saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
HILI suala la mikopo tusipoliangalia litugawa kama Taifa, alianza Ndugai tukaona ni utani akapoteza nafasi ya Uspika, akaja kulizungumzia bungeni Luhaga Mpina naye akapoteza nafasi ya kuteuliwa kugombea nafasi ya NEC aliyoomba kupitia CCM.
Akazungumza tena bungeni Oran Njeza Mbunge wa Mbeya Vijiji naye hatujui nini kitamkuta, Mbunge wa Viti Maalum Hawa Mchafu anaye alizungumzia, majuzi kalizungumzia Gerald Hando naye anasakamwa mitandaoni.
Leo Mbunge Mariam Ditopile naye amelizungumzia ila kwa upande wa kutetea kwamba halina madhara na miradi inatekelezwa.
Ushauri kwa wabunge Bunge lijalo la Januari 2023 muunganishe nguvu za pamoja kuitaka Serikali iwasilishe taarifa bungeni ya mikopo yote iliyopokelewa mwaka 2022 na miradi iliyokwenda kutekeleza kwa mchanganuo mahususi ya kila mradi ili kuondoa sintofahamu inayoendelea kwenye taifa kuhusu mikopo.