Wabunge/ Mbunge akijirekodi faragha anaweza kupoteza Ubunge wake?

Wabunge/ Mbunge akijirekodi faragha anaweza kupoteza Ubunge wake?

Umeuliza jambo la maana sana lakini binafsi sitatoa jibu la moja kwa moja ila tunatakiwa tutafakari kwa pamoja.

Umetumia neno "faragha" au kwa kiingereza "privacy" na hapa ndipo msingi wa majadiliano yangu.

watanzania tukijua maana ya faragha hatutakuwa na maswali mengi na kwa bahati mbaya ukiijua faragha ya mtu hutaitumia kumdhalilisha bali utahifadhi faragha yake.

Ni nani anayetoa hiyo faragha ya mbunge? Ni yeye mwenyewe anaiweka Whatsapp,Telegram,Insta au FB? Kama ni yeye mwenyewe anapost katika account yake hilo ni kosa inabidi alibebe.

Kuna fundi simu na wa computer amabo ukiwapelekea chombo chako wanakagua faragha zako na wanazihamishia kwao,hawa ndio wengi na inabidi washughulikiwe.

La mwisho pamekuwa na wimbi la Polisi wakikamata watu maarufu wanakimbilia kuchukua simu zao na Computer, hawa ni watu wanatakiwa wafanyiwe mjadala wa kina na tuelezwe kuhusu wakikuta faragha za mtuhumiwa wanazifanyia nini?

Tuheshimu faragha za watu, ndio ustaarabu. Tumepiga hatua kutokupiga picha maiti au ajali na naamini katika hili nalo tutafanikiwa.
Kama simu za watu zilirekodiwa na sauti zao kuwekwa hadharani tena viongozi wakubwa kabisa itakuwa hizo.
 
Heeeh kumekucha sas lol, mwageni mchele sie tudonoe.
 
Tunaogopa kuwatumia wengine ma Mwela tu humu kibao
 
Wapo wamejirekodi
Kuna wabunge ambao wamewatengenezea video ya ngono sasa wanataka kuwalipua!!!! Hizi video za kuumba kama hatutakuwa makini watu wengi wataumizwa!!! Kwenye jamii ambayo haijaelimika na hivyo kuamini kila kitu kiwekwacho kwenye mitandao bila kuchunguzwa hii italeta hatari sana.
 
Back
Top Bottom