tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Ili kupata fedha za kununua dawa kwa wagonjwa wa UKIMWI, ukoma na kifua kikuu, watawala wa CCM wameamua kuwakamua raia mamilioni ya shilingi. Licha ya kuwa tayari wananchi wanaendelea kukamuliwa tozo za trab and tat baada ya kushindwa kuhamia Burundi, bado serikali ya CCM hairidhiki. Inataka iendelee kuwakamua wanyonge hadi tome la mwisho la damu. CCM ni kama mfugaji mpumbavu asiyemlisha ng'ombe wake lakini kila siku utamkuta amening'inia kwenye chuchu anakamua.
Juzi kati wamewavuruga wahisani na kujikuta kunyimwa misaada na USAID huku wakitamba kuwa nchi bado ina pesa za kutosha, kumbe walikuwa wanaringia fedha za walalahoi! Watawala wa nchi hii wamerogwa sio bure.
Wakati wananchi wakizidi kukamuliwa bila huruma, wabunge walioteuliwa na CCM kuingia bungeni kwa nguvu ya dola, wanalipwa mabilioni ya shilingi bila kujali umaskini wa wananchi wanaojidai kuwawakilisha. Kana kwamba hilo halitoshi, imedokezwa kwamba kila mwananchi mwenye atalazimika kukamuliwa Tsh 1000 kwa siku kupitia makato ya simu ili kuchangia mfuko wa bima ya afya kwa wote (NHIF) ambao Samia aliahidi kuutekeleza ndani ya siku 100 za utawala wake. Hii maana yake ni kwamba kwa mwezi mmoja kila mtanzania atakamuliwa Tsh 30,000 atake asitake.
Tukumbuke mwaka uliopita baada ya bunge la 12 kuvunjwa, serikali ya CCM imelipa jumla ya Tsh trilioni 139 kama mafao kwa wabunge, ambapo kila mbunge alinyonya Tsh 400,000,000 cash akaondoka nazo na kuiacha hazina ikiwa tupu. Ndio maana sasa wanahaha kutafuta fedha kwa kuwakamua wananchi hadi damu ilmradi wao malengo yao ya kujineemesha kiuchumi yamekamilika.
Pamoja na magumu yote wanayopitia wananchi, kila mwezi serikali hutumia matrilioni ya shilingi kuwalipa mafao wenza wa viongozi licha wao wenyewe ya kulipwa 80% ya mishahara yao ya zamani. Ujinga huu ulipendekezwa na mama Salma Kikwete na kupitishwa kwa kura zote na bunge tukufu la CCM. Mmojawapo wa watu wanaolipwa matrilioni haya ni Tulia Ackson ambaye pia mume wake ameanza kulipwa mafao baada ya mke wake (Tulia) kustaafu. Na pia wake wawili wa marehemu Job Ndugai kila mmoja analipwa 80% ya mshahara wa Ndugai alipokuwa spika. Hawa watu peke yao wanatafuna zaidi ya nusu ya pato la taifa lakini utashangaa wachumiatumbo kama MamaSamia2025, Lucas Mwashambwa , Lucas mwashamba , ChoiceVariable na wapumbavu wengine wanakuja hapa kutetea uhujumu huu wa uchumi unaofanywa na CCM.
MAONI YANGU
Wakati umefika sasa wabunge na wenza wa watawala waachie walau robo ya mafao yao ili yaende kununulia dawa za UKIMWI na kutunisha mfuko wa bima ya afya kwa wote (NHIF) badala ya kuendelea kuwakamua raia wanyonge wanaopambana kila kukicha kutafuta pesa za kula walau mlo mmoja kwa siku. Hivi hawa jamaa huu utajiri wanaokusanya kwa kuchota pesaza umma zinazotokana na kodi za wanyonge zitawapeleka mbinguni? Inauma sana kuona jinsi wananchi wanyonge wanavyohujumiwa hazina yao na kundi dogo la walafi wenye roho za kutoshiba kama mafisi.