Wabunge msiotosheka na 12M, achieni ngazi young graduates wachukue nafasi zenu

Wabunge msiotosheka na 12M, achieni ngazi young graduates wachukue nafasi zenu

Hawa Wabunge wengepewa Toyota Corrola na la pili unapewa mwaka mmoja kama hudilivery katika jimbo lako unafukuzwa kutokana na ahadi ulizotoa nafikiri jeuri ingewatoka wanatakiwa watiwe pressure ya hali ya juu .Unajua kwenye Bunge kuna pesa ndio maana kila mtu anapigania kuwa mbunge plus hakuna kazi yyote ni sehemu ya starehe na kuparty tu .
Kwa uhuru kabisa anakwambia yeye mpaka anaingia bungeni katumia 72m lakini kunawengine wapo wametumia mpaka 600m [emoji846][emoji846][emoji846].

Nilivyomsoma anataka 72m zake zirudi na faida juu as if kapanda shamba anategemea mavuno na faida wakati aliapa kuwa anakwenda kuwatumikia wananchi as long as kazi ni ya hasara au faida.

Binafsi sijawahi kuona mtu anaomba kufanya kazi, anakuta haimlipi au haimpi hitaji lake anaendelea kubaki hapohapo wakati anajitanabaisha kuwa ananyenzo nyengine zinazomuingizia kipato.

Kweli Tanzania tunasafari ndefu na wabunge wa aina hii.!!
Ndio maana hata sikushangaa SUGU alivyoimba kwenye wimbo wake ule wa freedom yuko na Mr Blue anasema kila siku kwenye account yake akiangalia kunamamilioni
 
Wanabodi,
Nimesikitishwa sana na kitendo cha yule Mbunge juzi kutoa hoja ya wao wabunge waongezewe mishahara maana wana kazi nyingi sana.
Kama hilo halitoshi Mbunge yule ameenda mbali akisema hata malipo ya mishahara yao yafanyike kwa malipo ya dola za kimarekani.

Kwa jinsi hasira zilivyokaba sikutaka kujua jina la Mbunge wala jimbo lake na wananchi wake anaowawakilisha..

Ifike hatua wabunge waache "ubinafsi "......

Miaka nenda rudi wamekua wakitumia nafasi zao kama watunga sheria..wakitunga sheria zinazowapendelea wao kwenye suala la malipo.

Leo hii mshahara wa Mbunge haukatwi kodi yeyote.

Mbunge anapata posho (allowances) ya laki tatu kwa kila kikao anachoingia.

Na anaweza akaja ..akasaini akaondoka asikae mpaka mwisho au anaweza akahudhuria na akakaa kimya mpaka kikao kikaisha.

Wabunge wengi wamekaa tu pale,wakipigwa na Viyoyozi huku wakiwa wamesinzia.

Kweli mshahara wa 12 millions ambao hauna statutory deductions nyie hauwatoshi?

Kweli posho ya laki 3 kwa kila kikao haziwatoshi???

Kweli posho kwenye hizi standing committees za bunge nazo haziwatoshi?

Hebu muogopeni MUNGU..

sasa ni muda sahihi wa wabunge wote wanaoona mshahara wa Million 12 hauwatoshi WAACHIE NGAZI ili Young Graduates waje kushikilia nafasi hizo za ajira.

Nyie mmekaa hapo miaka zaidi ya mitano na hakuna mabadiliko yeyote kwenye majimbo.

Sasa ni wakati muhimu Vijana wahitimu washike nafasi zenu...

ONDOKENI .

Hivi ni Graduate gani ataacha mshahara wa 12M??????

Rais Samiah alisema kwenye hotuba ya men mosi kwamba hatopandisha mishahara sababu nchi haina hela.

Uchumi umeshuka mpaka 04% ,wewe ni nani wa kuomba uongezewe zaidi.

Graduates, chukueni nafasi zao hawa....wanasema 12M Ndogo sana.
Young Graduates wanazengua!
 
Kwa uhuru kabisa anakwambia yeye mpaka anaingia bungeni katumia 72m lakini kunawengine wapo wametumia mpaka 600m [emoji846][emoji846][emoji846].

Nilivyomsoma anataka 72m zake zirudi na faida juu as if kapanda shamba anategemea mavuno na faida wakati aliapa kuwa anakwenda kuwatumikia wananchi as long as kazi ni ya hasara au faida.

Binafsi sijawahi kuona mtu anaomba kufanya kazi, anakuta haimlipi au haimpi hitaji lake anaendelea kubaki hapohapo wakati anajitanabaisha kuwa ananyenzo nyengine zinazomuingizia kipato.

Kweli Tanzania tunasafari ndefu na wabunge wa aina hii.!!
Ndio maana hata sikushangaa SUGU alivyoimba kwenye wimbo wake ule wa freedom yuko na Mr Blue anasema kila siku kwenye account yake akiangalia kunamamilioni
Kutumia 72m au kutumia 600m sisi haituhusu....
Hizo ni rushwa na takrima ni zake na wapiga kura wake .....

Sisi tunachojua kikatiba ni moja ya watu wanaolipwa vizuri kwa less qualifications zao .....

Kujua kusoma na kuandika.
Kwenda pale kutunga sheria, kupitisha sheria na kuishauri serikali.

Hizi kazi haziendani na malipo ya 12m..

Wabunge wako 300+ unakuta mpaka bunge limaisha Mbunge hajafungua bakuli lake kuongea labda awe waziri.

Imagine inafika alhamisi kwenye maswali ya papo kwa papo kwa PM ,Mbunge anasema hana swali.

Imagine unasikiliza Mbunge akiishauri serikali utalia...wengi wana ushauri hata ukisililiza unaweza kulia.
 
Haya ndo madhara ya kupeleka wabunge wa mbeleko, wabunge waliochaguliwa kihalali na wananchi hawawezi ku-behave kindezi ndezi namna hii...
 
Haya ndo madhara ya kupeleka wabunge wa mbeleko, wabunge waliochaguliwa kihalali na wananchi hawawezi ku-behave kindezi ndezi namna hii...
Kwenye swala la pesa wabunge wote akili yao ni moja wawe CCM au UPINZANI wanachojali ni matumbo yao tu
 
.... DC ni mhimili mwingine na Bunge ni mhimili mwingine.
Uko sahihi....ni mihimili miwili tofauti.

Na muhimili wa Bunge ndo wenye dhamana ya kutunga na kupitisha serikali.

So,wanaweza wakaibua hoja ya kimaslai kwao ,mfano hoja ya kuongezewa malipo then bunge hilo hilo likaacha agenda muhimu zingine za kitaifa na wakajikita kujadili hoja yao ya malipo.

Ikajadiliwa...na sitoshangaa wakaipitisha .

Hao ndo wabunge....
 
Back
Top Bottom