moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,904
- 4,902
Wanabodi,
Nimesikitishwa sana na kitendo cha yule Mbunge juzi kutoa hoja ya wao wabunge waongezewe mishahara maana wana kazi nyingi sana.
Kama hilo halitoshi Mbunge yule ameenda mbali akisema hata malipo ya mishahara yao yafanyike kwa malipo ya dola za kimarekani. Kwa jinsi hasira zilivyokaba sikutaka kujua jina la Mbunge wala jimbo lake na wananchi wake anaowawakilisha.
Ifike hatua wabunge waache "ubinafsi" Miaka nenda rudi wamekua wakitumia nafasi zao kama watunga sheria..wakitunga sheria zinazowapendelea wao kwenye suala la malipo.
Leo hii mshahara wa Mbunge haukatwi kodi yeyote. Mbunge anapata posho (allowances) ya laki tatu kwa kila kikao anachoingia. Na anaweza akaja akasaini akaondoka asikae mpaka mwisho au anaweza akahudhuria na akakaa kimya mpaka kikao kikaisha.
Wabunge wengi wamekaa tu pale,wakipigwa na Viyoyozi huku wakiwa wamesinzia. Kweli mshahara wa 12 millions ambao hauna statutory deductions nyie hauwatoshi?
Kweli posho ya laki 3 kwa kila kikao haziwatoshi? Kweli posho kwenye hizi standing committees za bunge nazo haziwatoshi? Hebu muogopeni MUNGU.
Sasa ni muda sahihi wa wabunge wote wanaoona mshahara wa Million 12 hauwatoshi WAACHIE NGAZI ili Young Graduates waje kushikilia nafasi hizo za ajira.
Nyie mmekaa hapo miaka zaidi ya mitano na hakuna mabadiliko yeyote kwenye majimbo. Sasa ni wakati muhimu Vijana wahitimu washike nafasi zenu.
ONDOKENI
Hivi ni Graduate gani ataacha mshahara wa 12M? Rais Samiah alisema kwenye hotuba ya men Mosi kwamba hatopandisha mishahara sababu nchi haina hela.
Uchumi umeshuka mpaka 04%, wewe ni nani wa kuomba uongezewe zaidi. Graduates, chukueni nafasi zao hawa wanasema 12M ndogo sana.