Wabunge msiotosheka na 12M, achieni ngazi young graduates wachukue nafasi zenu

Kwa uhuru kabisa anakwambia yeye mpaka anaingia bungeni katumia 72m lakini kunawengine wapo wametumia mpaka 600m [emoji846][emoji846][emoji846].

Nilivyomsoma anataka 72m zake zirudi na faida juu as if kapanda shamba anategemea mavuno na faida wakati aliapa kuwa anakwenda kuwatumikia wananchi as long as kazi ni ya hasara au faida.

Binafsi sijawahi kuona mtu anaomba kufanya kazi, anakuta haimlipi au haimpi hitaji lake anaendelea kubaki hapohapo wakati anajitanabaisha kuwa ananyenzo nyengine zinazomuingizia kipato.

Kweli Tanzania tunasafari ndefu na wabunge wa aina hii.!!
Ndio maana hata sikushangaa SUGU alivyoimba kwenye wimbo wake ule wa freedom yuko na Mr Blue anasema kila siku kwenye account yake akiangalia kunamamilioni
 
Young Graduates wanazengua!
 
Kutumia 72m au kutumia 600m sisi haituhusu....
Hizo ni rushwa na takrima ni zake na wapiga kura wake .....

Sisi tunachojua kikatiba ni moja ya watu wanaolipwa vizuri kwa less qualifications zao .....

Kujua kusoma na kuandika.
Kwenda pale kutunga sheria, kupitisha sheria na kuishauri serikali.


Hizi kazi haziendani na malipo ya 12m..

Wabunge wako 300+ unakuta mpaka bunge limaisha Mbunge hajafungua bakuli lake kuongea labda awe waziri.

Imagine inafika alhamisi kwenye maswali ya papo kwa papo kwa PM ,Mbunge anasema hana swali.


Imagine unasikiliza Mbunge akiishauri serikali utalia...wengi wana ushauri hata ukisililiza unaweza kulia.
 
Haya ndo madhara ya kupeleka wabunge wa mbeleko, wabunge waliochaguliwa kihalali na wananchi hawawezi ku-behave kindezi ndezi namna hii...
 
Haya ndo madhara ya kupeleka wabunge wa mbeleko, wabunge waliochaguliwa kihalali na wananchi hawawezi ku-behave kindezi ndezi namna hii...
Kwenye swala la pesa wabunge wote akili yao ni moja wawe CCM au UPINZANI wanachojali ni matumbo yao tu
 
.... DC ni mhimili mwingine na Bunge ni mhimili mwingine.
Uko sahihi....ni mihimili miwili tofauti.

Na muhimili wa Bunge ndo wenye dhamana ya kutunga na kupitisha serikali.

So,wanaweza wakaibua hoja ya kimaslai kwao ,mfano hoja ya kuongezewa malipo then bunge hilo hilo likaacha agenda muhimu zingine za kitaifa na wakajikita kujadili hoja yao ya malipo.

Ikajadiliwa...na sitoshangaa wakaipitisha .

Hao ndo wabunge....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…