Wabunge kugawiwa mitungi ya Gesi linaleta ukakasi mkubwa. Je, haiwezi kuwa rushwa au waziri kutafuta kukubalika?

Wabunge kugawiwa mitungi ya Gesi linaleta ukakasi mkubwa. Je, haiwezi kuwa rushwa au waziri kutafuta kukubalika?

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
1,856
Reaction score
2,417
Wadau hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku ya kulijenga taifa letu.

Kwanza niunge mkono juhudi za serikali na wadau mbalimbali wa mazingira ktk nishati safi ya kupikia

Wakuu najiuliza majukumu ya wabunge ni yapi na je wamefanikiwa yote Hadi wapewe jukumu lingine la kugawa gesi kwa wananchi.

Ndani ya nchi yetu Kuna wadau wengi sana wa mazingira wenye elimu ya mazingira na wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutoa elimu kwa jamii kwanini serikali isishirikiane nayo.

Lakini pia kwenye halmashauri zetu naamini Kuna maafisa au kamati za mazingira, kwa nini waziri asishirikiane na viongozi wa halmashauri na wadau katika ugawaji na utoaji wa elimu endelevu.

Nafikiri hata spika ameona huo ukakasi ndo maana akafununua bila kuombwa ufafanuzi tena akajibu maswali yalipaswa kujibiwa na waziri mwenye dhamana.

Bado naendelea kuangalia maamuzi mbalimbali ya mhe January Makamba kama ndani yake Kuna Nia njema
Je Waziri akikosea kesho wabunge watakua na ujasiri wa kutosha kumkosoa?
 
Mbona nimeona Mkuu wa Mkoa wa Singida akigawa mitungi ya gas Kwa mama Lishe?

Serikali imeanzisha sera ya Nishati safi ,sio tuu mitungi Bali watahawa majiko banifu 200,000
 
Mbona nimeona Mkuu wa Mkoa wa Singida akigawa mitungi ya gas Kwa mama Lishe?

Serikali imeanzisha sera ya Nishati safi ,sio tuu mitungi Bali watahawa majiko banifu 200,000
Soma hoja yangu I uilewe kwanza mkuu,

Nazungumzia wabunge wenye jukumu kubwa la kuisimamia kuishauri na hata kuikosoa serikali kupitia mawaziri wenye dhamana. Leo waziri mmoja anawagawia mitungi ya gas kwa utaratibu wenye ukakasi vile,
Wakati serikali ina mifumo yake maafisa wake kila halmashauri Tena wa kudumu. Hivi kila waziri akitumia huo utaratibu itakuwaje.

Waziri wa kilimo naye awape wabunge mifuko 100 ya mbolea na mwingine naye hivyo hivyo
Itakuwaje. Jitahidi kuelewa kwanza hoja mkuu.
 
Ni rushwa + cashe wamepewa ya 10M kila mmoja
Kama ni kweli itakuwa jambo la aibu sana mkuu,

Kwa maoni yangu naona hiyo inaweza kuwa dharua kubwa kwa muhimili wa bunge lenye watu mia tatu kushindwa kung'amua Hila ya waziri. Kila siku tunapiga kelele kutengenisha mihimili Serikali na bunge. Leo naona kama bunge linataka kuingizwa kwenye mtego wa waziri wa serikali.
 
Hii awamu ya sita naona ndio imezidi kuonesha udhaifu wa Makamba kiuongozi, hana ubunifu wowote, anadeka na kudekezwa tu, kadri anavyozidi kuachwa, ndio anazidi kuonesha udhaifu wake mkubwa na mamlaka yake ya uteuzi kifikra.
 
Soma hoja yangu I uilewe kwanza mkuu,
Nazungumzia wabunge wenye jukumu kubwa la kuisimamia kuishauri na hata kuikosoa serikali kupitia mawaziri wenye dhamana
Leo waziri mmoja anawagawia mitungi ya gas kwa utaratibu wenye ukakasi vile ,
Wakati serikali ina mifumo yake maafisa wake kila halmashauri Tena wa kudumu
Hivi kila waziri akitumia huo utaratibu itakuwaje
Waziri wa kilimo naye awape wabunge mifuko 100 ya mbolea na mwingine naye hivyo hivyo
Itakuwaje
Jitahidi kuelewa kwanza hoja mkuu
Mkuu bajeti ya Tanzania hauhitaji kuhonga Ili ipitishwe unless wangekuwepo wapinzani ndio utasema wanahongwa Ili "wasiongee".

Katiba yetu inasema bajeti ikikataliwa na wabunge basi Rais anaweza kulivunja bunge. So utaona hata hao CCM huwa wanakosoa weeeh ila anamalizia kwa kusema "Naunga mkono hoja" na utasikia"Nimeachia shilingi". Sasa mazuzu kama hao wanaobanwa na katiba uwahonge kwa kazi Gani?

Huo ni ufisadi kama ulivyo ufisadi wa kutumia Mali za umma kujinufaisha wenyewe ila sio rushwa sababu katiba HAIRUHUSU kupinga bajeti yoyote yule..
 
Hiyo ni rushwa ya wazi wazi.
Kwa nini asubiri mpaka siku anawasilisha bajeti ya wizara yake bungeni ndiyo atoe hiyo mitungi? Huhitaji kuwa mpiga ramli kujua kuwa hiyo ni rushwa.
 
Back
Top Bottom