Wabunge matajiri wafanyabiashara, wanasimamia Maslahi ya akina nani bungeni?

Fuatiliq jinsi maseneta wa Marekani walivyo matajiri na wanavyofaidika na inside trading wakiwa bado wabunge.
Sheria zao ni Kali,

Hukatazwi kuwa mfanyi biashara, bt kutumia uongozi kutafuta personal gains Sheria zao ziko tight sana.

Trump tumeona akibanwa na analipa Kodi,

Vp huku kwetu?
 
Ukiwa mbunge nchi masikini halafu una hela basi ujue unatafuta fursa za kujuana na mawaziri wa kila wizara unayotaka kufanya biashara

Utapata Tenda za kila aina na kwa marejesho unampa waziri % katika biashara zako au na yeye anazungusha hela chafu humo humo

Kuwa mbunge Nigeria au popote ni fursa ambazo sio halali kabisa
Ndio maana corruption haziishi Africa
 
Sheria zao ni Kali,

Hukatazwi kuwa mfanyi biashara, bt kutumia uongozi kutafuta personal gains Sheria zao ziko tight sana.

Trump tumeona akibanwa na analipa Kodi,

Vp huku kwetu?
Hata zamani maseneta wa Rome hawakuruhusiwa kufanya biashara. Lakini ndiyo walikuwa matajiri na wenye kunufaika na vyeo vyao hivyo.

Hizo sheria hata kwetu zipo za kutotumia cheo kujinufaisha zipo.
 
Kuingia bungeni hao wafanyabiashara huweka Ubunge kama ndo bima yao ya maisha.

Nafikiri utaelewa.
 
Hata zamani maseneta wa Rome hawakuruhusiwa kufanya biashara. Lakini ndiyo walikuwa matajiri na wenye kunufaika na vyeo vyao hivyo.

Hizo sheria hata kwetu zipo za kutotumia cheo kujinufaisha zipo.
Ndo tunajiuluza, ikiwa hizo Sheria zipo vizuri,

Musukuma au Abuud, amemkabidhi nani biashara zake Ili tuamini kuwa, hatumii Cheo chake kuhakikisha nauli zinapanda na hatetei tena wananchi, WALIO Abiria wake Kwa wakati huo huo.
 
Kuingia bungeni hao wafanyabiashara huweka Ubunge kama ndo bima yao ya maisha.

Nafikiri utaelewa.
Ubunge unakuwaje bima ya maisha ya Wabunge matajiri Wafanyabiashara?
 
Ni kweli, hiyo huwasaidia khasa kufanya lobbying na kutafuta business opportunties.

Na si Tanzania tu huo ndo mfumo wa dunia ulivyo mwenye pesa hutamba.

Lakini wenzetu huweka maslahi ya majimbo yao kwanza huku wakiendelea na biashara zao.

Ila wengi ni wabunge wa kawaida sana na ndo wale ambao huwa na second jobs au second home kupata kipato cha kujiongeza.

Wabunge kama Msukuma au Bashe na wengine si wana biashara zao ambazo hazilingani na biashara za yule mbunge mwarabu mwenye mabasi lukuki?

Lakini wote hukimbilia kuwa wabunge kujilinda.
 
"Siasa Hulinda utajiri" Mwisho wa Kumnukuu Daniel Arap Moi Rais wa Pili wa Kenya
 
Ubunge unakuwaje bima ya maisha ya Wabunge matajiri Wafanyabiashara?
Kuna kitu chaitwa Collateral wakifahamu hichi?

Ndo maana hutumia njia hiyo ya ubunge kama bima dhidi ya "sudden event" ikitokea.
 
"Siasa Hulinda utajiri" Mwisho wa Kumnukuu Daniel Arap Moi Rais wa Pili wa Kenya
If that is the case,

Wananchi tuwakatae matajiri na Wafanyabiashara wanataka nafasi za kisiasa wasiosimamia maslah ya wananchi.

Ikiwa wamo bungeni, tuhakikishe hawarudi bungeni 2025.
 
If that is the case,

Wananchi tuwakatae matajiri na Wafanyabiashara wanataka nafasi za kisiasa wasiosimamia maslah ya wananchi.

Ikiwa wamo bungeni, tuhakikishe hawarudi bungeni 2025.
Kuwakataa ni vigumu kwani wengi wao ndo wachangiaji wakubwa au donors wa chama kinotawala.
 
Kuwakataa ni vigumu kwani wengi wao ndo wachangiaji wakubwa au donors wa chama kinotawala.
Ikiwa wameteka chama tawala,

Tuchague upinzani.

Na ndio hasa Siri ya kwanini wagombea wa upinzani Huwa Wana nguvu sana ya kukubalika na wananchi, hata kama hawatumii pesa kuhonga.
 
Maslahi ya wote! πŸ˜„
Ila umaskini siyo mzuri hata kdg, kwa hiyo km tajiri anaweza kuwa kiongozi mzuri naona ni ahueni ili asaidie jamii.
 
Haswa, hii ni kila mahali na kama ulivyosema kwa wenzetu wanajilinda sana na wanaangalia maendeleo ya majimbo yao
Hata wao kama wazungu unaweza kuta ana Ubunge zaidi ya miaka 30
 
Hilo halina shida lakini je, mazingira yaruhusu na wapiga kura wana nia ya kweli ya kuchagua wapinzani?
Nia IPO kabisa.

Na wananchi Si wajinga,

Ndomana pamoja na kuhonga katika uchaguzi, Huwa haitoshi kupata kura,

Wanalazimika pia kuiba na kuweka kura fake.
 
Maslahi ya wote! πŸ˜„
Ila umaskini siyo mzuri hata kdg, kwa hiyo km tajiri anaweza kuwa kiongozi mzuri naona ni ahueni ili asaidie jamii.
Tajiri kuwa mbunge si tatizo,

Tatizo ni kuendelea na biashara akiwa mbunge.

Tatizo ni kutumia ubunge kulinda biashara zake na kukwepa Kodi sababu ana access na mawaziri na viongozi wa Serikali Kwa ukaribu.

Umeelewa?
 
Maslahi ya wote! πŸ˜„
Ila umaskini siyo mzuri hata kdg, kwa hiyo km tajiri anaweza kuwa kiongozi mzuri naona ni ahueni ili asaidie jamii.
Pia unatakiwa ujue kuwa,

Mbunge tajiri na mfanyabiashara, Huwa hatumii pesa yake mfukoni kujenga shule au kujenga hospitali au kununua madawa,

Pesa inayotumika ni pesa ya Kodi zetu,

Hivyo wananchi tuchague viongozi Bora , brains, bila kujali viwango vyao vya pesa.

Uzalendo , uadilifu ziwe sifa mojawapo katika kuwapima viongozi.
 
Uko sawa lakini je, wananchi ni waelewa?

Na kama ni waelewa basi mwaka 2025 uwe mwaka wao wa kuonyesha ukomavu wa kiakili kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
 
Uko sawa lakini je, wananchi ni waelewa?

Na kama ni waelewa basi mwaka 2025 uwe mwaka wao wa kuonyesha ukomavu wa kiakili kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
Wananchi ni waelewa,

Ingawa viwango vya uelewa vinatofautiana,

Ndio sababu sisi tuliobahatika kupata uelewa kidogo, tunatumia uelewa huo kidogo Kutoa ELIMU ya uraia ambayo ni HAKI ya wananchi ambayo Watawala wasingependa wananchi waipate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…