 1692348
View attachment 1692255
 
Ivi mbona kuna Clip nimesikiliza Juzi juzi hawa Wabunge 19 baraza lao kuu wameshawarudishia uwanachama wao?? Ivi Baraza wamekubaliana waendelee na ubunge wao ama inakuwaje naona sielewi hapa imekaaje hili sakata? naomba ufafanuzi
Clip ya uchochoroni hiyo,Baraza Kuu halijakaa kuwajadili na kamwe hawatarudishwa,hao watabaki kuwa wabunge wa Ndungai hadi 2025, huu ukiwa ni ushahidi wa jinsi kodi zetu zinavyochezewa.
 
Ruzuku mbona haikataliwi...!
Wacheni propaganda mfu hizo, hakuna ruzuku iliyotumwa, na hata ingetumwa haitokani na hao covid 19, ruzuku inakokotolewa kutokana na idadi ya kura alizopata mgombea Urais na idadi ya wabunge wa kutoka majimboni.
 
Kama CDM wangekuwa makini wangeomba tafsiri ya Mahakama kuhusiaana na uhalali wao kuwakilisha chama wakati si wanachama.
Nafikiri hilo litafuata baada ya Baraza Kuu kusikiliza rufaa yao, kwani hadi sasa Chadema hawajamuandikia Spika na NEC juu ya fate yao kwa vile mchakato wa kuwafukuza haujakamilika.
 
Ili uwadhihirishie hao CHADEMA kuwa wewe siyo MPUMBAVU,wawekee na udhibitisho hapa jamvini kua wanapokea ruzuku,hawajui kua wewe una akili sana,hebu wafanyie waone,ikiwezekana kama wewe ndo uliwapa ruzuku,wadhihirishie fasta,hawa CHADEMA wanazingua.
Umeshalifukuza hilo bumunda halielewi lipo lipo tu.
 
Sasa hao walikata rufaa ya nini kama tayari wanakimbilia bungeni wakati rufaa yao haijasikilizwa.

Hapo sasa ndipo baraza kuu likae na liwafukuze kabisa ndio waje wawe wabunge wa mahakama. Iweje leo Magufuli awang'ang'anie wakati alisema wapinzani ndio wanazuia maendeleo.!
Baraza Kuu, walikuwa wanawavizia tu akina Halima. Hawakutaka kukutana, mpaka ujanja na uchu wa kuutaka Ubunge ufike mwisho. Kwa sasa sina shaka litakutana na kubariki kufukuzwa kwao.
Sasa, ngoja tuone baada ya baraka hizo, na kukimbilia Mahakamani, tusubiri yaliyokuwa yanahubiriwa jana kwenye siku ya sheria kuhusiana na kesi ziwe zinachukua muda mfupi, kama itatekelezwa!
 
Back
Top Bottom