Wabunge matajiri wafanyabiashara, wanasimamia Maslahi ya akina nani bungeni?

Ukichunguza vizuri hata magu aliutaka ubunge na urais kwa ajili ya madili yake.

Jiulize uwanja wa chato ulijengwa na kampuni ya nani.
 
Maslahi ya masikini !
My word ! My foot !
🙏🙏😎
 
CCM NYERERE ILIKUWA INAWAPISHA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI KUWA WABUNGE LAKINI BAADA YA NYERERE KUNG'ATUKA ILAZALIWA CCM MATAJIRI NA WANYABIASHARA AMBAYO INASIMAMIA MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO
 
Mwalimu ana hela ya kufanya kampeni?
Mwalimu hana uwezo wa kushinda kampeni, kama hana chanzo cha ziada cha kuwapa wapiga kura, kuanzia chama chake cha siasa na gharama za uchaguzi zilivyo..... Siasa ni uwekezaji sasa , hakuna cha kutumikia wananchi au nini
 
Mfanyabiashara tajiri mwenye vituo vya mafuta Nchi nzima, anagombea ubunge na kuacha kusimamia biashara zake Ili akae bungeni na kulipwa 80,000 Kwa siku, ni ana mapenzi na wananchi au Kuna nini nyuma yake?
Natamani ningekuwa na access na uwezo wa kuchora katuni
Hili ningechora mwananchi amekondaa analipa nauli kubwa alafu hela inaenda kwa yule aliyemwambia kanisaidie kuomba nauli ipungue. Halafu aliyeenda kuomba nauli ipungue alipofika sehemu husika kakaa anakunywa soda kwenye mrija na ana likitambi flani hivi
 
Uzi ufungwe. Hili ndo jibu
Ikiwa hili ndilo jibu,

Umma wa wananchi Walio wengi wakulima na wafanyakazi, wamchague viongozi watakaokwenda kupigana Maslahi ya wananchi ,Si maslah binafsi.

Tuwe macho uchaguzi ujao 2024&2025.
 
Wananchi tupambane kuhakikisha tunachagua viongozi watakaokwenda kutetea Maslahi ya wananchi wengi wa MAISHA ya chini,

Si Hawa wenye kwenda kutetea Maslahi ya matajiri na kujiongezea ukwasi.
 
CCM NYERERE ILIKUWA INAWAPISHA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI KUWA WABUNGE LAKINI BAADA YA NYERERE KUNG'ATUKA ILAZALIWA CCM MATAJIRI NA WANYABIASHARA AMBAYO INASIMAMIA MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO
Ikiwa tutakosa tumaini ndani ya CCM iliyoasisiwa na Nyerere, tuchague upinzani, wasiotununua Kwa pesa.

Tuangalie akili na wenye Nia ya kututumikia.
 
Ikiwa huo ndio UKWELI,

Tujitahidi wasirudi bungeni.

Tunahitaji mtu mwenye maono asimamie Maslahi ya wananchi wote Ili wapate fursa sawa katika JAMII.
Wanalinda biashara zao. Mabasi ya hawa hakuna askari wa barabarani anayethubutu kuyasimamisha.

Kampuni/biashara zao hakuna ofisa wa tra anayepeleka pua yake.
 
Wanalinda biashara zao. Mabasi ya hawa hakuna askari wa barabarani anayethubutu kuyasimamisha.

Kampuni/biashara zao hakuna ofisa wa tra anayepeleka pua yake.
Kwa kuwa Wabunge Hawa, hawawakilishi maslah ya umma wa wananchi,

Tuhakikishe hawarudi bungeni,

Tupate wananchi wenye maono watakaokubali kutumwa KAZI na wananchi na kutetea Maslahi ya wananchi.

Tukiwakosa CCM, tusisite kuchagua wa upinzani ikiwa wanafaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…